Waziri wa Elimu simamia utawala katika vyuo. Wanafunzi wanaumizwa na elimu inaanguka!

VETA, NACTE na TCU ni vyombo ndani ya wizara hii. Kulikuwa na malalamiko na matukio ya wanafunzi kunyanyaswa kingono. UDOM na Uhasibu Arusha vimekuwa ni mfano wa wazi.

Hata hivyo hatujasikia Wizara ikisema lolote juu ya matukio kama hayo pamoja na jamii kuyasikia tena na tena!

Nimefanya mahojiano na baadhi ya wanafunzi na hata waliomaliza ktk vyuo vya: UDSM, SUA, St. Augustine-mwanza, CBE, IRDP na Uyole-Mbeya na Ukiriguru-Mwanza. Hali siyo nzuri kwa vyuo vya certificates na diplomas. Tishio kubwa ni marks za mitihani! Yaonekana marks ni za bandia kutegemea uhusiano wao na waalimu au uzem,be wa mwalimu.

Nimepata majibu mengi lakini klwa kila chuo kuna jibu lililotia fora.

UDSM: Wanafunzi wanadekeza mtindo huo nadhani kwa utu uzima wao wako kwenye umri wa mahusiano, lakini kuna kozi marks zinagawiwa tu!

SUA: Mahusiano yapo kwa baadhi ya waalimu lakini hata wanafunzi wanayatafuta nje ya chuo

St. Augustine-mwanza: Wanaogopa mambo ya nidhamu tu, lakini mitaani wanakutana sana!

CBE-Dodoma: Hakuna shule serious. Watu wanakuja kuchukuwa vyeti na waalimu wamefanya ni jambo la kawaida kabisa kutoa marks tu! Wanafunzi wanashindana kupata waalimu.

IRDP-Dodoma: Hakuna shule serious na kuna waalimu ambao mahusiano ni sehemu kubwa ya kazi yao kuliko hata kufundisha. Wanafunzi wanapangishiwa na walimu wao mitaani.

Tengeru-Arusha: Hali iko kawaida. Utawala unakomaa sana na matukio ya wanafunzi.

Ukiriguru-Mwanza: Hapo utawala haujali kabisa. Walimu wanajifanyia wanachotaka, ni masela tu. Marafiki wanapata marks nzuri.
Hapo ukiriguru -Mwanza siyo kweli jombaaa hakuna mwalimu kijana pale isipokuwa tu yule mkuryaa nae age imeenda
 
Nilipoona kichwa cha habari nilidhani unazungumzia taaluma inayotolewa labda haikidhi mahitaji ya soko la ajira!
Kumbe ni masuala ya upendeleo ktk utoaji wa alama, rushwa za ngono na mahusiano kati ya walimu na wanachuo.

Kusemaukweli binafsi huwa naamini kama mwanachuo anajiamini kwamba, anaweza kupata alama zinazotakiwa, basi hawezi kushawishika kutoa rushwa ya aina yoyote ile.
Tatizo kubwa la vyuo vya juu, ni kuruhusu masuala yote ya mtaala kuwa chini ya chuo husika.
Nadhani wizara ilitakiwa kuweka utaratibu wa kukagua kozi zinazotolewa na kila chuo, na pia kufuatilia uhalali wa ufaulu kwa vyuo husika.

Kuna vyuo wanasoma mambo mengi kwa muda mfupi mfano UDOM, na wakati vyuo vingine wana mada chache japo kozi zinafanana.
Upimaji nao pia huwa tofauti. Jambo linalosababisha elimu kuwa kama vita. Na matokeo yake ndio hayo kwa baadhi ya wanachuo kutafuta kamserereko, kwa kukubaliana na hayo yaliyosemwa kwenye andiko hili!
 
Mleta mada bila kuweka ushahidi wa tuhuma zako wazi. Binafsi ninakubakisha katika sehemu ya kundi lenye nia ovu ya ku katisha tamaa malekichara na matutorio, na mainstrakta ili wafanye kazi kwa uoga. Hata hivyo, ninavyowajua hao wafanyakazi wa vyuo wataendelea kusimamia weledi ili kuliokoa taifa.
 
Hakuna cha mtaala mmoja. Kila chuo kinatoa walimu wake kulingana na somo lililopo kwenda kuingia kwenye panel ya usahihishaiji.

Mambo ya sasa mwalimu anakwenda kujifungia chumbani kusahihisha karatasi Za mwanafunzi wa chuo kikuu zimepitwa na wakati bro.
Ni nchi gani wanasahihisha mitihani ya chuo Kikuu kwa utaratibu huo?
 
Nilipoona kichwa cha habari nilidhani unazungumzia taaluma inayotolewa labda haikidhi mahitaji ya soko la ajira!
Kumbe ni masuala ya upendeleo ktk utoaji wa alama, rushwa za ngono na mahusiano kati ya walimu na wanachuo.

Kusemaukweli binafsi huwa naamini kama mwanachuo anajiamini kwamba, anaweza kupata alama zinazotakiwa, basi hawezi kushawishika kutoa rushwa ya aina yoyote ile.
Tatizo kubwa la vyuo vya juu, ni kuruhusu masuala yote ya mtaala kuwa chini ya chuo husika.
Nadhani wizara ilitakiwa kuweka utaratibu wa kukagua kozi zinazotolewa na kila chuo, na pia kufuatilia uhalali wa ufaulu kwa vyuo husika.

Kuna vyuo wanasoma mambo mengi kwa muda mfupi mfano UDOM, na wakati vyuo vingine wana mada chache japo kozi zinafanana.
Upimaji nao pia huwa tofauti. Jambo linalosababisha elimu kuwa kama vita. Na matokeo yake ndio hayo kwa baadhi ya wanachuo kutafuta kamserereko, kwa kukubaliana na hayo yaliyosemwa kwenye andiko hili!
Kozi zote zinazofundishwa vyuo vijuu lazima zipitishwe TCU waziaprove. Na Kila baada ya miaka mitatu zinakuwa reviewed.
Halafu pia lazima external examiner apitie mitihani aone kama iko chini ya kiwango. Wizara si ya kulaumu imeweka mifumo mizuri labda kama ufanyaji kazi wa hiyo mifumo ndio tatizo.
 
Mleta mada bila kuweka ushahidi wa tuhuma zako wazi. Binafsi ninakubakisha katika sehemu ya kundi lenye nia ovu ya ku katisha tamaa malekichara na matutorio, na mainstrakta ili wafanye kazi kwa uoga. Hata hivyo, ninavyowajua hao wafanyakazi wa vyuo wataendelea kusimamia weledi ili kuliokoa taifa.
Hayo mambo ya kutaka ushahidi ndo yanasababisha mitaani tunawachoma moto vibaka. Tuko mitaani na wengine ni wazazi na wengine ni wahitimu au wanafunzi. Tukisema unasema lete ushahidi, wakati huo muhusika pia anajitahidi kuficha ushahidi. Sasa hivi hata viongozi wa dini wakituhumiwa wanadai ushahidi wakati wao wanafundisha yasiyo na ushahidi.
 
Kozi zote zinazofundishwa vyuo vijuu lazima zipitishwe TCU waziaprove. Na Kila baada ya miaka mitatu zinakuwa reviewed.
Halafu pia lazima external examiner apitie mitihani aone kama iko chini ya kiwango. Wizara si ya kulaumu imeweka mifumo mizuri labda kama ufanyaji kazi wa hiyo mifumo ndio tatizo.
Hao TCU waropokaji tu! Ni wale wale toka vyuoni, eti wakifika TCU wanakuwa wajuzi kuliko wengine. Kila siku wanakopi ya nchi zingine, bureeee!
 
Back
Top Bottom