Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu liangalie hili njama zinazofanywa na Madaktari na watu wa Maabara

Jun 17, 2020
75
268
Hosipitali hasa za Wilaya kuna tabia moja ya madaktari kula njama na watu wa maabara kupima kila kipimo ni Tsh. 2000!.

Mgonjwa akienda kwa Daktari akimweleza dalili za ugonjwa daktari anamwandikia vipimo zaidi ya vinne! Na ili mgonjwa akapimwe mpaka akalipie kwanza. Hii imekuwa kero kwa wananchi wa kipato cha chini!.

Daktari uliyesomea na kuwa qualified napata mashaka hata kama hana uhakika zaidi ya vipimo vinne?.
 
Utakatifu na haki,

Sasa mkuu ulitaka akapime kwanza ndio alipie?akipima halafu akakataa kulipia?

Halafu gharama za vipimo zinatofautiana na kipimo chenyewe,haiwezekani kipimo mfano cha hepatitis B kikawa sawa na kipimo cha malaria

Ulikuwa unasuggest kipimo cha elfu mbili kiwe shilingi ngapi?
 
Sasa mkuu ulitaka akapime kwanza ndio alipie?akipima halafu akakataa kulipia?

Halafu gharama za vipimo zinatofautiana na kipimo chenyewe,haiwezekani kipimo mfano cha hepatitis B kikawa sawa na kipimo cha malaria

Ulikuwa unasuggest kipimo cha elfu mbili kiwe shilingi ngapi?

Inshu sio ku-suggest kiwango cha vipimo kipimo hata kikawa 5000 5000,hamna shida,tatizo linatokea pale ambapo hata dalili za awali unaweza hata ww kujua tu hii ni malaria au sio malaria, sasa dakitari uliyesomea kabisa unapredict zaidi ya magonjwa manne au hata matano! Huoni hilo ni tatizo? Huoni kuna mazingira ya Rushwa yanatengenezwa! Kwa nn usiwepo utaratibu mzuri.
 
Nitapambana Na Rushwa Bila Kigugumizi Chochote Na Dawa Ya Jipu Ni Kulitumbua
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Inshu sio kusaggest kiwango cha vipimo kipimo hata kikawa 5000 5000,hamna shida,tatizo linatokea pale ambapo hata dalili za awali unaweza hata ww kujua tu hii ni malaria au sio malaria!,sasa dakitari uliyesomea kabisa unapredict zaidi ya magonjwa manne au hata matano! Huoni hilo ni tatizo? Huoni kuna mazingira ya Rushwa yanatengenezwa. Kwanini usiwepo utaratibu mzuri.

Dalili zinaingiliana mkuu,unaweza kuwa na tatizo la kuwashwa ukatakiwa kupima kipimo zaidi ya kimoja ili kujua muwasho unasababishwa na nini

Hata hiyo malaria unayosemea dalili zake zinaingiliana na baadhi ya magonjwa mengine
 
Hosipitali hasa za Wilaya kuna tabia moja ya madaktari kula njama na watu wa maabara kupima kila kipimo ni Tsh. 2000!

Mgonjwa akienda kwa Daktari akimweleza dalili za ugonjwa daktari anamwandikia vipimo zaidi ya vinne! Na ili mgonjwa akapimwe mpaka akalipie kwanza. Hii imekuwa kero kwa wananchi wa kipato cha chini!

Daktari uliyesomea na kuwa qualified napata mashaka hata kama hana uhakika zaidi ya vipimo vinne?


Jiwe kasema mujifukize na kula malimau na tangawizi,hospitali umefuata nini wewe kula vitunguu swaumu na mwarobaini.

Mkuu umeshapewa shati na kofia ya kijani?
 
Hosipitali hasa za Wilaya kuna tabia moja ya madaktari kula njama na watu wa maabara kupima kila kipimo ni Tsh. 2000!

Mgonjwa akienda kwa Daktari akimweleza dalili za ugonjwa daktari anamwandikia vipimo zaidi ya vinne! Na ili mgonjwa akapimwe mpaka akalipie kwanza! Hii imekuwa kero kwa wananchi wa kipato cha chini!

Daktari uliyesomea na kuwa qualified napata mashaka hata kama hana uhakika zaidi ya vipimo vinne?
Tatizo ni miongozo ndugu yangu
Mfano=mwanzo ilikua inaruhusiwa kutibu clinical malaria yaani daktari au nurse amemuona mgonjwa anayo kila dalili ya malaria basi ilikua inaruhusiwa atoe tiba ya malaria kwa mgonjwa huyo hata kama hakupima,lakini sasa hivi ni lazima apime kwanza then akishakua positive ndio apewe dawa kama inatokea mgonjwa ana kila dalili ya ugonjwa husika na kipimo kimeonyesha negative huruhusiwi kumpatia tiba ya ugonjwa huo.

Mfano=amekuja mgonjwa ana kila dalili ya malaria lakini umempima kwa MRDT ambayo kimsingi parasite chini ya kumi kwenye kipimo hiki majibu yatasoma negative yaani mgonjwa ana wadudu 9,8........1 kwenye MRDT hawatoonekana hivo basi hutoruhusiwa kumuanzishia tiba ya malaria hata kama ameonyesha dalili zote ama kadhaa za malaria.

Pia inaleta walakini kwa mgonjwa ambae mfano amepima malaria akawa negative huko maabara lakini kwa daktari inaonekana amepewa tiba ya malaria kwa sababu daktari ameona Kua mgonjwa anayo kila dalili ya malaria itaonekana kua dawa hizo zimepigwa kwasababu anapewaje dawa ya malaria mgonjwa asie na malaria hapa watu wa AUDITING watakusumbua


Hope nimeeleweka kidogo maana sio mwandishi mzuri,ahsante
 
Mleta mada uko sahihi. Hiyo Tabia ipo Sana kwenye hizi maabara. Nilimpeleka wife sehemu kupima malaria, jamaa ananiambia eti tupime na kichocho, typhod, na mimba.

Na muda huo keshaandika kabisa kwenye karatasi yake. Nilimkazia jicho yule bwana nikamwambia hivyo vingine tutapima siku nyingine akanywea. Nilipotoka pale nikajua janja yao ya kufosi kupata pesa kihuni.
 
Na hata kama ungechukuliwa kipimo kimojakimoja ungelalamika tu maana wanapima hichi huna hichi huna unarudia Tena huna mpk hata Mara ya tano!.. ukitoka hospitali unatoka umekunja sura kama ulikuwa umelazimishwa kwenda😂
Mkuu kuwa mpole tu wachukue vya jumla wanaweza kugundua na mengine yanayonyemelea.. hiyo ni afya sio siasa.
 
Inshu sio ku-suggest kiwango cha vipimo kipimo hata kikawa 5000 5000,hamna shida,tatizo linatokea pale ambapo hata dalili za awali unaweza hata ww kujua tu hii ni malaria au sio malaria, sasa dakitari uliyesomea kabisa unapredict zaidi ya magonjwa manne au hata matano! Huoni hilo ni tatizo? Huoni kuna mazingira ya Rushwa yanatengenezwa! Kwa nn usiwepo utaratibu mzuri.
Sasa kama ww wajua ni malaria au si malaria waenda hosp kufanya nn? Watu kama nyie ndio mnazingua sana dawa yenu kuwaandikia vipimo 10 kabisa naona hivyo vi4 havikutoshi, wenzio huwa waja hosp kwaajili ya vipimo, kama ww wajua una malaria nenda duka la dawa
 
Mleta mada uko sahihi. Hiyo Tabia ipo Sana kwenye hizi maabara. Nilimpeleka wife sehemu kupima malaria, jamaa ananiambia eti tupime na kichocho, typhod, na mimba. Na muda huo keshaandika kabisa kwenye karatasi yake. Nilimkazia jicho yule bwana nikamwambia hivyo vingine tutapima siku nyingine akanywea. Nilipotoka pale nikajua janja yao ya kufosi kupata pesa kihuni.
Hayo ni makubaliano yenu na ww uliyakubali sasa walia nini?
 
Back
Top Bottom