Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, kukata hela katika muda wa maongezi ni chanzo cha mapato

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
155
385
Kuna kitu ambacho sikielewi kwa hawa viongozi wetu hususani katika Muhimili wa Bunge, hawa wabunge hawalipi kodi yoyote katika posho zao na wanapokea posho nyingi tu ambazo hazina makato.

Lakini cha ajabu wanapopewa jukumu la kubuni vyanzo vya mapato kwao uwa ni mtihani mkubwa sana japokuwa kuna rasilimali nyingi sana hapa nchini, mara nyingi utasikia ongeza kodi katika sigara, Pombe, mara sijui mawigi yani wanafikiria katika vitu ambavyo sio sustainable.

Sasa hivi wameamia katika mitandao ya simu, kuna wakati Andrew Chenge alikuwa mwenyekiti wa kamati ya kubuni vyanzo vya mapato, unajua ni nini? Pamoja na usomi wake woote na kamati yake eti walibuni kuweka plate namba za majina binafsi alafu mtu analipia kwa mwaka milioni tano, sasa jiulize hawa ndio think tanker wa nchi ambao kazi yao ni kuvuta posho, lakini kwenye kufikiri namna ya kupata hizo posho ni zero kabisa.

Mwigulu anazungumzia juu ya watanzania walivyojitolea vitu mbalimbali katika vita ya Uganda, anasema watanzania wawe na mioyo ya kujitolea anasahau kuwa wabunge wake hawakatwi chochote katika posho zao, kama ni uzalendo wa kujitolea waanze wao wabunge kama mfano siio blah blah.

 
Wabunge wamejificha kwenye neno posho ili wasilipe kodi.

Napendekeza neno posho lifutwe na liwe mshahara. Na huo ndiyo utakuwa mwarobaini wao kutokulipana mamilioni lukuki bungeni.

KUMBUKA: posho haina kodi bali mshahara ndiyo hukatwa kodi.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom