Waziri wa Fedha, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha pamoja na Gavana hivi mna kinga ya kutoshitakiwa?

Watu hawa ni wa ajabu sana. CAG katoa tuhuma nzito sana ya shillingi 1.5 trillion kutojulikana ilikopotelea. Wahusika wote Serikalini wameamua kupiga kimya na kumpa jukumu la kujibu tuhuma hiyo nzito tumbili ambaye kwanza hayumo ndani ya Serikali na sijui ni nani aliyempa hilo jukumu ambalo si jukumu lake hata chembe.

Tunataka kumsikia jiwe kuhusu tuhuma hii nzito ya pesa nyingi sana za walipa kodi. Na ni akina nani waliowajibishwa kuhusu upotevu huo wa pesa nyingi sana.

Jiwe kuendelea kupiga kimya kuhusu tuhuma hii nzito ni kuonyesha dharau kubwa sana kwa CAG na walipa kodi wote nchini.
Dawa na sisi ni kuiba kwa kwenda mbele na tusiulizane. Inauma na kukera sana
 
Rais hana uwezo wa kumuondoa CAG
Kwa Serikali hii ya sasa, Bashite tu anaweza kumng'oa CAG. Wala haitohitaji kufika kwa malaika mkuu mtarajiwa. Sijawahi kuona CAG anatoka hadharani "kumuomba radhi Rais na waTZ kwa ujumla"
 
Kuna nafasi kwa aina hii ya utawala ukipewa kiungwana inabidi umwambie bwana mkubwa unashukuru ila 'No Thank you' maana ni za kushushiana pii!
Akikuambia kimya kimya sawa, ila akikutangaza hadharani huwezi kukataa uteuzi,, wengi walikuwa wanakataa mwanzoni, baadaye akaamua kuwa anattangaza bila kumshirikisha mteuriwa

Mfano hai ni katibu wake wa Chama
 
Akikuambia kimya kimya sawa, ila akikutangaza hadharani huwezi kukataa uteuzi,, wengi walikuwa wanakataa mwanzoni, baadaye akaamua kuwa anattangaza bila kumshirikisha mteuriwa

Mfano hai ni katibu wake wa Chama
Sikia mkuu...unaita press kutangaza nimemteua Horseshoe Arch fine nitaitika wito...kisha nami naita press yangu nasema namshukuru mheshimiwa sana mkuu asiyepangiwa na mtu kwamba hiyo nafasi amuongezee majukumu Bashite kisha nasepa zangu madibira kulima numbu na kuokota songwe nyikani huku nikiburudika na mijagi!
 
Sikia mkuu...unaita press kutangaza nimemteua Horseshoe Arch fine nitaitika wito...kisha nami naita press yangu nasema namshukuru mheshimiwa sana mkuu asiyepangiwa na mtu kwamba hiyo nafasi amuongezee majukumu Bashite kisha nasepa zangu madibira kulima numbu na kuokota songwe nyikani huku nikiburudika na mijagi!
Sidhani kama utafika madibira aisee
 
Walaaam,

Yaani kwa madudu haya yaliyoibuliwa na CAG wafuatao wajiandae kwenda jela inaweza isiwe leo,kesho au pengine hata kesho kutwa ila amini nawaambieni watakuja kufungwa tu tena kifungo kitakatifu.

Yaani watanzania wanateseka hivi kwa kukamuliwa na TRA kumbe wanawajusanyia pesa watu watatu au wanne hakika Mungu yupo na wananchi na kilio cha watanzania kimesikika na majibu yameanza kuonekana tunusubiri siku yenu kwa hamu pesa iliyoibwa haitapatikana yote kiasi itarudi na Mwenyezi Mungu atawafuta machozi kwa katibu mkuu hazina,waziri wa fedha na gavana huyu anayejua 'kutoa pesa tu'.

Watanzania tujiulize manunuzi ya ndege hayajaosheshwa kwene taarifa ya CAG kama hayajaonyeshwa ina ndege zimeingizwa kama pesa kuhamia za kuhamia makao makuu ambazo hata kiasi chake hakijulikani.

Tuwaombe wabunge watuonee huruma wananchi kwa kuokoa fedha ambazo wangelipwa kukaa Dodoma kujadili bajeti ambayo kimsingi haina maana kwa Serikali ya awamu ya tano hivyo ni bora tukaokoa hata hizo pesa za kulipana posho kuliko kupata hasara mara mbili.
Usiwaulize wao iulize serikali.
 
Sasa hivi tunajadili upotevu wa mabilioni ya shillingi ndani ya CHADEMA.

Mbowe njoo ujieleze
 
Sidhani kama utafika madibira aisee
wengine tumechanjiwa, kama wewe ni mtu usiyejulikana ukija kukesha mlangoni kwangu ili nijiteke basi ule muda nakuwa nimepumzika na mkeo nyumbani kwako wakati kunakaribia kupambazuka unarudi kwako nami narudi kwangu kuoga kisha naenda zangu Kibengu kupalizi viazi!
 
Unaweza ukamuheshimu mtu kwa maneno yake ila ukamdharau kwa matendo yake Huu ndio Wimbo wa Uzalendo tuliokuwa tuna ubiriwa
 
Msije kushangaa huko mbeleni kuwa awamu ya 5 ndio ikawa na ufisadi wa kupindukia. Muda ni mwalimu mzuri sana.
 
Back
Top Bottom