Ninahamu sana kutaka kujua matoke ya DRS la VII yamekaaje mwaka huu kulingana na mazingira ya mwaka huu wakati mitihani ilikuwa imetanguliwa na mambo kadhaa hasa kubwa ni lile la mgomo wa walimu kutokana na kulipwa maslahi DUNI hali iliyopelekea mgomo ambao ulitikisa na serikali kuupuuza hatimae walimu kurejea madarasani hiku wakiapa kutoka sare ya bila bila mwaka huu je wametekeleza au bado. Tulishuhudia sms zilizokuwa zikisambazwa kwa walimu kuwa Tangu sasa ni Kufundisha kadri unavyolipwa. Lipwa kidogo fundisha kidogo Je, wamefaulu au la!