Waziri wa afya Ummy Mwalimu aadhimisha siku ya Malaria Duniani kwa kupima Malaria

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
Waziri wa afya Ummy Mwalimu aadhimisha siku ya Malaria Duniani kwa kupima Malaria

Aprili 25 kama ulikuwa hufahamu ni siku ya Malaria Duniani.Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ameadhimisha siku hii kwa kupima malaria.

Waziri Ummy amewataka Watanzania kwa pamoja kuungana kupambana na ugonjwa wa Malaria ili kusaidiana na serikali kutokomeza ugonjwa huo ambao husababisha vifo vya watu wengi nchini.

“Msisitizo mkubwa wa Wizara yangu ni kwa wananchi na wadau wote kuona umuhimu na kutoa kipaumbele katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria kwa kuhakikisha matumizi sahihi ya mikakati iliyopo katika kuuthibiti ugonjwa huu,

“Iwapo mikakati hiyo itatekelezwa ipasavyo ni dhahiri kuwa maambukizi yataendelea kupungua kwa kiasi kikubwa na hatimaye kumaliza kabisa tatizo hili,” alisema Waziri Ummy.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom