#COVID19 Waziri wa Afya upimaji wa COVID-19 Airport ni kero. Gharama sijui unafanya kazi gani?

muzi

JF-Expert Member
Jun 17, 2016
1,038
1,448
Tanzania tunatia aibu, nimesafiri kwenda nje nikapimwa na kupewa certificate na kulipa pesa. Baada ya kufika nje nilionyesha certificate wakagonga muhuri nikaendelea na shughuli zangu.

Baada ya kumaliza pilika pilika nikapima kule nje baada ya kufika Dar eti wanalazimisha kupima tena, kuwaonyesha certificate niliyopewa kule jana yake hawataki kujua wala kusikia, njaa zao wakupige $100 hata sidhani kama wanapima.

Kwa kweli inakera sana, mbona certificate zetu kule wanatambua na kuheshimu?

Kwanini certificate ambayo mtu kapima ndani ya 24-48 hours hamziheshimu?

Kama ni njaa ya fedha mmeshidwa kutafuta toka kwenye vyanzo vingine?

Watu wengi foleni kubwa wameacha na ndege za kuunga kwenda kwingineko

Hii ni kero TWO TO THREE MONTHS LEO, Waziri wa Afya kimya, haongei chochote, tangua ameacha kukimbia mazoezi ya kunywa sijui nini nothing is working. Katika awamu zote hatujawahi kuwa na waziri ya afya worse kama huyu, shughuru mama ana huruma ungeshatumbuliwa mapema. Hii kero imeshaletwa humu lakini waziri kama vile haoni


AIBU SANA!

1621343672615.png
 
Serikali ya majambazi. Eti ukiondoka $100 ukirudi $100 huyu mama aje uswahilini ajue maisha yalivyo magumu. Tangu 1977 anakula kuku kwa mrija hawezi kujua watu wanavyolala njaa huku.
 
Tatizo mamlaka husika zimetulia zinavuna hela
 
Tanzania: hakuna corona.

wajuaji:kwe kwe kwe kweeeee kweeee

Tanzania: Haya tunaweka vipimo

Wajuaji: Yamewashuka walibisha nini sasa

Tanzania: Vipimo lazima na gharama hizi hapa

Wajuaji: uwiiii,yelewiiii oweeee oaaaaah tunataka chanjo vipimo gharama. usumbufu huuu,serikali wezi
 
Inakuwaje tunawalazimisha watu kupima Airport wakati wametoka nchi kama Marekani ambako wamechanjwa na ushahidi wanao ? Marekani huwezi kupanda ndege kama hujachanjwa!! Tuachane na mihemko kwasababu tumechelewa kuikabili corona hivyo tunafanya mambo yasiyoeleweka!

Kama ni kodi waTanzania wanalipa ya kutosha wanastahili kupima bure!!
 
Mimi nadhani katika hili wamekurupuka nchi zote kabla unaonesha certificate ziko nchi 96 hours na ziko 72 Hrs hiyo ni standard na ziko nchi chache unatakiwa upimwe airport na inategemea unatoka nchi gani. Hili sio tatizo lakini kwa Tanzania ni tatizo kubwa tu sababu corona sio kwamba ni ugonjwa haupo nchini upo tayari na maambukizi ya ndani yapo ingelikuwa ndio umeanza huko nje unazuia sawa lakini miaka miwili tumeshapigika sana leo ndio tunaamka kumekucha. Ok kaja Mtanzani anarudi kwake kapima positive utamfanya nini? sana sana utamwambia jitenge nyumbani kwako na je mgeni utamfanya nini? kumrudisha au maana sio clear. Sote tunajuwa issue hii iko India zuia mtu yoyote katika siku 14 kama kapita India kupima au quatantine lakini sio kila abiria. Mimi sijui lakini hili halijakaa sawa wakati dunia inafunguka airport nyingi sisi ndio tunafunga haya mambo miaka miwili ilikuwa shida kusafiri leo nchi zote masharti yanalegezwa hasa ukiwa na chanjo basi tena no PCR sisi utasema tumeamka usingizi tutaachwa nyuma tu na wenzetu. Corona ipo ndani wala haitoki nje.
 
Waziri wa Afya ameshashindwa tafadhali Mh. Rais SSH msaidie kazi huyu mama, akafanye shughuli nyingine.

Sijui kwanini viongozi wetu ni wazito !!
 
Hizi zilikuwa ni sheria Kayafa alipokuwa ameshika hatamu!
..sio kila jambo asingiziwe mwendazake.

Kama ni yeye basi kwann hawaondoi jambo hilo sasa?
Haswa baada ya mwendazake kufariki?

Magufuli amefariki mambo ya kupima corona ukirudi nyumbani yalikuwa hayapo.
Sasa nani kaweka kupima corona ukirudi Tanzania kama sio utawala wa sasa?

Kelele zipigwe kwa walioshika hatamu sasa watoe huo upuuzi.

Duniani kote unapimwa corona unapotoka na sio unapoingia.

Serikali yetu iwe na huruma kwa raia zake.
Nasema imetosha sasa....

Nimeondoka nimetoa 230000 covid + 25000 gharama za hospital.
Na bado nirudi nilipe tena 230000?

Mimi nakuja hapo na sitoi sent tano,
Tuone mtanipeleka wp..?
 
Back
Top Bottom