Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,500
- 9,279
Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amemteua Therese Coffey kujaza pengo ambalo limeachwa wazi na waziri wa ajira na pensheni Amber Rudd ambaye amejiuzulu kwa kutokubaliana na namna ambavyo Johnson anaendesha mchakato wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya-Brexit.
Kujiuzulu kwa Rudd kumekuwa pigo kwa Johnson anayekabiliwa na ukosoaji mkali kufuatia hatua zake kama vile kuahirisha bunge, kuwafukuza wabunge kutoka kwenye chama chake na kuitisha uchaguzi wa mapema.
Johnson ameapa kuiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya ifikapo Oktoba 31, iwe kwa makubaliano au bila ya makubaliano.
Coffey ambaye ni waziri wa mazingira na mbunge wa Suffolk mashariki mwa England alipinga Uingereza kujitenga na Umoja wa Ulaya wakati wa kura ya maoni