Waziri wa Ardhi na Makazi, suala la Anwani za Makazi ni Itifaki ya Rais. Kuwa makini wasikuharibie

Master Legendary

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
543
736
Wanajamvi kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia zoezi hili naona kinachotokea ni Mkanganyiko Mkubwa na Vurugu tupu kuanzia kwenye ajira za hawa vijana, mafunzo hadi utendaji kazi. Nimeshindwa kuelewa hili zoezi kweli lina Msimamizi au linajiendea lenyewe bora liende.

Nikiangalia Dhamira ya Rais na namna alivyolipa uzito na kinachoendelea huku Mtaani ni vitu viwili tofauti sijui kama wenzangu mnaelewa kitu.

Kwa bahati nzuri niliwahi kushiriki zoezi la Mwanzo la Majaribio ambalo lilinipa ufahamu kidogo wa hili zoezi.
Kwa wasiofahamu lengo la hili zoezi ni zuri sana likifanyika kwa umakini unaweza kufika popote na kufikiwa popote kwa maana hiyo kiuchumi,kibiashara,kiusalama,kijamii na hata kisiasa ni zoezi zuri sana na muhimu.

Ila nashangaa juzi nilikutana na kijana mmoja anayefanya hili zoezi analalamika wanafanya kazi karibu wiki sasa hawajalipwa hawana nauli mara malipo yao hayajulikani ni kiasi gani hadi sasa,mafunzo yao yalijaa mizengwe wanaofundisha huku chini hawajaelewa vizuri sasa wanawaelimishaje wenzao.

Jana nimepita maeneo ya Ilala kule ni Fedheha tupu sijui kinachofanyika ni nini nimechukua jina la Barabara na namba moja nimemtumia Afisa mmoja wa Wizara nimemwambia ajaribu kama ataweza kufika,huko Mbezi Msakuzi Kusini kinachofanyika ni aibu Barabara ziko vizuri kabisa wananchi wamezitoa ila namba zilivyotolewa huwezi kufika popote wala kupeleka mzigo kokote, hakuna flow ya Namba katika Barabara za Mitaa zinazoeleweka na maeneo mengi hawataki kutoa majina kwenye Barabara ndogo ambazo zingeweza kupewa majina zikasaidia ila wanavuta nyumba zote kwenye Barabara kubwa,matokeo yake eneo lina Barabara nzuri ya kupewa jina ila ukisoma namba za nyumba zote ni Witiri hakuna Shufwa na hazieleweki kabisa wanaojua haya mazoezi wananielewa.

Kwa hali ilipofikia ni vyema Waziri aingilie kati mapema asisahau hili zoezi limesukumwa na Mama halitahitaji Kamati teule za Bunge.
Mnaomsaidia Waziri wa Ardhi mfikishieni.
 
Kwenye matangazo ya hizi ajira dar walitaja malipo wazi wazi.

Anataka nauli ya nini wakati ni mkaz wa hapo hapo anapofanyia kazi/mtaa

hili zoezi linasimamiwa na ile wizara ya nape ,,ardhi sio sana
 
Ni issue ya dunia hii wala siyo ya rais although yeye amehamua kuisimamia kama watoa shekeli wanavyotaka kulingana na wanaoyotoa.
 
Sisi bongo kitu peke ambacho tupo nacho siriaz ni umbea na upuuzi mwingine ila mambo ya umuhimu hayapewi uzito unaostahiki.

Tukija kwenye elimu mtu unasoma features of wave erosion mara Chimurenga war ambavyo havina umuhimu wowote.
 
Majina ya mitaa kwanza ni aibu tupu. Waliotoa majina hawana vigezo vinavyoeleweka . Mfano Sinza C wana majina kama shehe Bofu, vikindu watu hawana sababu yoyote na sinza. Wapo wazee maarufu kama ni majina wanataka. Bora majina ya wanyama, ndege, nk kulio mara afweli, shehe bofu, nk.

Pia anwani za mijini wanaandika tu jina la nyumba badala ya namba kamili inayojumuisha mkoa, wilaya, kata ndio nyumba au kiwanja. Watu watashindwa kujaza fomu ipasavyo.

Upande wa vijijini ndio uangalifu unahitajika maana utakuta mji wa mzee say Mrisho utakuta watoto wamejenga hapo, wajukuu hapo nk. Ingekuwa ni vyema anwani zitoke kwa majina ya waanzilishi na sio wakazi wa sasa maana orodha itakuwa ndefu mnooo bila maana.


Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app
 
Zoezi liliharibika tangia mwanzo halmashauri nyingi kwa sasa ukiritimba na kujuana kumerudi kama zamani ajira zimetolewa kimjuano vijana hawajui wajibu wao huenda ht training haikuwa vzr
 
Ila nashangaa juzi nilikutana na kijana mmoja anayefanya hili zoezi analalamika wanafanya kazi karibu wiki sasa hawajalipwa hawana nauli mara malipo yao hayajulikani ni kiasi gani hadi sasa,mafunzo yao yalijaa mizengwe wanaofundisha huku chini hawajaelewa vizuri sasa wanawaelimishaje wenzao.
Nimewakuta mtaani kwetu wanaandika namba kutani na mikaa, hawana vyombo vya kazi na unaweza kudhani ni vishoka
 
Sijui nitakuwa sawa au la! Kuna usemi unasema "vya bure aghali"

Mwanzo nilisikia hili zoezi litafanywa na wafanyakazi wa wizara na ingetumika kama bilion 600. Sasa sijui wizara nayo walipanga bajeti kubwa kiasi hicho kwa nini! Wao ndio wanajua!

Baadae ikaonekana wawatumie halmashauri ili kupunguza gharama. Kweli wamefanikiwa kupunguza gharama na kufikia bilioni 27.

Wakurugenzi nao wakaona hii ndio fursa ya kupiga hela pamoja na watendaji wao wa chini kama vile watendaji wa kata, vijiji na mitaa.

Kuna maeneo ni kama hili zoezi limekwama, na kujaa ubabaishaji.

Kwa mfano, yanachukuliwa majina ya waliofanya usaili kimya kimya kwa ajili ya ushahidi wa malipo, ila hao watu hawapewi kazi na wakati mwingine hawajulishwi. Badala yake, wanawatumia wenyeviti wa vitongoji kwenye hili zoezi na kuwalipa elfu tano badala ya elfu 20 iliyopangwa. Elfu 15 inatiwa mifukoni mwa hao watendaji.Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hili zoezi lilitakiwa lifanywe na wizara husika ambayo ingetoa ajira za mkataba na kutoa semina ya kutosha, tofauti na sasa ambapo ni vurugu tu. Kwa kifupi hili zoezi limebuma!

Warudi wakajipange upya!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom