Waziri wa Afya: Ni marufuku kabisa kutaja majina ya wagonjwa wa Corona, Mwana FA, Sallam na Isabela walijitangaza wenyewe siyo Serikali

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,462
141,163
Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema ni marufuku kwa mtu yeyote kutangaza majina ya wagonjwa wa corona kwani hiyo ni siri kati ya Daktari na mgonjwa.

Waziri amesema kutaja taja majina kunaleta unyanyapaa kitu ambacho ni kibaya sana mbele ya jamii na mbele za Mungu. Na zaidi Ummy amesema ndio maana hata yeye na mwenzie Hamad wa Zanzibar huwezi kuwasikia wakitaja majina zaidi ya yale ya Isabela, Mwana FA na Sallam ambao walijitangaza wenyewe.

Waziri Ummy amesema ni marufuku pia mtumishi yeyote wa Serikali kutoa takwimu na taarifa za wagonjwa wa Corona zaidi ya yeye Waziri, Waziri mkuu na Rais mwenyewe.

Source ITV habari!
 
Tulimaliza kutaja siku ile , il tumuumbue Mbowe,maana.technically aliomba ugonjwa huo uingie nchini.
Kazi ilikwisha siku ile
 
  • Nzuri
Reactions: UCD
Makonda msema ovyo sijui kama amemsikia waziri wa Afya maana yule jamaa mdomo wake anaujua yeye mwenyewe
 
Banana republic. Mawaziri wanauzunguka mbuyu tu. Seems Mr. Bashite is above and beyond the laws
 
Back
Top Bottom