Waziri wa Afya ni bora ungeanza na mchakato wa Bima ya Afya kwa kila Mtanzania kuliko kutoa agizo kama hili

What does service costing entail?

Based on the above evidence of running heath services in Tanzania.

How should society top up given the current government allocation on health expenditures; how much is the deficit given the estimated costs?

Come up with an argument based on that scenario then I can give you a discussion, otherwise acha kurupoka.

Asubuhi njema.
Offpoint. Na kwa post kama hii ni dhahiri kuwa wewe ni mbulula.
 
Eti mchango wa elfu 20 utibiwe figo kiukweli ni ndoto za mchana kweupe,maana hizo bima za kulipia milioni 2 kwa mwaka bado zinabagua baadhi ya magonjwa.
Mbona mnawaza figo na magonjwa makubwa kama kisukari/Bp wakati malaria ndio inaongoza kuua akina mama na watoto wenye umaskini.
 
Mbona mnawaza figo na magonjwa makubwa kama kisukari/Bp wakati malaria ndio inaongoza kuua akina mama na watoto wenye umaskini.
Sasa malaria tiba yake ni nyepesi kuna vimaabara vingi mtaani wanapima kwa buku 3 tu,na dawa pharmacy zinauzwa elfu 5.
Ni pesa ambayo mtanzania wa kawaida anaweza kumudu.
Lengo la kuwa na bima ni kujiandaa endapo utapata ugonjwa mkubwa ambao hautamudu gharama zake ndipo hapo bima itakusaidia.
 
Sasa malaria tiba yake ni nyepesi kuna vimaabara vingi mtaani wanapima kwa buku 3 tu,na dawa pharmacy zinauzwa elfu 5.
Ni pesa ambayo mtanzania wa kawaida anaweza kumudu.
Lengo la kuwa na bima ni kujiandaa endapo utapata ugonjwa mkubwa ambao hautamudu gharama zake ndipo hapo bima itakusaidia.
Madhara ya kukariri maisha ya kwenye mitandao ya kijamii. Kuna familia nyingi sana hata kupata 3000 kwa siku ni kazi.
 
sawa najua kuna watu kama hao kijijini ila zahanati za vijijini zina utaratibu wao tofauti na mijini.
Sidhani kama vijijini wanalipishwa elfu 10 kumuona dokta.
Madhara ya kukariri maisha ya kwenye mitandao ya kijamii. Kuna familia nyingi sana hata kupata 3000 kwa siku ni kazi.
 
Wana JF poleni na pilika pilika za sikukuu.

Kama kichwa cha uzi kinavyojitanabaisha niseme kuwa agizo la waziri wa afya sio zuri kwa mustakabari wa watanzania.

Watanzania wengi tunaishi maisha ya kubahatisha,wengi tunatafuta chakula. Habari ya matibabu huwa ni dharula ndio maana tukiugua au kupata mgonjwa huwa tupata tabu sana.

Kitendo cha waziri mwenye dhamana ya afya zetu kuagiza hospital ziwe zinatukaba tuwe tunalipa gharama ya matibabu kabla ya bahati mbaya ya kufariki haijatokea ni habari mbaya.

Chukulia mkulima wa kijijini ambae amegongwa nyoka na kukimbizwa hospital atapata wapi pesa za kulipia haraka ili atibiwe na asifariki? Mama wa kijijini ambae amepatwa malalaria ghafla ataweza kumudu haya aliyoagiza waziri wa afya?

Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu,hoja ya bima ya afya kwa kila mtanzania iliibuka na kuwa gumzo. Uzuri rais Magufuli kwa kujibu mapigo ya wapinzani alisema suala la bima ya afya lipo kwenye ilani ya Ccm. Na itakuwa bima ya afya kwa watanzania wote.

Waziri wa afya alitakiwa kwa nia njema ya watanzania maskini ambao anajua ndio huwa wanakwama kupata maiti za wapendwa wao ahakikishe bima ya afya kwa kila mtanzania inapatikana haraka ili tusije kupoteza maisha kwa kukosa matibabu maana kiuhalisia ni ngumu kuwa na cash wakati wote.
Naunga mkono hoja, tena naunga sana.
Haya matamko ya kisiasa yasiyozingatia hali halisi ifikie mahali wananchi tuyakemee.
Hawa hawa Mawaziri ndio wanaowakemea na kuwafokea Madaktari hasa MaDMO pale mapato ya hospitali yanapopungua, lakini Leo mtu yuleyule kwa vile anajua kuna jambo linakera wananchi anakuja na tamko la jumla jumla huko akijua tamko lake litasababisha wananchi sasa wasubiri matibabu hadi hadi pale watakapolipia. Anajua vizuri masharti waliyopewa maDMO ambao ndio wenye mamlaka ya kutoa misamaha ya malipo. Hawa siyo kwamba wanatoa misamaha kiholela bali mpaka upate huo msamaha mgonjwa atakuwa marehemu.
Tangazo alilotoa Dr Gwajima halina tofauti na maagizo ya LUGOLA aliyekuwa anakemea ukamataji wa Askari wa Usalama barabarani, akitoka kwenye Media anawahenyesha maRPC kwa nini makusanyo ya adhabu za barabarani yanapungua?
Suluhisho la wananchi kutoingia kwenye fedheha hizi za maiti ndugu ya ndugu yao kuzuiwa mortuary ni kila familia kuwa na Bima ya Afya inayojitosheleza, ambayo gharama zake zinahimilika nchi nzima. Kitendo cha Chama chake kurukia hoja iliyoandaliwa na Upinzani bila kutafiti misingi yake inatupeleka kwenye janga kama la Elimu Bure ambayo imegeuka kuwa Bure kabisa kama jina lake. Waliporukia Bima ya Afya tulijua kwa vile afya ni jambo la kwanza kabla ya yote, sasa hivi lingekuwa ndo jambo linalohimizwa na kuwekewa mikakati kila kona ya nchi, lakini tunaona sarakasi za Maiti kutozuiwa bila mbadala. Yaani Waziri anataka kuwaambia watanzania kwamba serikali haina tatizo na gharama za matibabu, ETI wenye tatizo ni Madaktari ndo wanaonea Wananchi. Kwamba Madaktari wetu ndo wana roho mbaya na sisi wakati hawana maslahi yoyote na hela tunazotoa. Kweli Madaktari hawana maslahi na fedha hizi wakati mmewapa kauli ya "KUTENDA KAMA WENYE MALI?". Tabia ya wanasiasa kubambika kesi kwa Watumishi ni ya kukemea sana, hawa ni waongo wanaotaka wananchi wawachukie watumishi huku wao kama wawezeshaji wakiwa hawatimizi jukumu la uwezeshaji.
 
Mshahara wake unatokea wapi?

Kwanini nilipie kumuona kama anafanya kazi taasisi ya serikali?

Can you justify that kwenye service costing za serikali?
Duniani kote kuna mortuary cost,hapo labda useme garama wafanye ziwe nafuu na siyo za kukomoana
Narudia tena dunia ya leo hakuna cha bure mzee kila kitu watu wanataka maslahi

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Katika mambo ambayo Waziri alipaswa kujipa muda wa kufikiria kabla hajatamka ni kama hayo.

Nadhani Hospitali waliona njia pekee na rahisi ya kurudisha gharama za matibabu kutoka kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Mgonjwa basi ni wakati wanapoandaa mazishi yake....kwa tamaduni zetu nyingi sisi Wabongo ni rahisi zaidi kuchangishana wakati wa msiba kuliko wakati mwingine wowote, ukiondoa kuchangia harusi....Hivyo wakati inatafutwa milioni tatu ya mazishi wajue kuna milioni moja ya Hospitali.

Na kama Waziri ataona hakuna haja ya kuwadai Ndugu na Jamaa kwa kuzuia maiti, sidhani kama kutakuwa na mashiko tena kuwadai wakati Mgonjwa yupo hoi kitandani na anahitaji matibabu ili kunusuru maisha yake.

Itafika mahali Hospitali zitakuwa zinasitisha matibabu pale watakapoona kwamba Mgonjwa ana nafasi ndogo ya kuishi na kuendelea kumtibia ni kuongeza mzigo kwa Wapendwa wake wanaomuhudumia pamoja na Hospitali yenyewe.

USHAURI:-kuwe na bima za dharura kwa kila Mgonjwa asiye na bima pindi tu anapofika hospitali...na bima hii iwe inalipika kirahisi na manufaa yake yaeleweke vizuri kwa Mgonjwa na Jamaa zake ile iwe rahisi kuchangishana na kulipa kwa wakati.
 
sawa najua kuna watu kama hao kijijini ila zahanati za vijijini zina utaratibu wao tofauti na mijini.
Sidhani kama vijijini wanalipishwa elfu 10 kumuona dokta.
Unakosea, hali ya masha ya watanzania ni ngumu sana iwe mjini au kijijini, majority wanahali ngumu.
 
Angalau angewekwa Faustine huyo mama nakuambia hatoboi mwaka hapo
Kwangu mimi huyu wa Waziri wa afya ndiye waziri wa hovyo zaidi.
Ni mpenda sifa na mkurupukaji.
Anafanya vitu kwa sifa na hana weledi wowote.
 
Bima ya Afya itatolewa kwa mtindo upi kwenye taifa ambalo ma jobless ni wengi zaidi ya wenye ajira?

Zaidi wataweka kiwango cha chini mwanachama kulipia kwa mwaka, lakini mwanachama huyo akiugua ugonjwa mkubwa wakuhitaji gharama kubwa hiyo bima haitamsaidia chochote, ataambiwa tena alipie, matokeo yake tutarudi kule kule.

Hapa serikali ni vyema ikatenga fungu kwa ajili ya kuwasaidia wale wataokwama kulipia gharama zote za matibabu yao.
Nafikiri ni ubunifu tu hakunana ila tukiamua kulivalia njuga linawezekana, kuna watu wana katwa zaidi ya milioni kws mwaka lakini gharama alizotumia kupata matibabu hazifiki 200000.

Maana yake ni kwamba mtu mmoja anaweza kucover huduma ya afya kws watu watano au zaidi, kukiwa na mipango mizuri inawezekana tu.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Unakosea, hali ya masha ya watanzania ni ngumu sana iwe mjini au kijijini, majority wanahali ngumu.
Yote najua hayo mkuu,wapo watu wanapiga deiwaka mjini leo amepata kesho amekosa lakini ikitokea anaumwa na hela hana kuna msaada wa ndugu,marafiki hawawezi kushindwa kumchangia elfu 10 au 20 kwa ajili ya ishu ya ugonjwa akijieleza.
 
Yote najua hayo mkuu,wapo watu wanapiga deiwaka mjini leo amepata kesho amekosa lakini ikitokea anaumwa na hela hana kuna msaada wa ndugu,marafiki hawawezi kushindwa kumchangia elfu 10 au 20 kwa ajili ya ishu ya ugonjwa akijieleza.
Sawa,hayakukuta.
 
Sisi wewe makampuni hatuwezi kuwapa bima wafanyakazi wetu kwa sababu zifuatazo

1.mfanyakazi unamlipia 10 % NSSF
2.mfanyakazi unamlipia WCF

3.mfanyakazi tena umlipie 3% Ya NHIF

4.unalipa SDL

5.unalipa kodi ya mapato

Hivi ukilipa hivyo vyote wewe unabaki na nini?
 
Hiyo ni kweli mkuu ila shida gharama zenyewe hazina uhalisia.
Kumdai mfiwa milioni 10 kama gharama ya mortuary tena kwenye hospitali ya umma haina uhalisia
Duniani kote kuna mortuary cost,hapo labda useme garama wafanye ziwe nafuu na siyo za kukomoana
Narudia tena dunia ya leo hakuna cha bure mzee kila kitu watu wanataka maslahi

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom