Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,093
- 5,567
Waziri wa Viwanda na Biashara, Selemani Jafo, ameunda kamati ya watu 15 inayoongozwa na Edda Tandi Lwoga wa Chuo cha Elimu ya Biashara-CBE ili kuchunguza biashara za rejareja zinazofanywa na wageni kinyume cha sheria, hasa katika soko la Kariakoo. Kamati hiyo itafanya kazi kwa siku 30 ili kubaini uhalali wa vibali vya biashara za wageni na athari zake kwa wafanyabiashara wazawa.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na uongozi wa wafanyabiashara wa Kariakoo, Februari 2, 2025 Jijini Dar es Salaam Dkt. Jafo amesema kamati hiyo itachunguza sekta zilizoathirika, mfumo wa utoaji vibali kwa wageni, na mbinu zinazotumiwa kufanya biashara kinyume cha sheria na kupendekeza hatua za kudhibiti hali hiyo na kusaidia wafanyabiashara wa Kitanzania kushindana kibiashara.
Soma Pia: Rais Samia aagiza Waziri wa Biashara kudhibiti Wageni kufanya biashara za Machinga, ahoji vijana wetu watafanya kazi gani?
Dkt.Jafo ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikia malalamiko ya wafanyabiashara wa Kariakoo kuhusu wageni wanaofanya biashara za rejareja badala ya kuwekeza ambapo hali hiyo inaathiri uchumi wa Watanzania hususan vijana.
Dkt.Jafo pia amesema tatizo hili pia lipo kwenye sekta nyingine kama madini, hivyo ripoti ya kamati hiyo itapendekeza suluhisho la kudumu.