Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mpango anapaswa kujibu swali la Hawa Mchafu kwa vitendo

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
Nimekutana na clip ya sessions za bunge kuhusu swali tata lakini genuine la Hawa Mchafu ambalo limehoji very specific kwa nini fedha za dawa na fedha za deni la MSD hazijapelekwa kulipia dawa.

Swali hilo limejibiwa na Waziri wa afya ingawa majibu hayajajotosheleza sababu kubwa ya majibu kutojitosheleza ni kwa sababu mheshimiwa Hawa Mchafu ameuliza swali kwa wizara isiyohusika wizara inayotoa fedha ni wizara ya fedha na mipango chini ya waziri Mpango.

Hivyo ni muhimu swali hili lingejibiwa na wizara ya fedha na mipango kwa nini hawapeleki budgeted fund kwa Wizara ya Afya kama wanavyopeleka kwenye wizara nyingine?

Wizara ya Afya imepambana sana kuzuia upotevu na wizi wa dawa,imewaminya haswa watendaji wote ngazi ya wizara,mikoa na halmashauri kuhakikisha fedha na dawa zinakuwa salama lakini fact moja ya msingi ni kwamba wizara ya fedha na mipango haijatoa kipaumbele kwenye sekta ya afya kama ilivyojipangia.

Kutowapa fedha stahiki wizara ya afya kunapelekea malalamiko kwa wananchi,kuoneana ndani ya sekta ya afya na mengineyo yanayojiri.

Katika kipindi hiki cha kukabiliana na janga la corona ni vyema wizara ya fedha ikatambua na kutoa kipaumbele kwa wizara hii nyeti ya afya kwa kuwapa fedha zaidi za kuendesha shighuli za kawaida na shughuli za kukabiliana na dharura sio kupunguza fedha.

Mwenendo huu wa wizara ya fedha ambao umekuwa adopted hadi kwenye ngazi za halmashauri na vijiji unazorotesha sekta ya afya na kupelekea malalamiko na frustration kwa wananchi na watumishi wa afya.

Mawaziri wa afya hawawezi kulisemea hili ,watendaji wa afya hawawezi kulisemea hili kwa kuwa nature ya madaktari sio wanasiasa...but the truth should be said!!

Nampongeza SpikaNdugai kwa kutoa msisitizo kuwa swali la mh Mchafu ni national problem...hivyo naamini kama kiongozi wa bunge aje na azimio stahiki.

Fedha za bajeti ya afya zipelekwe sawia na fedha za elimu bure,bodi ya mikopo n.k

MH MPANGO AJIBU HOJA YA MBUNGE. HAWA MCHAFU.

BUNGE HILI NI LA WANACCM...BUNGE HILI LILETE GENUINE POINTS AND GENUINE SOLUTIONS.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AJIBU ILI KIRAHISISHA KAZI YA MAWAZIRI WENZAKE.
 
Sekta ya afya inaweza kujitegemea iwapo tutaweka mikakati na kutoa kipaumbele
 
Huu ni mwezi wa nane baada ya Mwaka rasmi wa serikali 2020/21 kuanza. Hadi Sasa fedha za serikali za mfuko wa afya ( Health sector busket fund) zimeota mbawa. Kinachohubiriwa sicho kinachoendelea kwa ground.
#Mitano Tena.
Hata ukipigwa mawe huu utabaki kuwa ukweli tu.
 
Huu ni mwezi wa nane baada ya Mwaka rasmi wa serikali 2020/21 kuanza. Hadi Sasa fedha za serikali za mfuko wa afya ( Health sector busket fund) zimeota mbawa. Kinachohubiriwa sicho kinachoendelea kwa ground.
#Mitano Tena.

Hii Ni kashfa au skendo kubwa... Kwa hiyo hizo pesa zimepigwa? Au zimeamishwa kwa matumizi mengine..
 
Back
Top Bottom