Waziri wa biashara amefuta leseni za wafanyabishara sita kwa kuuza sukari kwa bei ya juu na kutoa onyo kwa wengine

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,845
141,767
Waziri wa biashara wa Zanzibar amewaonya wafanyabiashara wanaopandisha bei za bidhaa kiholela na amewanyang'anya Leseni wafanyabiashara sita wa sukari kisiwani Pemba.

Waziri amesema bei ya sukari isizidi tsh 2000/= kwa kilo, Mchele tsh 1600/= kwa kilo na Unga wa ngano tsh 1600 kwa kilo.

Source: ITV habari
===
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe Omar Said Shaban amefuta leseni za wafanyabishara sita kwa kuuza sukari kwa bei ya juu na kutoa onyo kwa wengine.
 
Wahenga walisema maeno matupu hayavunji mfupa, mbona hajalikabili lile jitu la kutisha matozo, makodi &_allies
 
Nasubiri Waziri Kitila naye amuige waziri wa nchi jirani tuliyoungana nayo katika kuingilia kati upandaji holela wa bidhaa hasa mafuta ya kula
Ngoja tuone.

Kesho ana kongamano.

Ila Waziri wa biashara Zanzibar anatokea ACT wazalendo!
 
Nilijua bara Kama Zanzibar sahihi tena wangeuza hata chini ya hapo sukari 1600.Kama isingekuwa Ni koloni la bara
 
Waziri wa biashara wa Zanzibar amewaonya wafanyabiashara wanaopandisha bei za bidhaa kiholela na amewanyang'anya Leseni wafanyabiashara sita wa sukari kisiwani Pemba...
Nilidhani ni hawa majambazi wa Ccm bara. Serikali imekaa kimya kama hamna kitu kina tokea huku bara. Nadhani Mama Samia arudi tuu kwao Makunduchi. Bara imemshinda
 
Hizi bei elekezi ndo huzidi kuharibu mambo, cha msingi ni kuacha bidhaa ziwe nyingi kweye mzunguko bei zitashuka automatic.

"The higher the supply, the lower the price".
Nakumbuka enzi zetu Wahenga katika nchi hii tulikuwa na hiyo bei elekezi ambayo tuliielewa kama "controlled price". Kwa bahati mbaya kabisa bei hii ikatokea kuleta matatizo ya vitu kupotea madukani. Tunakumbuka hata wenzetu walitushangaa na kusema huko Tanzania " the controlled price is a price at which the commodity is not available". Je, historia yataka kujirudia tena?
 
Nasubiri Waziri Kitila naye amuige waziri wa nchi jirani tuliyoungana nayo katika kuingilia kati upandaji holela wa bidhaa hasa mafuta ya kula

Kule ni rahisi maana una control mkoa kama pwani au dar es salaam huku bara ngoma ngumu sabay na doria zake ila sukari iliiuzwa bei
 
Waziri wa biashara wa Zanzibar amewaonya wafanyabiashara wanaopandisha bei za bidhaa kiholela na amewanyang'anya Leseni wafanyabiashara sita wa sukari kisiwani Pemba.

Waziri amesema bei ya sukari isizidi tsh 2000/= kwa kilo, Mchele tsh 1600/= kwa kilo na Unga wa ngano tsh 1600 kwa kilo.

Source: ITV habari
Washushe na bei ya mbolea na pembejeo nyingine basi wasilete janja janja
 
Back
Top Bottom