Waziri wa Fedha, Dr Mgimwa awasilisha Bajeti ya serikali 2013 - 2014

Kwa kweli nilikua napata kichefuchefu kwa makofi yanayopigwa pale bungeni mpaka nimeamua kuzima mchina wangu, shame on them, hivi ni nini kinachowapeleka pale? Kuna furaha gani mpaka ikawa wao ndo wanaweza kusapot vitu visivokua na msingi, iv mbona mabunge mengine hatusikii utumbo kama huu wa makofi yaliyokua hayana utaratibu. Mwisho hapa ndo nilijua bunge hili ni la aina yake na utalikuta Tz tu pale niliposikia watu wa bodaboda watakuwa hawakati leseni, ilikua ni makofi tuu, jamani pumbazo hili mnatufanya sote ni wapumbavu? Hebu wabunge wetu tuambieni kama nyie mukiwa munapiga makofi kama hivo sisi huku nje tufanyeje?

Mkuu we acha tu,hilo bunge hakuna tofauti na club ya mateja
 
Kwani ukisoma kwa kliingereza ndio kujua sana au ulimbukeni?

Huna akili, sio wote wanaojua kiswahili hapa Tanzania.... Kuna watu waliomba kupata copy ya kingereza. Hata bosi wangu litaka ya kingereza ili asome mwenyewe kwa sababu hajui kiswahili.
 
tanzania kuna vyanzo vingi vya mapato, madini, maliasili, utalii, inakuwaje pombe na vinywaji ndo viongoze nchi....this is bullshit..

hivyo vitu vinatozwa kodi na ndio vinavyoingiza kodi kubwa sema pombe na vinywaji vinakuwa maarufu kwa sababu vinatumiwa na wengi ie vinawagusa wengi na ni daily consuption
 
Jaribu kuweka siasa pembeni.
Kwa akili za kawaida tu, kuondoa kodi kwenye bodaboda inawasaidiwa vijana au mwenye bodaboda? Zunguka kwenye vijiwe vya bodaboda ujionee wamiliki wa hizo kitu. Nenda kawahoji waendesha Taxi na bodaboda/bajaji nani anapata income kubwa kuliko mwenziwe. Nenda MOI kaangalie majeruhi wa bodaboda kisha ungekuwa policy maker kama ungelihamasisha hizi kitu. Ni majanga; hii policy na mbaya haina wema kwa vijana hata kidogo tofauti na alivyoweka mbwembwe pale wakati akiwasilisha hii kitu.
 
Kwa akili za kawaida tu, kuondoa kodi kwenye bodaboda inawasaidiwa vijana au mwenye bodaboda? Zunguka kwenye vijiwe vya bodaboda ujionee wamiliki wa hizo kitu. Nenda kawahoji waendesha Taxi na bodaboda/bajaji nani anapata income kubwa kuliko mwenziwe. Nenda MOI kaangalie majeruhi wa bodaboda kisha ungekuwa policy maker kama ungelihamasisha hizi kitu. Ni majanga; hii policy na mbaya haina wema kwa vijana hata kidogo tofauti na alivyoweka mbwembwe pale wakati akiwasilisha hii kitu.

Kama ulikua unafuatilia bunge, nadhani unajua hili sakata lilipoanzia. Wawakilishi wa wananchi ndio waliolianzisha na siyo waziri wa fedha.
 
Mkuu, ile hotuba haina maana, kuna vyanzo kibao vya mapato sijui inakuaje...Kuna madini, utalii, gesi, simu, nk. Kukimbilia kupandisha petroli na dizeli, road licence, nk ni kutaka kutuangamiza watanzania wa kipato cha chini na kati. Hawa ni wahuaji, ningetamani kama tungekuwa na wanaharakati wenye akili kama wale wa Kenya tungeandamana mpaka malango ya Bunge kuonyesha kutufurahishwa kwetu na hii bajeti ya mauti.

Bahati mbaya vyanzo vyote hivyo vinamuelemea mtu yuleyule - wa kipato cha kati na chini; ambao kwa mfumo wetu ni wachache wanaolipa kodi.
 
Hii bajeti ni hatari sijaweza elewa kama ni kutaka kuua wananchi: mafuta juu, simu bei juu, road licence juu, road toll and fuel juu!! halafu mshahara sh.1500/= kwa mwezi!!
 
(i) Kuongeza kiwango cha Ushuru wa Bidhaa kwenye magari yasiyo ya uzalishaji (Non-Utility Motor Vehicles) ya umri wa zaidi ya miaka 10 kutoka asilimia 20 hadi asilimia 25. Hatua hii inalenga katika kupunguza uagizaji wa magari chakavu, kulinda mazingira na kupunguza ajali;

Kosa watawala wetu wanalofanya kwa makusudi ni kudhani kuwa always gari la miaka mingi ni chakavu! Wenzetu hasa Wajapan wanatunza magari yao mno na yanafanyia services za uhakika na kukaguliwa mara kwa mara hivo yanavouzwa kama used bado mapya! Mfano mzuri na halisi mimi nilinunua Toyota Noah ya mwaka 1999 ilikuwa imetembea kilometa 75,000 nimelipa kodi ya uchakavu sawa ila gari ni mpya haina dosari kabisa Rafiki yangu akanunua Toyota Noah ya mwaka 2004 ili kukwepa ushuru wa uchakavu ila gari yake imetembea kilometa 230,000 sasa inamsumbua na anafikiria kuiuza au kubadili injini! hivi kati ya magari haya mawili lipi chakavu??lipi linaweza kusababisha ajali na lipi linachafua mazingira? Kiuhalisia nani alitakiwa kulipa ushuru wa uchakavu??Wahusika na hususani wahandisi watafute njia nyingine ya ku evaluate uchakavu wa magari sio umri wa gari!!
 
Back
Top Bottom