Waziri wa Elimu na TAMISEMI, ni sawa Wanafunzi Shule za Serikali kuambiwa waende na dissecting kit na vitabu vya tahasusi?

Hiyo shule inawapenda hao wanafunzi waliochaguliwa.Shule zingine wanatelekezwa bila hivyo vitu vyote vilivyotajwa wanasoma hadi anamaliza kichwani hana kitu.Elimu bure ni kivuli kinachowalevya wazazi wengi na kujiona kua hawastahili kuwajibika kwa watoto wao.Sikudanganyi elimu bure haiwezi kumtengeneza mwanao awe yule unayemtaka.Shuleni hakuna vifaa muhimu na hivyo vitabu havipo pesa ya kuendesha shule hazipo.Mzee somesha mwanao hali ni tete kwenye hizi shule mpya.
 
1. Mwanangu amechaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita (F. V & VI) mwaka huu 2021 Shule ya Sekondari Nyantakara katika tahususi (Combination) ya Chemistry, Biology & Geography (CBG) iliyoko wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera. Hii ni shule ya serikali ya Tanzania.

2. Licha ya orodha ya mahitaji mengi anayotakiwa aende nayo mfano; fagio wa kufagilia ndani, sabuni ya maji ya chooni, fagio wa kufagilia nje, ream ya kataratasi nk nk, lipo hili ambalo mimi limeniacha hoi hata kujiuliuza kulikoni hizi shule za serikali? Nimeambiwa nimnunulie mwanangu

[A.] Vitabu yote vya tahasusi (subject combinations) anayokwenda kusoma yaani CBG & Basic Applied Maths

[B.] Dissecting Kit ya somo la Bailojia

3. Nikajiuliza ina maana shule hii anayokwenda kusoma mwanangu haina vitabu? Imekuwaje inaanza kidato cha tano huku ikiwa haina vitabu? Kipi kilipaswa kuanza, majengo au vitabu na walimu kwanza? Hivi mzazi kama nanunua vitabu vyangu kwa ajili ya mwanangu, si bora asomee nyumbani sasa na siku ya mtihani aende kufanya tu?

4. Nimelileta humu tujadiliane ili tujue majigambo ya serikali kuwa imeboresha elimu Tanzania, yana maana gani kama hali iko hivi ktk shule zake?

4. Naambatanisha na Joining instructions ya shule kwa ajili ya ushahidi na reference zaidi kwa atakayetaka kuthibitisha maelezo yangu.

5. Honestly, baada ya kuipata hii fomu ya maelekezo, nimeanza kusaka fedha tu na kufikiri kumpeleka shule ya binafsi.
View attachment 1829765View attachment 1829766View attachment 1829769
Hiyo ndogo mkuu,kwingine unatakiwa dawati na meza!
 
Wewe nashindwa hata kukujibu kwa sababu ni wazi hujelewa mantiki ya andiko langu lote. Na hiki unachosema "Elimu ni gharama" na kuwa kama sitaki gharama, nijaribu UJINGA, it's completely irrelevant na mantiki ya hoja yangu...

Anyway, ngoja nikupe tip kidogo kufungua ufahamu wako...

Mada yangu kimantiki inahusu "SHULE ZA SERIKALI" na mapungufu yake...

Wewe umejibu kitu kilicho "out of context" na ni kana kwamba unahalalisha upungufu huu na kuona ni sawa tu...

For your information, mwenzio nimesoma shule bora sana zenye kila kitu na ni za serikali. Labda kwa kwa kuwa ni zile ilizorithi toka kwa wakoloni na zingine ilizotaifishwa toka mashirika ya kidini miaka ya 1970s...

Pia, watoto wangu wamesoma na bado wengine wanaendelea kusoma shule bora za mashirika ya dini zenye kila kitu...

Huo usemi wa "IF YOU THINK EDUCATION IS EXPENSIVE, THEN TRY IGNORANCE" naufahamu maana yake pengine kuliko wewe unavyoelewa. Na haunihusu mimi na wewe tu. Unamhusu kila mtu nchi hii yote na serikali kwa ujumla na maamuzi ktk mipango yake..

Seriously, ninaye mtoto mmoja. Amefaulu vizuri O'Level na kapata nafasi shule za serikali kidato cha 5&6....

Niliona nipunguze gharama kidogo asome shule hizi hizi za serikali...

Nilipotumiwa Joining Instructions, nilichokisoma kikanishangaza na nikaona napeleka mtoto Jehanamu tu. Hiki ndicho kilichonifanya nishee nanyi humu ili tujadili...

Sasa watu badala ya kujadili hoja, wengi ufahamu wao mdogo sana kumbe wa kuelewa mambo kwani badala tujadili hoja, wengi wanaleta mipasho na kujadili mtu....

Nakubali kuwa serikali haiwezi kukamilisha kila kitu kwenye shule zake Mara moja. Lakini mambo ya msingi kama vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa ajili ya ujifunzi wa watoto wetu mashuleni ni lazima iyape first priority....

Naomba tujadili hilo tukihusianisha na jukumu kuu la serikali ktk kutoa huduma kwa wananchi. Achana na hiki ulichokiandika hapa maana hakuna mwananchi ambaye halipi kodi ili kuboresha shule zetu...
We mwenyewe umekubali kuwa serikali Haina uwezo wa kukidhii mahitaji yote shuleni, so yanayibaki mzazi jitahidi uyatimize kama unahitaji mtoto. Wako afauulu
 
Ndo umemaliza kusema na kushauri tayari?

Umeelewa mantiki (logic) ya hoja yangu kweli wewe?

Wewe shule uliyosoma wakati ule uliagizwa uende na karibu pickup nzima ya vifaa mfano fagio, mundu, kwanja, sabuni ya maji lita 5 au 10, maboksi ya vitabu nk nk ?

Kwani kuna sababu na ugumu gani kwa serikali kusema moja kwa moja tu kwa wananchi kuwa ada ni 1,000,000 ili tujue kuwa tunagharamia wenyewe elimu kuliko kudanganya watu na sera za kijinga na kipumbavu kuwa Tanzania tuna sera ya "elimu bure/bila malipo" huku mambo yakiwa tofauti..?

Tuache kudanganyana. Serikali ikokotoe tu gharama ya kusomesha mtoto mmoja kwa mwaka, iweke wazi na kumtaka kila mwenye mtoto alipie hiyo ili wanaoweza wapeleke watoto shule na wanaoshindwa washindwe...!!
Teh tunapenda mambo ya bure mkubwa, ukisema ada wanaona ni mzigo, tunasahu bure ndio ghali
 
Back
Top Bottom