Waziri wa Elimu: Elimu ya juu inaporomoka, viwango vya Uprofesa vimeshuka

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema elimu ya juu inaporomoka huku akishangaa kushuka kwa viwango vya kupata uprofesa.

Hali hiyo imemfanya ayatake Mabaraza ya Vyuo Vikuu Tanzania kuwepo na ubora kwa kutoshusha vigezo ili kupata watu wengi.

Alitoa kauli hiyo jana Aprili 11, 2022 alipokuwa akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo Dodoma.

Alisema viwango vya kutoa Uprofesa lazima vipandishwe badala ya kuwa na kila mtu profesa. "Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kina University Standards (vigezo vya chuo), lakini wanashangaa mbona wengine wanapata Uprofesa kwa viwango tofauti na mishahara tofauti na ni serikall ileile,” alisema.

Pia, alisema kuna baadhi ya vyuo shahada za Walimu wake zinatia shaka na kusisitizalazima elimu ya vyuo vikuu iangaliwe.

"Tunataka akiwa profesa wa uhandisi awe ni profesa kwelikweli, tuone anazalisha watu kwa ajili ya SGR (reli ya kisasa) wanatusaidia kurekebisha ndege tunazonunua, akini siyo kujaribu kujenga mazingira ya kila mtu apate,” alisema.

Alipendekeza elimu ya juu iwe na viwango na kuwa na uhitaji wa vyuo vingi zaidi bila kushusha viwango.

"Nasema hili ingawa wengine watakasirika elimu ya juu inaporomoka, yaani walimu walewale, mitaala ileile, jina tu, kutoka chuo sijui cha nini kuwa chuo kikuu.

“Mwanzoni tulikuwa na tabia kama chuo kinataka kuwa Chuo Kikuu kishikizwe na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa kuwa hata chenyewe kilipoanza kilishikizwa na Chuo Kikuu cha London kusimamia ubora…

"Sokoine iliangaliwa na Chuo Kikuu Dar es Salaam sasa hivi mtu anataka atoboe hapohapo aende, hataki kuatamiwa kwa sababu kuna baadhi ya vyuo hata digrii za walimu zina mashaka, kuna chuo kilikuwa kinaongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo ambapo shahada yake inatokana na NGOS yaani zile digrii ambazo unalipa kiasi fulani unapata, lakini ukiajiriwa tutakuuliza digrii yako ni ipi? Ukiajiriwa na Serikali tunataka kujua PhD yako ulipata wapi,” alisema.

Kadhalika alisema kama watashindwa kusimamia viwango vya elimu ya juu mageuzi yatazungumzwa hadi mwisho wa dunia.

Alihimiza kuongeza ubora wa elimu ili Vijana wanaohitimu waajirike na kuajiri.

“Katibu Mkuu wetu hapa alipoingia wizarani alisema utengenezaji wa magari ya Wizara ufanywe na VETA kwa kuwa wanafundisha utengenezaji magari, wakasema aah! Tunaomba ukaombe kibali TEMESA, yaani unapewa kazi unakataa, tunachukua vijana tunasema tunawafundisha ufundi magari hivi kweli tunawafundisha ufundi magari au tunadanganya wazazi, alihoji.

Prof. Mkenda alisema atafanya uamuzi wa kuimarisha ubora wa elimu na sio kubembelezana na kwamba elimu inayotakiwa kutolewa ni ya kumuwezesha kijana kujiajiri na kuajiriwa.

Hata hivyo, alisema elimu ni uwekezaji wa vizazi na vizazi na kwamba uwekezaji ukifanywa vizuri itakuwa ni kuwekeza katika maendeleo ya nchi.

Akizungumzia kuhusu sera, Prof.Mkenda alisema sera ya elimu ya mwaka 2014 inataka mtoto asome kwa miaka 10 elimu ya lazima suala hilo halijafutwa na kwamba sera hiyo ipitiwe na wakubaliane au wabadilishe sera.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Eliamani Sedoyeka alisema baraza hilo linajukumu la kuishauri wizara na kuhakikisha utekelezaji wa majukumu yanafanyika kwa weledi.


Chanzo: Nipashe
 
Anarifaa riport ya kinyesi cha mto Mara nini?

Manyele jitathmini upropesa wako.


Viva Mkenda
 
Kwa kweli tunapoangalia ubora wa elimu yetu upo chini sana kwa ngazi zote. Yaan unakuta mtu amesoma na mavyeti chungu mzima lakini hana maarifa yoyote. Leo hii watu wanafikia ngazi ya digrii wakiwa wengi sana kama waliohamishwa kutoka shule ya msingi kwenda sekondari ya kata bila kujali vigezo stahiki vya ufaulu. Elimu imekuwa ni kama fasheni za mavazi tu ndio maana ubora wake umeshuka sana. Hongera waziri kuliona hilo lakini ukweli ukitaka kutibu tatizo hilo rudi kuanzia ngazi ya chini kabisa shule za msingi.

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 
Waziri badala ya kujikita kuweka mitaala ambayo inalenga kuwapa vijana uwezo na ufanisi wa kukabiliana na changamoto za sasa, anaenda kupambana na kuwananga wenye PhD na maprofessa ambao wanazalishwa na mfumo anaousimamia yeye mwenyewe.........
 
Waziri badala ya kujikita kuweka mitaala ambayo inalenga kuwapa vijana uwezo na ufanisi wa kukabiliana na changamoto za sasa, anaenda kupambana na kuwananga wenye PhD na maprofessa ambao wanazalishwa na mfumo anaousimamia yeye mwenyewe.........
ah ahhhhhhhha ahhhhhhhhhhh
 
Back
Top Bottom