Waziri wa Biashara na Viwanda, Godfey Mwambe apiga marufuku taasisi zilizo chini ya Wizara yake kufunga biashara za watu kwa kisingizio chochote

Huyo waziri anajua kua kuna mtu anaitwa TRA??
hashikiki huyo mtu hata waseme vipi
 
Wawafungulie Biashara zao majadiliano yaendelee .Deni huwa halifungi mtu ni kesi tu ya madai .Hivi unafunga duka la mtu kisa kodi nk si mjadiliane tu ama ipunguzwe au alipe kidogodogo kwa installments Kufunga biashara that is too...
Kuna dhana moja imesaidia sana Haya kutokea. Kwamba kila tajiri au mwenye kiwanda ni mwizi... na umasikini ndo uzalendo....
KINGINE WANAWEKEANA MONTHLY TARGETS AMBAZO ILI UZIFIKIE LAZIMA UWE MKATILI KWENYE UKUSANYAJI
 
Ni wakati muafaka sheria zitungwe ili haya matamko yawe na nguvu ama sivyo...!
 
[/QUOTE]
Wanakera, mfanyabiashara kapanga wanakuja na rangi kuchafua ukuta.maandishi makubwaaa
Kichekesho unakuta ameandika huna leseni funga !!!! si waonane na mhusika tu waongee kuwa baada ya miezi miwili tutapita tena uwe umeshatafuta leseni wanampa na tarehe ya kuja na kumtia moyo kuwa hatutapita kukuliza tena hata ukiona tunakuja usifunge usidhani tunakuja kwako.Tunakupa miezi miwili utaratibu wa keseni ni huu hata ikibidi watembee na fomu kabisa wampe wamwelekeze kujaza na viambatanishi vinavyotakiwa .Kama anavyo vyote ajaze hapo hapo wampe na control number alipe hapo hapo kama anazo kwa mobile money au akaunti kama akimaliza vyote kujaza waondoke na fomu zake wamwambie tutakuletea leseni hapahapa dukani endelea na biashara yako Hiyo ndio friendly approach inatakiwa

Lakini jitu linakwambia funga huna leseni hata ukiliambia nipe fomu basi ya kuomba leseni nijaze sasa hivi halina hata fomu limekaa kigaidi gaidi tu na mirangi ya kuandika funga na mikufuli!!! huna TIN ohh huna kibali ohhh hujalipa kodi ohhh leseni huna nk funga!!!!

Mtu leseni hana advice him or her give him or her time without asking him or her to close business
 
Tatizo nadhani wasomi wetu wengi hawaelewi somo la business administration hili somo kazi yake si tu kusimamia biashara zako unakofanya kazi lakini pia ni kwa Afisa wa serikali au taasisi ya serikali kusimamia business zilizoko private sector kuwa zinakuwa encouraged zinafanya vizuri na haifungwi ovyo ili ziendelee kutoa gawio yaani kodi kwa serikali.kodi ni dividend inayotolewa na private sector kwa serikali sasa wakifa hovyo hovyo dividend utatoa wapi? TRA,watoa leseni ,vibali nk wajione kama business adminstrator wa private sector na sio tu watoza kodi nk.Business adminstrator yeyote interest yake ya kwanza kubwa business i perform vizuri ili itoe dividend nzuri

TRA nk nadhani hili somo.hawalijui japo wako wamejaza midgrii kibao yenye hilo somo ndani

Funga funga za biashara na viwanda ni uthibitisho
Mwambe is the best business administrator
 
Wakifunga wanasifiwa wakifungulia wanasifiwa... we are like Bendera fuata upepo... tupo kama kwenye Majaribu ya Chanjo katika kuongoza Nchi
 
To me Mwambe is the best Macro and Micro business Adminisrator
 
Kwenye taarifa ya habari ITV leo ya saa mbili nimemsikia Waziri wa Biashara na Viwanda, Godfey Mwambe amepiga marufuku taasisi zilizo chini ya wizara yake kufunga biashara za watu kwa kisingizio chochote ahimiza majadiliano badala ya funga funga. Amesema asisikie. Huo ni uhujumu uchumi

TRA na Taasisi zingine za umma mnaotembea na Makufuli na wino wa kuandika maduka na viwanda vya funga funga na mi X kibao mumesikia alichosema Mwambe?

Au huko kwenu kazi yenu kufunga biashara za watu?
Amesema ukweli, suluhisho sio kufunga biashara za watu, mazungumzo ndio suluhisho kwani mara nyingi hayo makosa yanatokea bila kukusudia, na ukifunga hizo Biashara unaikosesha Serikali mapato, Ni sawa Waziri akisema Mtumishi atakayefunga Biashara ni mhujumu uchumi, na isiishie hapo tu, Mtumishi wa Serikali atakayefunga Biashara ashitakiwe mahakamani kwa uhujumu uchumi, na Serikali ifanye kila kitu digital, ili kuondoa rushwa.
 
Naomba serikali ianze kurudisha majeshi mazee nyuma .Waanze kuweka post kubwa za juu taasisi za serikali waliozaliwa Miaka ya 80 kwenda mbele wengi era before 80s vichwa vyao vimefikia upeo kwenye maeneo mengi .Wengi hawashauriki utasikia miaka yote sisi tumekuwa tukifanya hivi!!! hawako tayari kuruhusu new knowledge kuingia na ku think outside the box nk hao wa before 80s wapewe tu vyeo vya advisors wakisubiri kustaafu wapishe new blood hasa taasisi za serikali na mashirika ya umma hao vijana waanze ku practice what they have learned currently and know currently!!!
 
Amesema ukweli, suluhisho sio kufunga biashara za watu, mazungumzo ndio suluhisho kwani mara nyingi hayo makosa yanatokea bila kukusudia,
Uko sahihi nilikuwa na rafiki yangu siku moja kuna rafiki yangu alikuwa akitengeneza komeo hizi za milango ya kiswahili ya kufunga na kufuli nyumbani kwake kisha anajaza kwenye viroba anazunguka madukani kuuza ya vifaa vya ujenzi kuuza .Siku hiyo wakaja wakamkuta kilichomkuta alikoma sema alihonga lakini ikabidi kiwanda afunge na alikuwa kaajiri watu 20 wenye familia zao .Wote wakaachishwa kazi na yeye hakukaa sana akafa Wakamwambia sijui anavunja sheria sijui za leseni za viwanda sijui nini na yeye hakuwa akijua chochote hizo sijui leseni sijui nini unaanzia wapi na unaishia wapi siji kusahau It is one if the bitter experience that I will never forget in my life
 
  • Thanks
Reactions: Lob
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom