Waziri wa Fedha na Waziri wa Ujenzi, msijisahaulishe kuweka ahadi ya barabara za jimbo la Kibamba aliyotoa JPM (RIP) wakati akizindua stand ya mbezi

Kwasenga

Member
Feb 24, 2021
27
45
Kwa kuwa kila anayesimama anasema tutamuenzi kiongozi wetu Hayati JPM, basi waziri wa ujenzi na yule wa fedha msije kusahau kuwa kabla ya umauti kumkuta mzee wetu alikuwa ameagiza TANROAD kuanza kushughulika na barabara za jimbo la Kibamba kwa maana ni jimbo pekee ndani ya Dar ambalo lina chini ya asilimia 5 tu ya barabara za lami.

Kati ya hizo asilimia nadhani zitakuwa zinabebwa na barabara ya Morogoro, kipandw kidogo cha kwenda Muloganzila, sehemu ya barabara ya kwenda kinyerezi, sehemu ya barabara ya goba, pamoja na ka kipande ka kwenda maji ya chumvi.

Yaani ndo jimbo lenye barabara mbaya kuliko zote za mkoa wa Dar. Basi kama tunamuezi JPM, tunategemea kuona mambo ya barabara za Kibamba yakianza mapema iwezekanavyo baada ya bajeti.
 
Omera Yawa

JF-Expert Member
May 5, 2016
954
1,000

hasa Barabara ya Maji chumvi muhimu sana inasaidia sana kuepuka foleni za buguruni na tabata
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom