Waziri wa Afya unafahamu lolote kuhusu ubabaishaji huu ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa Afya unafahamu lolote kuhusu ubabaishaji huu ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndebile, Nov 12, 2011.

 1. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  leo ni siku ya kwanza ya chanjo ya kitaifa ya surua,watumishi wa afya hasa wauguzi jana walipewa semina elekezi ya siku moja. Malipo ya semina hiyo hapa Mwanza waliambiwa ni sh.15,000 tu! Nayo hawakupewa kisa eti hela haijatumwa kutoka wizarani hivyo maskini wauguzi hao waliikopesha serikari sijuhi watalipwa lini?alafu kiwango hiki cha hela ni posho,takrima,nauli au nini?maana hakipandi ni miaka 4 sasa wanalipwa hivi,hivi muuguzi hawezi kupanda hata tax, 15,000 kwa siku inaweza kumkimu mtu kwa kitu gani? Pamoja ugumu wa shughuli yenyewe, maana itajumuisha pia kutoa sindano kituo kimoja amepangwa muuguzi mmoja tu!ndio maana wauguzi wanajeruhiwa na sindano kwasababu ya over working! na mwisho malipo ni sh. .10000 tu kwa siku! Hebu jaribu kuwalipa wabunge msimbazi moja tu kwa siku muone kama hapatachimbika. Na kwanini muanzishe kampeni hii kama hakuna pesa za kutosha?usalama wa afya watoto wetu ukoje kwa hawa manesi walioikopesha serikali posho zao ambazo hata nauli haitoshi?
   
 2. V

  Vitalino mlelwa Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unashangaa hilo mi nimeajiliwa wilaya ya mbeya vijijini idara ya afya toka mwezi Wa tano kifupi na miezi saba hadi leo sijaingia kwenye paylaw na ukifuatilia unaambiwa tunafuatiliwa wizarani hadi huwa sielewi iv kuajiriwa selikalini ni adhabu au kwasababu kuna rafiki yangu alikaa miezi kumi na moja hadi alipoamua kwenda mwenyewe wizarani akatoka baada ya mwezi moja sasa utawala wa shelia uko wapi na kama sisi tunafanya kazi ya kufatilia wizarani hawa wanaohusika wanalipwa mishahara ya nini huwb najutia sana ktajiriwa hapa kwahiyo ubabaishaji afya kawaida wala usishangaeg.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,871
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  paylaw!
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  well well well.... paylaw!! i think it is payroll,
   
 5. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,866
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Kwa mujibu wa mratibu wa zoezi hilo la Chanjo Anthony Mwakemwa, chanjo hiyo dhidi ya maradhi mbalimbali ikiwemo surua, itatolewa kwa siku nne kuanzia tarehe 12 -15 Novemba mwaka huu. Matone hayo ya chanjo yanatarajiwa kutolewa kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano (5), ambapo zoezi hilo hadi kukamilika kwake linatarajiwa kuwafikia watoto zaidi ya milioni 6 katika vituo zaidi ya 45,000. Chanjo hiyo kwa watoto inalenga kuwawekea watoto kinga maalumu dhidi ya maradhi mbalimbali sugu, hususani surua, polio na magonjwa mengine yanayoambatana na hayo. News / Event | Raisi kuzindua chanjo ya watoto Arusha — Dar411

  Nina imani kuwa serikali haiwezi kujiwekea malengo makubwa kama hayo (kuwafikia watoto zaidi ya milioni 6 katika vituo zaidi ya 45,000) halafu iwe na bajeti kiduchu ya kuwapa watekelezaji. Je wakiamua kuingia mitini na hizi chanjo wakazitupa porini nani alaumiwe???
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Hivi nyinyi hata mnapopewa semina mnalipwa nje ya mshahara wenu? bahati yenu, huwa mnakwenda kwenye semina au kwenye hizo 15,000/=?
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  nimeajiliwa = nimeajiliwa
  paylaw = payroll
  shelia = sheria

  Tena inaonesha wewe ni daktari.
   
 8. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  hawa jamaa sijuhi kama wanaelewa wanachokifanya!
   
 9. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  FaizaFox acha upupu wako kwenye mambo ya afya za watoto! Mtu anatoka kituo chake cha kazi umbali wa km 49 kuhudhuria semina,nauli,chakula,usumbufu n.k asilipwe? Matokeo yake vitoto vyetu vinachomwa sindano na wauguzi wenye njaa na kupata majipu,
   
Loading...