Waziri wa Fedha, Katibu Mkuu na Wakuu wa Idara na Vitengo waliohusika katika malipo wawajibike

Wilderness Voice

JF-Expert Member
May 19, 2016
921
1,637
Waziri Mkuu aliiibua matumizi mabaya ya fedha za Umma katika Wizara ya fedha. Kiasi cha shilingi Bilioni 2 na ushee, zililipwa ndani ya watumishi wa Wizara husika isivyo halali.

Waziri aliagiza Mkurungezi wa TAKUKURU kuchunguza, na aliwataja watumishi 9 kusimamishwa kazi wakisubiri uchunguzi wa Takukuru. Nimejiuliza sana taratibu za malipo ya kiserikali zinapofanyika, hasa katika Wizara kubwa kama hii ya fedha, je! Katibu Mkuu huwa hajui kilichofanyika? Je, Wakuu wa Vitengo na Idara husika malipo yanapoelekezwa, huwa hawajui juu ya malipo hayo?

Isitoshe Waziri akiwa ndiye msimamizi na kiongozi wa juu katika wizara, ambaye ana uwezo wa kuitisha Vote Book, na kupewa taarifa ya matumizi ya fedha katika wizara, je. Waziri husika haya malipo ya mabilioni hakuwa na taarifa nayo?

Kwanini Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watu 9 pekee, wakati Katibu Mkuu, ndiye mpitishaji wa mwisho kuruhusu fedha itoke au isitoke ameachwa?

Katibu Mkuu, kabla malipo hayajafanyika, lazima ajiridhishe kwa mujibu wa sheria kama malipo yamefuata taratibu au lah? Kwanini katibu Mkuu ameachwa?

Tupewe sababu kama watanzania ambao tunalipa kodi, Kwani fedha za watanzania zinachezewa. Kipi kinamfanya mlipaji Mkuu katika wizara asalimike katika hili?

Na Kipi kinamfanya Waziri wa Wizara ya Fedha, asiwajibike juu ya malipo haya ambayo wizara yake imefanya? Hivi waziri anateuliwa kuwa pambo tu katika wizara na si kusimamia wizara? Kashfa ya Richmond ilimfanya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzuru. Je Waziri wa fedha ni nani asiwajibike katika hili ambapo malipo yaliyofanyika si halali?

Kwa sababu zilizotolewa juu ya malipo ukitazama tu hata bila kuambiwa ni kinyume. Kwasababu kazi iliyotekelezwa ni ndani ya majukumu yaliyo katika utendaji wa wahusika. Hata kama shughuli hiyo ilifanyika nje ya Dodoma, je kulikuwa na haja gani kufanyika nje ya eneo la kazi au mkoa?

Huu ni wizi na ubadhilifu wa fedha ya serikali. Hivyo mtu anae shiriki katika wizi au kuwezesha, nae uhesabiwa ni mtuhumiwa na kushitakiwa. Nimuombe Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan, Kuchukua hatua zaidi kwani yeye ndo mwajiri Mkuu wa Serikali. Achukue hatua dhidi ya wafuatao wakati uchunguzi ukiendelea;

Kwanza ampumzishe Waziri wa fedha kupisha uchunguzi katika Wizara yake? Kama alivyosimamisha uongozi mzima wa soko la Kariakoo basi na hili la Wizara ya Fedha achukue hatua kali. Kama alivyosema hajafurahishwa na utendaji wa Uongozi wa soko basi naomba hata utendaji ndani ya wizara ya fedha usimfurahishe. Huu ni wizi Mkubwa.

Pili, amsimamishe Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, na wakuu wa Idara au Vitengo ambako fedha imelipwa. Pengine Waziri Mkuu hana uwezo kumsimamisha Katibu Mkuu na Waziri wa Fedha, hivyo Mhe. Rais husika katika hili.

Tatu, watumishi wote waliopokea fedha isivyo kihalali, wakati wakitambua kuwa malipo waliopewa si sitahili yao, nao wachukuliwe hatua za kinidhamu, ikiwemo onyo kali, na warejeshe hiyo fedha haraka.

Hii itasaidia kuheshimu matumizi halali ya fedha. Wizara ya Fedha imekuwa ikituhumiwa sana. Hata mweshimiwa Rais mama Samia, nakumbuka alitoa agizo kwa Mkaguzi mkuu wa Serikali kuchunguza matumizi ya fedha katika Wizara hii toka January hadi mwezi March. Tunaomba kuambiwa uchunguzi umefikia wapi? Mbona kimya? Kunanini kinafanya uchunguzi huo usiwekwe wazi? Mbona chunguzi nyingine uwekwa wazi?

Na Rais aliagiza lifanyike huku akionesha ukali kabisa!

Je, Mkaguzi na mthibiti Mkuu, Ofisi yake imedharau agizo la Rais? Pengine hii imeleteleza hata Wizara kujiona wako juu ya sheria na hivyo kuzidi kutafuna fedha ya serikali kwani hawawezi kuguswa.

Mhe. Rais huku kuleana na kulindana, hakutomaliza ubadhirifu wa mali ya umma. Watu huko mtaani wakiiba kuku wananyanyaswa vibaya na polisi. Wengine wanauwawa kisa kaiba simu. Hawa ni raia wa hali ya chini kabisa. Hawana ajira, wanaishi kwa kubahatisha, hawajui kesho yao. Hivyo ushawishika kufanya vitendo vya uvunjifu wa sheria hasa kuiba vitu vidogo. Na wakikamatwa uhadhibiwa vibaya hata kuzidi thamani ya kile walichoiba.

Siwatetei wezi wa mtaani la asha! Bali natoa mlinganyo wa uharifu. Kunaibua kuwepo uharifu matakatifu kwa watumishi wa umma na uharifu wa kishetani kwa uharifu wa mtaani. Sheria isibague!

Iweje serikali iwalee waliowabadhirifu wa mali ya umma? na wamefahamika wazi? Kwanini serikali inawalinda? Kwanini serikali inanyamazia haya yanayoendelea Wizara ya fedha? Kwanini serikali inataka walaghai wananchi wake? Sheria ipo wazi, ukiwezesha wizi au jambo baya kufanyika nawe utakamatwa ili kusaidia polisi na hata kushitakiwa.

Katibu mkuu kawezesha malipo kufanyika huku akijua si sahihi, na Waziri wa Fedha alikuwa na taarifa, na hakufanya lolote lile. hivyo alibariki malipo. Haiwezekani Waziri mkuu apate taarifa harafu Waziri wa fedha asijue kinachoendelea ktk wizara yake. kama hajui basi hawezi majukumu yake hivyo aondolewe kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Sina wivu na watumishi wa wizara ya fedha, Waziri au Katibu Mkuu bali ni kutaka kuwepo na uhajibikaji, ili kuondoa mazoea ya kufumbiana macho hasa linapokuja suala la ubadhirifu wa mali ya Umma. Mhe. Rais, uliongea kupambana na wezi na Majambazi.

Hadi ukabadili kamanda wa Mkoa wa Dar es Salaam, hii ilionesha kashindwa. Tunamajambazi wizara ya fedha, kama waziri kashindwa na Katibu Mkuu nao waondolewe. Kwanini tufanye kwa wengine na wengine wawe na kinga ambayo sheria haiwapi hiyo kinga?

Naomba kuwasilisha!! Tunaimani nawe Rais wetu! kazi inaendelea!
 
Sio kwa Tanzania nakuapia hakuna kati ya hao uliowataja Atawajibika Historia unamtaja Mzee MWINYI ndio SHUJAA alipowajibika Enzi za NYERERE Sasa Hivi Wakubwa Wanalindana.
 
Sio kwa Tanzania nakuapia hakuna kati ya hao uliowataja Atawajibika Historia unamtaja Mzee MWINYI ndio SHUJAA alipowajibika Enzi za NYERERE Sasa Hivi Wakubwa Wanalindana.
Ndo maana namwomba Rais wetu aingilie kati! Mwinyi alikuwa so special, haijapata tokea. Mwenyezi Mungu alimbariki kwa moyo wake mnyenyekevu aliouonesha japo hakuhusika, hatimaye akawa Rais wetu. Mwenyezi Mungu azidi mpa maisha marefu.
 
Back
Top Bottom