Waziri wa Elimu anasimamia asichokiamini? Mwanae anasoma English Medium

Mwl Nyerere watoto wake walisoma Tabora,Bunge,Tambaza. Waziri wake wa Elimu aliyajua matatizo yote ya elimu kwakuwa hata watoto wao walisoma shule hizo hizo.Watoto wake walikwenda JKT,walipigana vita vya Uganda hapakuwepo ubaguzi wa aina yoyote kama tunavyoona leo.
Waliopo hawana tofauti na wezi, majambazi, majangili
 
Sasa njoo na utar

Nasema tena, usiturudishe ujimani ebo!! Mpuuzi kweli wewe, eti kwa kuwa ni waziri wa elimu basi apeleke watoto wake shule za kata? What a hopeless thinking?
Ndio maana mbunge msukuma anawatukanaga tu.

Pumbavuuuuuuuu.
 
Heshima sana wanajamvi,

Tanzania pengine ni nchi pekee duniani yenye maajabu yasiyoweza kulinganisha au kufananishwa na nchi nyingine.

Ni jambo la ajabu waziri wa elimu msimamizi wa elimu yenu na mustakabali wetu wa siku zijazo.Waziri wetu huyu watoto wake hawasomi katika shule za umma,wapo katika zile shule zetu "english medium" binafsi. Ikiwa Waziri hana imani na shule zetu za Kata au ukipenda St Kayumba na wakati huo huo yeye ni msimamizi na mwangalizi au ukipenda mlezi mkuu hapeleki watoto wake huko maana yake nini ?.

Mwl Nyerere watoto wake walisoma Tabora,Bunge,Tambaza. Waziri wake wa Elimu aliyajua matatizo yote ya elimu kwakuwa hata watoto wao walisoma shule hizo hizo.Watoto wake walikwenda JKT,walipigana vita vya Uganda hapakuwepo ubaguzi wa aina yoyote kama tunavyoona leo.

Ifike mahali uzalendo usisitizwe katika nyanja kama hizi,ukibahatika kupata nafasi ya kuongoza wizara ya Viwanda basi wewe kama Waziri lazima uonyeshe mfano wa kununua bidhaa za Tanzania mfano thamani za maofisini,nguo. Ukibahatika kuongoza Wizara ya Elimu lazima watoto wako wasome shule za kata wakutane na changamoto za ukosefu wa waalimu,vitabu madarasa,matundu ya choo na nk.Hii itasaidia Wizara kupanga mipango ambayo italenga kuondoa kero zote zinazozikumba shule za umma.

Ni aibu kwa jamii iliyostaharabika kuhubiri jambo ambalo kwa hakika wewe mwenyewe huliamini unalitilia shaka,unalionea aibu,hulipendi hauko tayari jamii yako ya karibu kwa maana ya watoto wako wasilishiriki.

Mama Ndalichako, Ummy ikiwa watoto wenu hawasomi shule za serekali wakati nyinyi ni wasimamizi wakuu wa elimu Tanzania basi hakuna nafasi nyingine zaidi ya kujiuzulu.
Uzi wako ungekuwa na maana sana endapo ungewataja haonwatoto wa Waziri ni akina nani hasa na wanasoma Shule gani? Maana naona kama umepiga porojo tupu au dhahania. Weka wazi, watoto wake wanasoma English Medium ipi na wakina nani hao? Inaonekana unawajua.
 
Jitu kama wewe ndio mnarudisha maendeleo ya taifa nyuma. Potelea mbali na mawazo yako ya kijima. Tulishatoka huko. Eti waziri asomeshe mtoto wake shule ya kata ndio ulizike? Thinking ya kijinga kabisa. Naona unachuki na waziri na si vinginevyo.
Hujakosea mke wangu mtamu.
 
Magufuli angekuwepo tungemshauri aweke kigezo viongozi wote waoneshe mfano watoto wao wasome shule za umma. Kama hataki aachie uongozi. Hili wazo jiwe asingelikataa. Ungekuwa ndiyo mwanzo wa kuboresha shule za umma.
 
Magufuli angekuwepo tungemshauri aweke kigezo viongozi wote waoneshe mfano watoto wao wasome shule za umma. Kama hataki aachie uongozi. Hili wazo jiwe asingelikataa. Ungekuwa ndiyo mwanzo wa kuboresha shule za umma.
Unajua watoto wa Magufuli husoma FEZA Schools?
 
Back
Top Bottom