WAZIRI WA AFYA NJOO MUHIMBILI KITENDO CHA FIGO UTUMBUE MAJIBU

Dazzle 2

Senior Member
Oct 9, 2015
125
71
Pamoja na Rais JPM kufanya ziara ya kustukiza muhimbili pia wafuatao walitembelea muhimbili ambao ni katibu mkuu kiongozi na leo hii Naibu waziri mh Dr Hamis Kingwagala ametembelea hospitali hii.

Pamoja na viongozi wote hawa kutembelea muhimbili takribani wote hakuna aliyetembelea kitengo cha wagonjwa wa figo ambacho kimejaa matatizo kibao. Pamoja na umuhimu wa kitendo hiki ni mara chache sana unaweza kuwakuta madaktari kwani muda mwingi manesi huachiwa kufanya kila kitu bila kujua changamoto za wagonjwa wa aina hii.

Jambo la pili kuna ushirikiano mdogo sana kati ya madaktari na manesi katika kuhudumia wagonjwa. Jambo hili ni hatari sana maana inapotokea dharura inayohitaji Dr inakuwa ngumu maana wengi wanaingia kusainia tu wagonjwa homu na kuongoka eneo la kitengo.

Kuna wakati vifaa na madawa kama vile heparin injection, bags nk vinakosekana. Waziri na msaidizi wako tunaomba mmulike kitengo hiki na utendaji wake wa kazi maana inavyoonekana kasi ya hapa kazi tu hawaiwezi
 
Back
Top Bottom