mwembemdogo
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 2,282
- 1,252
Nadhani wakati umefika kwa Waziri wa Ardhi kukemea na kuchukua hatua kwa wananchi wenye kuvamia mashamba/viwanja vinavyomilikiwa kisheria.
Viongozi wengi wamekuwa wakilitatua suala hili kisiasa badala yake linakuwa sugu.Tumejionea aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh.Makonda badala ya kuwatoa wavamizi aliagiza wahakikiwe ili watambuliwe.Hivi unapomhakiki mvamizi na hukumchukulia hatua naamini hata kesho atavamia eneo lingine na lingine.
Wakati umefika wa kuwakomesha wavamizi kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafunga ili kumaliza migogoro ya Ardhi.Tunakuomba Mh.Lukuvi hebu weka sheria hadharani ili atakaye ivunja asimlaumu mtu.