Waziri wa Elimu Shukuru Kawamba unatia aibu

Mr.Busta

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
672
99
Asubuhi ya leo nilikuwa nasikiliza kipindi cha BBC NA radio one walikuwa wanazungumzia elimu nchini Tanzania kama inakidhi viwango.kwaujumla walijaribu kugusa karibu wadau muhimu wakiwemo walimu, wanafunzi,wachapishaji wa vitabu,maafisa elimu halmashauri,wazazi na shirika la uwezo linalofanya tafiti kuhusu elimu.kwa ujumla wameonyesha mapungufu.ilipofika zamu ya waziri wa elimu akasema hana muda wa kuzungumza,kwakweli iliniuma sana kwa aliharibu ladha nzima ya mada.pia najiuliza ni kweli hana muda wa kuzungumza?je anataka muda gani? Dr mzima kweli unakosa cha kuzungumza?
 
bora hakuzungumza, maana angeishia tu kusema, eee nanii, nanii, nanii....
 
Atazungumza nini wakati hajui chochote? maana yake hapo alitaka aseme leteni maswali tutawaletea majibu ili akaelezwe nini cha kusema. Halafu tunategemea na kuwasililiza watu kama hao katika kusadia maendeleo ya elimu Tanzania. Huyu jamaa yupo kwa kuwa tu mfumo una mlinda vinginevyo hafai kwa lolote zaidi ya familia yake.
 
Siku nyiiinga nilishamuona huyu jamaa kuwa hamna kitu!Hata U-DC,Hawezi!Nasikia anapewa hizo nafasi sababu kuna ukaribu namkuu wanchi!!
 
kuna mtu mmoja kama si humu jf alisema u-dkt wawe wanarenew maana watu kama hawa hatuna imani nao kabisa.
 
Nyie hamjui cku hizi hata doctorate watu wanaforge?huyu kilaza tu,kama ndugu yake jk.afu tangu liingie wizaran matatizo yanaongezeka tu!
 
Siku nyiiinga nilishamuona huyu jamaa kuwa hamna kitu!Hata U-DC,Hawezi!Nasikia anapewa hizo nafasi sababu kuna ukaribu namkuu wanchi!!

tulitazame hili kwenye katiba namna ya kupata mawaziri.maana uraisi unatumika vibaya awamu hii
 
Asubuhi ya leo nilikuwa nasikiliza kipindi cha BBC NA radio one walikuwa wanazungumzia elimu nchini Tanzania kama inakidhi viwango.kwaujumla walijaribu kugusa karibu wadau muhimu wakiwemo walimu, wanafunzi,wachapishaji wa vitabu,maafisa elimu halmashauri,wazazi na shirika la uwezo linalofanya tafiti kuhusu elimu.kwa ujumla wameonyesha mapungufu.ilipofika zamu ya waziri wa elimu akasema hana muda wa kuzungumza,kwakweli iliniuma sana kwa aliharibu ladha nzima ya mada.pia najiuliza ni kweli hana muda wa kuzungumza?je anataka muda gani? Dr mzima kweli unakosa cha kuzungumza?

Sasa kama hana muda ulitaka lazima aongee na BBC na Radio One?

Huo ni upunguani, unampangia wewe muda wa kazi zake? mnafikiria watu wote wako "idle" kupiga porojo time zote?
 
Ndugu yangu sikiliza: Masuala yaliyokuwa yanajadiliwa ni masuala muhimu yanayohusu elimu katika nchi na yeye ndiye waziri mwenye dhamana hivyo alipaswa kutoa ufafanuzi ili kuweka mambo sawa. Kujibu swali/maswali angetumia muda mfupi tu na akaeleweka.

Kwa waliobahatika kumsikiliza wakati wa mgomo wakati anahojiwa na radio moja hapa nchini watakubaliana nami kwamba alitia aibu. Pengine aliambiwa alivyojikanyaga hivyo amehofu kurudia makosa hayo kwenye chombo cha habari cha kimataifa.
 
hata mimi nimesikia...eti amekosa nafasi!!! Serikali dhaifu ina watendaji zaidi ya wadhaifu....
 
Sasa kama hana muda ulitaka lazima aongee na BBC na Radio One?

Huo ni upunguani, unampangia wewe muda wa kazi zake? mnafikiria watu wote wako "idle" kupiga porojo time zote?
We huelewi kitu jambo linalozungumziwa ni sensetive afu unaleta undugu hapa huna lolote nawe nilidhani una uelewa kumbe kiza
 
Huwa simkubali kabisaaaaaaaaaaaa huyu Bwana, Hana uwezo wa kuongoza, kichwa kizito kuelewa, akielewa hajui kujibu, Majibu yake siku zote sio ya uhakika. Nadhan undugu tu ndo uliompa nafas hiyo, lakin uwezo HANA.
Na akiendelea kuwepo wizaran mambo mengi yataendelea kuharibika, kazi kwako mzee wa magogoni...!
 
We huelewi kitu jambo linalozungumziwa ni sensetive afu unaleta undugu hapa huna lolote nawe nilidhani una uelewa kumbe kiza

Wewe unajuwa sensitivity? jambo sensitive linaongelewa BBC? usiwe punguani, funguka kidogo.
 
Sasa kama hana muda ulitaka lazima aongee na BBC na Radio One?

Huo ni upunguani, unampangia wewe muda wa kazi zake? mnafikiria watu wote wako "idle" kupiga porojo time zote?

sio kila mtu anafaa kuwa kiongozi wa uma. kuna wengine wanafaa kuongoza familia zao tu. kukubali kuwa huna uwezo na jukumu fulani ni sifa kuwa una uwezo wa kuelewa mambo.
 
Back
Top Bottom