Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, aagiza kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na Meneja udhibiti na ubora

Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
17,514
2,000
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwasimamisha kazi Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Dr. Nyambura Moremi na Jacob Lusekelo Meneja uthibiti na ubora ili kupisha uchunguzi.

Sasa wameanza kushughulika na wataalam badala ya kudeal na Corona

66420D51-6E73-4DA0-90FE-953B9D36EC22.jpeg

Dr. Nyambura Moremi

13D5A3EF-D6F0-40F5-9683-F13190A0D9A9.jpeg
 

RAYAN THE DON

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
646
1,000
Hongera zake ingawa hii kamati haipo sawa/ huru kwa sababu imesheheni wataalamu wetu wa afya ambao wanaweza kulindana kwa namna moja au nyingine.

Ingekuwa vyema kama wataalamu wa kada zingine wangewekwa katika kamati hiyo ili kuweka mizani katika hali ya usawa.
 

secret file

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
2,244
2,000
Ni muhimu wangepata na wataalam independent kutoka nje ya Tz lkn ndani ya bara la Afrika
 

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
2,477
2,000
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi Dkt. Nyambura Moremi (Mkurugenzi) na Bw. Jacob Lusekelo (Meneja Udhibiti wa Ubora) kupisha uchunguzi.

Hilo limekuja baada ya hotuba ya Mh. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa JMT hapo jana Mei 3, 2020 ambapo alibainisha changamoto na mapungufu ya utendaji wa maabara hiyo.


Sent from my TECNO AX8 using Tapatalk
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
5,834
2,000
Ni sawa "kusimamishwa" kupisha uchunguzi ni taratibu za kawaida duniani Kote nadhani.

Hawajafukuzwa hawa watumishi. Na kuwa mkurugenzi haimaanishi yeye ndiye hupima, wao ni wasimamizi wa wafanyakazi wengi.

Tuwape muda wafanye kazi yao, tusianze kuwa hukumu kabla.

Vinavyochunguzwa vingi naamini, watu uzoefu na taaluma zao hasa wahusika, machines zenyewe, chemicals/ reagents.
Na vingine tusivyo vijua.

Hivyo tuwape muda watuletee majibu.
 

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
10,378
2,000
Hongera zake ingawa hii kamati haipo sawa/huru kwa sababu imesheheni wataalamu wetu wa afya ambao wanaweza kulindana kwa namna moja au nyingine. Ingekuwa vyema kama wataalamu wa kada zingine wangewekwa katika kamati hiyo ili kuweka mizani katika hali ya usawa.
Ukiona hivyo ujue nyuma yao kuna wanaowachunguza,kwahiyo nina Imani mambo yatakuwa sawi tu...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom