kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,635
- 7,005
Wengi sana kwa sasa wapo hawana kazi,na wengine wanabadili taaluma baada ya kuona ajira nyingi wanachukua manesi wanaokubali kulipwa kidogo.Na ukifuatilia wengi pia wana vyeti vya kughushi.Mifano ninayo na kama wakaguzi wangekuwa makini kidogo tu,wangegundua.Hats hivyo baadhi ya wakaguzi wanajua,ila rushwa za ngono zinahusika sana.Nina ushahidi wa mtu ambaye hadi hivi ninavyoandika yupo famasi kama nesi lakini ameghushi cheti.Ole wako basi ujipeleke kimbele mbele kumripoti,utashangaa unaanza kupata vikesi na misuko suko mingi.Huku afya Ummy hana wasaidizi kabisa,wengi wanafanya kazi kwa mazoeaKuna ma technician wangapi nchini kukidhi mahitaji? Licence ya pharmacist mmoja inaweza kutumia hata na maduka matatu.
Sent using Jamii Forums mobile app