Waziri wa elimu mbona hatangazi matokeo std vii ?

RUKAKA

Senior Member
Apr 17, 2011
100
11
Ninahamu sana kutaka kujua matoke ya DRS la VII yamekaaje mwaka huu kulingana na mazingira ya mwaka huu wakati mitihani ilikuwa imetanguliwa na mambo kadhaa hasa kubwa ni lile la mgomo wa walimu kutokana na kulipwa maslahi DUNI hali iliyopelekea mgomo ambao ulitikisa na serikali kuupuuza hatimae walimu kurejea madarasani hiku wakiapa kutoka sare ya bila bila mwaka huu je wametekeleza au bado. Tulishuhudia sms zilizokuwa zikisambazwa kwa walimu kuwa Tangu sasa ni Kufundisha kadri unavyolipwa. Lipwa kidogo fundisha kidogo Je, wamefaulu au la!
 
Kweli RUKAKA; hata nami natamani matokeo!

Last edited by a moderator:
Wakati wa Bunge nilisikia Waziri kivuli wa elimu akimfagilia Kamishna mpya wa Elimu kuwa ni mchapa kazi, wadau niambieni hivi mpaka sasa ameleta impact gani? Wizara ina matatizo lukuki, wasiojua kusoma na kuandika wanazidi kuongezeka na wengine wanafanikiwa kwenda sekondari. Matokeo ya Darasa la saba wameyakalia walisema yatatangazwa Jumatano imepita na wala hakuna kilichoelezwa mpaka sasa.

Wizara ya Elimu mnatupeleka wapi au ninui mlioko hapo wizarani elimu yenu ni feki?

Eeh Mungu inusuru nchi yetu na majanga ya kielimu
 
waziri wa elim muislam unategemea nini zaidi ya malalamishi ya mfumo kristo na kuonewa?
 
Wakati wa Bunge nilisikia Waziri kivuli wa elimu akimfagilia Kamishna mpya wa Elimu kuwa ni mchapa kazi, wadau niambieni hivi mpaka sasa ameleta impact gani? Wizara ina matatizo lukuki, wasiojua kusoma na kuandika wanazidi kuongezeka na wengine wanafanikiwa kwenda sekondari. Matokeo ya Darasa la saba wameyakalia walisema yatatangazwa Jumatano imepita na wala hakuna kilichoelezwa mpaka sasa.

Wizara ya Elimu mnatupeleka wapi au ninui mlioko hapo wizarani elimu yenu ni feki?

Eeh Mungu inusuru nchi yetu na majanga ya kielimu
Tumechoka Kususubiri matokeo
 
Tatizo hata Prof Bhalalusesa amepelekwa pale kuwa Kamishna lakini hamna kitu yule ni janga la taifa. Alikuwa Mkuu wa Shule ya Elimu pale mlimani amekaa miaka sita lakini hakuna cha maana alivhofanya zaidi ya ufisadi mtupu. Alikuwa anachukua hela za TP kwa siku zote ambazo wanafunzi wako field lakini haendi kukagua hata mwanafunzi mmoja. Ma Lecturer wanaokagua wanaambiwa hakuna hela wakati ndogo zilizotolewa na serikali Bhalalusesa anakunja zote. kuna siku walimu walikosa gari la kupeleka mitihani kwa external examiners kwa sababu magari mawili ya elimu yalikuwa yanafanya kazi zake binafsi. Kumbuka magari yaliyopo ni matatu tu.

Wizara ya Elimu oyeeeeeeeeee mmepata Kamishna
 
Hivi huyu Kawambwa anataka mpaka watu waingie barabarani ndiyo atangaze matokeo.
JK una kazi maana wateule wako hawakusaidii, hata kutangaza matokeo ni tatizo?????
 
Watoto wa wenyenazo washajua shule ya S.t naniliu ndo ataenda na maandalizi tayali. Tunao subiri matokeo ya S.t KAYUMBA msipate presha madarasa ni mengi hata kama yako kama mabanda ya kuku lakini yatawatosha. Hata mtoto akipata 30/150 ataenda sekondari. Tuendeleze kula bata wazazi wenzagu serikali inatujali sana, msiwe na viwanda uongo.
 
Ni kweli si vema kuhusisha udini na uzembe wa kuchelewesha matokeo. Hata kama Waziri ni muislamu lakini wasaidizi wake ni wakristo, kama vile Kamaishana wa Elimqu, Mkurugenzi wa sekondari n.k. Kwa hiyo suala la Wizara kukaa na matokeo ni uzembe tu na kashfa kwa watendaji wote wa wizara ambao hawajali kabisa watoto wa maskini kwani watoto wa wenye vipato wameshajua shule watakazoenda watoto wao na hata tarehe ya kufungua shule.

Wizara ya elimu inapaswa kufumuliwa na kusukwa upya kwa sababu imejaza wachumia tumboni tu wasijali maslahi ya taifa. Tuliambia mwaka huu watoto watasiliba ili usahihishaji uenda faster, sasa matokeo yake ni kuwa matokeo yamechelew zaidi kuliko hata mwaka jana. nasikitisha sana.
 
..vumilia huenda th 21 au kabla kidogo. lakini haipiti x-mas hawajatangaza. Watoto wamefeli sana hadi shule zingine zilikuwa zinapata wanafunzi tisa tu badala ya 100 wanaotakiwa/ Hivyo wameshusha pass mark ili kupata idadi inayotakiwa!!! WAHUSIKA WAMERUDISHWA TENA KAZINI NA WAMEPEWA SIO ZAIDI YA SIKU TATU KUKAMILISHA ZOEZI HILO....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom