Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba majibu yako

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
1. Kuna baadhi ya Shule za Sekondari, kunakuwa na mihimili miwili inayokaribia kulingana kwa utendaji kazi wake.

Katika shule hizo, kuna Walimu walioanzisha Hostel za kwao. Hao wanakuwa na wanafunzi wao ambao hufundishwa masomo ya ziada baada ya Ratiba ya shule kukamilika. Hayo wanafanya kwa makubaliano na Wazazi wa wanafunzi hao.

Wanafunzi hao husoma shuleni lakini hawalali kwenye Hostel za shule, bali hulala kwenye Hostel za hao Walimu kwa lengo la kusoma muda wa ziada jioni na alfajiri.

Mimi sina shida sana na utaratibu huo. Shida yangu ni pale tarehe za kufunga na kufungua shule zinapotofautiana kati ya Wanafunzi hao wa Hostel za Walimu na wale wa Hostel za Shule husika.

Lakini pia hofu yangu ni kwamba, Walimu hao wenye Hostel za kwao wanaweza wasifanye juhudi sana kuwafundisha Wanafunzi wote darasani na wakatumia juhudi hizo kuwafundisha zaidi wanafunzi wa Hostel zao na hivyo kuwafanya wanafunzi wa Hostel za Shule kuwa na ufaulu mdogo kuliko wale wa Hostel za Walimu ili kuwavutia Wazazi kuwaandikisha wanafunzi wao kwa Walimu hao wenye Hostel za kwao binafsi.

Ahsante, naomba maoni.
 
Back
Top Bottom