Waziri wa Fedha, Dr Mgimwa awasilisha Bajeti ya serikali 2013 - 2014 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa Fedha, Dr Mgimwa awasilisha Bajeti ya serikali 2013 - 2014

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luiz David, Jun 13, 2013.

 1. Luiz David

  Luiz David Member

  #1
  Jun 13, 2013
  Joined: Jun 13, 2013
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana jamii, leo ndiyo siku ambayo hatma ya maisha ya mtanzania kiuchumi kwa mwaka wa fedha 2013/2014 inaenda kuainishwa na waziri wetu wa fedha dr W.Mgimwa pale atakapo wasilisha bajeti ya serikali.

  ===================

  Isome:

  Bajeti-2013/14 - Tanzania

  Kifupi:

  - Katika kipindi cha Julai hadi Aprili 2013, Serikali ilikopa shilingi bilioni 1,364.7 kutoka soko la ndani la mitaji kwa ajili ya kulipia dhamana za Serikali zilizoiva pamoja na shilingi bilioni 809.1 kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

  - Mwaka 2012/13 Serikali ilikadiria kupata mikopo yenye masharti ya kibiashara shilingi bilioni 1,254.1, sawa na Dola za Kimarekani milioni 800 kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika bajeti ya mwaka 2012/13 iliyopitishwa na Bunge lako tukufu. Hadi kufikia Mei 2013, Serikali ilipokea shilingi bilioni 947, sawa na dola milioni 600 kutoka benki ya Stanbic, na shilingi bilioni 59.2, sawa na dola milioni 37 kutoka benk ya Credit Suisse.

  - Serikali ilikadiria kutumia shilingi bilioni 15,191.9 katika mwaka 2012/13. Mgawanyo wa matumizi ya Serikali katika kipindi hiki ulikuwa kama ifuatavyo: shilingi bilioni 10,597.1 zilitengwa kwa matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 4,594.8 zilikadiriwa kutumika kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

  - Hadi kufikia Aprili 2013, matumizi ya kawaida bila kujumuisha malipo ya hatifungani zilizoiva (rollover) yalifikia shilingi bilioni 7,582.6, sawa na asilimia 82 ya makadirio ya mwaka. Kati ya kiasi hicho, malipo ya mishahara ya watumishi wa Serikali, katika wizara, Idara zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Taasisi za Umma yalikuwa shilingi bilioni 3,209.2 sawa na asilimia 85 ya makadirio ya mwaka ya shilingi bilioni 3,781.1.


  - Hadi mwishoni mwa Machi 2013, Deni la Taifa (likijumuisha deni la umma na sekta binafsi) lilikuwa shilingi bilioni 23,673.53 ikilinganishwa na deni la shilingi bilioni 20,276.6 Machi 2012 likiwa ni ongezeko la asilimia 17. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 18,282.02 ni deni la nje na shilingi bilioni 5,397.50 ni deni la ndani. Deni la nje, linajumuisha deni la umma la shilingi bilioni 15,203.34 na deni la sekta binafsi ni shilingi bilioni 3,078.69. Kiasi hicho cha deni la nje kinajumuisha deni halisi shilingi bilioni 16,087.43 na malimbikizo ya riba ya shilingi bilioni 2,194.59. Deni la ndani linajumuisha hati fungani za muda mrefu kiasi cha shilingi bilioni 4,261.03 na dhamana za Serikali za muda mfupi kiasi cha shilingi bilioni 1,136.48.

  Waziri anapendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332 kama ifuatavyo: -

  (i) Kupunguza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira kutoka asilimia 14 hadi asilimia 13. Hatua hii inalenga katika kutoa nafuu ya kodi kwa mfanyakazi;

  (ii) Kuanzisha kodi ya zuio ya asilimia 10 ya kamisheni (commission) ya usafirishaji wa fedha kwa njia ya simu za mkononi. Kodi hiyo itakusanywa na kampuni za simu kutoka kwa wakala wanaotoa huduma za kusafirisha fedha kupitia simu za mkononi;

  (iii) Kutoza kodi ya zuio kwa kiwango cha asilimia 5 kwenye malipo yatokanayo na huduma mbali mbali kama vile huduma za ushauri wa kitaalamu na nyinginezo (Consultancy services and other services). Kodi hii itatozwa bila kujali kama kuna Namba ya Utambulisho wa Mlipa kodi (TIN) au la. Lengo la hatua hii ni kudhibiti na kulinda mapato ya Serikali;

  (iv) Kutoza kodi ya zuio kwenye bidhaa zinazonunuliwa na Serikali na Taasisi zake kwa kiwango cha asilimia 2 bila kujali kama kuna Namba ya Utambulisho wa Mlipa kodi (TIN) au la. Lengo la hatua hii ni kudhibiti na kulinda mapato ya Serikali;

  (v) Kufuta msamaha wa kodi ya zuio kwenye ukodishaji wa ndege kwa walipa kodi wasio wakazi (non-resident). Hatua hii inalenga katika kupunguza misamaha ya kodi na kuhuisha mapato ya Serikali;

  Hatua hizi za Kodi ya Mapato kwa pamoja zitaongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 131,686.

  Waziri anapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 kama ifuatavyo:-

  (i) Kuongeza kiwango cha Ushuru wa Bidhaa kwenye magari yasiyo ya uzalishaji (Non-Utility Motor Vehicles) ya umri wa zaidi ya miaka 10 kutoka asilimia 20 hadi asilimia 25. Hatua hii inalenga katika kupunguza uagizaji wa magari chakavu, kulinda mazingira na kupunguza ajali;

  (ii) Kuanzisha kiwango kipya cha Ushuru wa Bidhaa cha asilimia 5 kwenye magari ya uzalishaji (Utility Motor Vehicles) yenye umri wa zaidi ya miaka 10 yanayotambuliwa katika HS Code 87.01, 87.02 na 87.04. Hatua hii haitahusisha magari chini ya HS Code 8701.10.00; na HS Code 8701.90.00 ambayo kimsingi ni matrekta yaliyounganishwa; na magari yasiyounganishwa chini ya HS Code 8702.10.11; 8702.10.21, 8702.10.91; 9702.90.11, 8702.90.21; 8702.90.91; HS Code 87.04; 8704.10.10; 8704.21.10; 8704.22.10; 8704.23.10; 8704.31.10, na 8704.32.10, 8704.90.10. Lengo la kuanzisha kiwango kipya cha ushuru ni kupunguza uagizaji wa magari chakavu, kulinda mazingira na kupunguza ajali. Aidha, matrekta na magari yasiyounganishwa hayatatozwa ushuru huu kwa nia ya kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta ya uunganishaji wa magari na hivyo kuongeza ajira na mapato ya serikali;

  (iii) Kurekebisha viwango vya Ushuru wa bidhaa kwenye mafuta ya Petroli kama ifuatavyo: -

  a] Mafuta ya Dizeli kutoka kiwango cha sasa cha shilingi 215 kwa lita hadi shilingi 217 kwa lita ikiwa ni ongezeko la shilingi 2 tu;
  b] mafuta ya Petroli kutoka kiwango cha sasa cha shilingi 339 kwa lita hadi shilingi 400 kwa lita; na,
  c] mafuta ya Taa kiwango hakitabadilika kwa kiwango cha sasa;
   

  Attached Files:

 2. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2013
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,978
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Vyanzo vya kodi vikiongezeka, ukusanyaji wa mapato,kupunguza misamaha ya kodi na wananchi kufanya kazi kwa bidii nadhani tutakuwa tumesonga mbele.
   
 3. G

  Getstart JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2013
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 5,271
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Mimi ninawashangaa mnpokuwa na mchecheto wa bajeti ambayo imekwishajadiiwa bungeni kuitia mawasilisho ya Wizara zote. Kipya ni kipi zaidi ya ongezeko la kodi
   
 4. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2013
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,713
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Wakati mwingine ubabe ni muhimu kutumika ili mambo yaende kunakotakiwa.
   
 5. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2013
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,217
  Likes Received: 3,484
  Trophy Points: 280
  Bajeti ya Tanzania ni the comedy!bajeti iliyopita haikutekelezwa hata kwa 60% maana kuna baadhi ya wizara zaidi ya 50% ya fedha za maendeleo hazijatolewa kwa bajeti iliyopita leo tunasoma nyingine?utasikia tuu manamba yanatajwa na mapesa kibao yanakuwa allocated kwa wizara ila pesa hazitolewi kutekeleza bajeti hiyo!!kwahiyo ni kama formality tu usitegemee kitu kipya cha ajabu sana sana bei za vitu kupanda ila hali ya maisha kuendelea kuwa ngumu! Bila kuwaondoa hawa watesi wetu kwa zaidi ya miaka 50 hatutapiga hatua yoyote!!
   
 6. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2013
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ngoja tusubiri,japo tunategemea ongezeko la kodi kwa bidhaa ile ile!
   
 7. M

  Mkolokotiatanas Member

  #7
  Jun 13, 2013
  Joined: Mar 2, 2013
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wadau wa jm mnaizungumziaje bajeti hiyo.
   
 8. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,571
  Likes Received: 13,318
  Trophy Points: 280
  Waziri wa fedha, w. mgimwa anaanza kwa kutoa shukrani kwa wote waliowezesha kufanikisha kwa bajeti hii
   
 9. nkyalomkonza

  nkyalomkonza JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2013
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 1,165
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Shukrani zimekuwa Too Much. Nimechoka kumsikiliza
   
 10. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,571
  Likes Received: 13,318
  Trophy Points: 280
  A
  nasema kuwa bajeti ya 2013/2014 ni ya tatu katika mpango wa taifa wa miaka 5 na imejikita katika maeneo 6
  maji
  nishati
  uchukuzi
  elimu
  kuongeza mapato
   
 11. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,571
  Likes Received: 13,318
  Trophy Points: 280
  Shukrani ni sifa ya kiungwana. So usiboreke sana
   
 12. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2013
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,489
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. m

  man lesha Member

  #13
  Jun 13, 2013
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Wazri wa fedha ndo anaanza kusoma bajet kuu ya serkali
   
 14. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2013
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kumbe uko LIVE! Ebu endelea kutujulisha zaidi.
   
 15. t

  thatha JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2013
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Anaendelea kuwasilisha anasema bajeti hii itatoa kipaumbele katika secta za elimu,maji nishati nk,huku ikilenga pia kupunguza misamaha ya kodi.
   
 16. ram

  ram JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2013
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 5,988
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Jamani wengine tuko kwa mkoloni huku, no tv na radio, tupeni updates za hiyo bajeti nadhani imeshaanza kusomwa
   
 17. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2013
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,217
  Likes Received: 3,484
  Trophy Points: 280
 18. KELVIN GASPER

  KELVIN GASPER JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2013
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 918
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  nawahi grocery nikanunue vinywaji (bia+viroba) vya kutosha. najua kesho wafanyabiashara hawana subira kesho sio mbali.
   
 19. M

  Mkolokotiatanas Member

  #19
  Jun 13, 2013
  Joined: Mar 2, 2013
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  2subiri saa 10 jioni,kivumbi cha kumdanganyia mtoto pipi kitaanza!
   
 20. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2013
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,978
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wavivu wote jipangeni ,
   
Loading...