MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,011
- 2,181
Katika nchi hii tumetapeliwa kwa njia tofauti kwa vipindi tofauti. Tulishakutana na Ngetwa, tukakutana na mzee wa Loliondo, walikuwepo akina ng'wizukulu sijui nani, sasa wapo akina Mwaka, nk. Wote hawa wanajineemesha kwa udhaifu wa uelewa wetu na pia ukosefu wa vyombo imara vya kisheria kuwadhibiti watu kama hawa.
Leo hii ktk ch. 10 nimemuona huyu Mwaka ambaye anajiita Doctor akiwa anajitetea na kujaribu kujibu yaliyotokana na ziara ya naibu waziri ktk hiyo kliniki yake. Kwa haraka unaweza ukagundua tu kwamba ni mtu asiye na msaada ktk sekta ya afya. Ni mtu anajipatia riziki kwa watu waliokosa matumaini. Watu wa aina ya Mwaka wanaojidai kutoa tiba mbadala au tiba ya asili ni wengi na kama ilivyokuwa kwa mzee wa Loliondo, wanapata umaarufu sana jijini Dar! Inaonekana Dar ni kitovu cha watu waliopoteza matumaini. Kuna mambo mengi ya hovyo hovyo yanafanikiwa sana Dar. Watu wanalipa gharama kubwa za matibabu bila faida yoyote!
Naomba nitoe wito kwa wizara ya afya. Hata kama huduma zetu mahospitalini ni mbaya, hii isiwe sababu ya kusajili watu wa aina hii na kuwafanya kwamba ni watoa tiba mbadala inayoweza kutumainiwa na wa TZ. Fungeni vituo hivi na kama sheria inaruhusu, fanyeni marekebisho ya haraka kama inavyofanywa kwa PPRA. Afya za watanzania hazistahili kuwa chini ya dhamana ya matapeli.