Waziri wa Afya: Ni marufuku kabisa kutaja majina ya wagonjwa wa Corona, Mwana FA, Sallam na Isabela walijitangaza wenyewe siyo Serikali

Hili bulldozer sijui lilizani Corona kama madawa ya kulevya!! Linaweza piga mpunga kwa kutisha watu!
 
Hadi sasa haieleweki vizuri kama kwa mfano wakuu wa mikoa kwa nafasi yao ya Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama hawaruhusiwi " kuwafichua" wagonjwa wa Coroma popote walipo.

Nafikiri litoke tamko rasmi ili kuepusha LIGI na utata unaoweza kujitokeza.

Maendeleo hayana chama!
 
Ukimwi sawa, lkn huu wa mlipuko wa kuambukizwaaaa? huyo waziri akasome tena, simuamini sana sijui kwa nini!...

Boris Jonson katajwa sembuse wewe maskini? sijui kwa nini wabongo wanamadhaifu ya kunyanyapaliwa!

Self isolation ni uelewa wa kujali Afya za wengine, hasa familia yako pendwa! uzanakini wanasema mficha maradhi ni kiriro kiri mubhona!
 
Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema ni marufuku kwa mtu yeyote kutangaza majina ya wagonjwa wa corona kwani hiyo ni siri kati ya Daktari na mgonjwa.

Waziri amesema kutaja taja majina kunaleta unyanyapaa kitu ambacho ni kibaya sana mbele ya jamii na mbele za Mungu. Na zaidi Ummy amesema ndio maana hata yeye na mwenzie Hamad wa Zanzibar huwezi kuwasikia wakitaja majina zaidi ya yale ya Isabela, Mwana FA na Sallam ambao walijitangaza wenyewe.

Waziri Ummy amesema ni marufuku pia mtumishi yeyote wa Serikali kutoa takwimu na taarifa za wagonjwa wa Corona zaidi ya yeye Waziri, Waziri mkuu na Rais mwenyewe.

Source ITV habari!
makonda ametaja majina hadharani,ila angekuwa lema ,sijui angekuwa hali gani,makonda kama baba wa taifa hili haguswi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom