Waziri wa Afya ni bora ungeanza na mchakato wa Bima ya Afya kwa kila Mtanzania kuliko kutoa agizo kama hili

Wana JF poleni na pilika pilika za sikukuu.

Kama kichwa cha uzi kinavyojitanabaisha niseme kuwa agizo la waziri wa afya sio zuri kwa mustakabari wa watanzania.

Watanzania wengi tunaishi maisha ya kubahatisha,wengi tunatafuta chakula. Habari ya matibabu huwa ni dharula ndio maana tukiugua au kupata mgonjwa huwa tupata tabu sana.

Kitendo cha waziri mwenye dhamana ya afya zetu kuagiza hospital ziwe zinatukaba tuwe tunalipa gharama ya matibabu kabla ya bahati mbaya ya kufariki haijatokea ni habari mbaya.

Chukulia mkulima wa kijijini ambae amegongwa nyoka na kukimbizwa hospital atapata wapi pesa za kulipia haraka ili atibiwe na asifariki? Mama wa kijijini ambae amepatwa malalaria ghafla ataweza kumudu haya aliyoagiza waziri wa afya?

Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu,hoja ya bima ya afya kwa kila mtanzania iliibuka na kuwa gumzo. Uzuri rais Magufuli kwa kujibu mapigo ya wapinzani alisema suala la bima ya afya lipo kwenye ilani ya Ccm. Na itakuwa bima ya afya kwa watanzania wote.

Waziri wa afya alitakiwa kwa nia njema ya watanzania maskini ambao anajua ndio huwa wanakwama kupata maiti za wapendwa wao ahakikishe bima ya afya kwa kila mtanzania inapatikana haraka ili tusije kupoteza maisha kwa kukosa matibabu maana kiuhalisia ni ngumu kuwa na cash wakati wote.
Watu wanaoishi Maisha ya kubahatisha wanaakili ya Maisha.wanauwezo wakuona changamoto kwa uhalisia na hao ski waimba mapambio
 
Uzuri rais Magufuli kwa kujibu mapigo ya wapinzani alisema suala la bima ya afya lipo kwenye ilani ya Ccm
Hata kutupeleka peponi lingekuwa ni suala wanaloweza liandika kwa ilani wangeliandika....ni siasa tu hizi hakitofanyika kitu!
 
Sekta ya afya ina changamoto sana....hiyo bima sio jambo dogo.
Ila huyu mama apunguze mdomo..asikilize ushauri itamsaidia sana.
Tunawza kuamua kila lita moja ya mafuta ikatwe tsh 50 iende kwenye mfuko wa bima.

Makampuni makubwa aingie kwenye mfuko wa bima wataifa

Kila mtalii aketwe pasentage ingie kwnye mmfuko wa bima

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Bima ya afya kwa kila mtanzania lazima kuwa na source of income itakayolipa hizo hela za dawa na mishahara plus huduma zote za afya.

Nani atakubali kuongezewa bei let's say ya petroleum products au madini kodi iwe kubwa au matajiri wa bongo waongezewe kodi. Ngoja tuone
 
Kwani ilani ya Ccm ukurasa wa 133 unasemaje kuhusu bima ya afya?
 
Hiyo bima ya afya kwa kila mwananchi itakatwa kwenye chanzo kipi cha mapato, iwapo asilimia kubwa ya wananchi hawana kipato angalau elfu 10 kwa mwezi kuweza kuchangia, tofauti na wafanyakazi ambao hukatwa kwenye mishahara yao kila mwezi.
 
Sisi ni matajiri hivi via gharama vya matibabu tuvilipe tu upinzani unataka wapi sasa, Si upinzani tumeuzika?
 
Kwangu mimi huyu wa Waziri wa afya ndiye waziri wa hovyo zaidi.
Ni mpenda sifa na mkurupukaji.
Anafanya vitu kwa sifa na hana weledi wowote.
Huyu Waziri wa Afya ni chizi au ni limbukeni wa madaraka!!!
Huyu alitakiwa awe mke wa Jiwe naona tabia zao zinaendana vizuri!!!
 
Wana JF poleni na pilika pilika za sikukuu.

Kama kichwa cha uzi kinavyojitanabaisha niseme kuwa agizo la waziri wa afya sio zuri kwa mustakabari wa watanzania.

Watanzania wengi tunaishi maisha ya kubahatisha,wengi tunatafuta chakula. Habari ya matibabu huwa ni dharula ndio maana tukiugua au kupata mgonjwa huwa tupata tabu sana.

Kitendo cha waziri mwenye dhamana ya afya zetu kuagiza hospital ziwe zinatukaba tuwe tunalipa gharama ya matibabu kabla ya bahati mbaya ya kufariki haijatokea ni habari mbaya.

Chukulia mkulima wa kijijini ambae amegongwa nyoka na kukimbizwa hospital atapata wapi pesa za kulipia haraka ili atibiwe na asifariki? Mama wa kijijini ambae amepatwa malalaria ghafla ataweza kumudu haya aliyoagiza waziri wa afya?

Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu,hoja ya bima ya afya kwa kila mtanzania iliibuka na kuwa gumzo. Uzuri rais Magufuli kwa kujibu mapigo ya wapinzani alisema suala la bima ya afya lipo kwenye ilani ya Ccm. Na itakuwa bima ya afya kwa watanzania wote.

Waziri wa afya alitakiwa kwa nia njema ya watanzania maskini ambao anajua ndio huwa wanakwama kupata maiti za wapendwa wao ahakikishe bima ya afya kwa kila mtanzania inapatikana haraka ili tusije kupoteza maisha kwa kukosa matibabu maana kiuhalisia ni ngumu kuwa na cash wakati wote.
Msimung'unye maneno bima ya afya kwa wote iwe chini ya serikali sitaki msinihusishe mpaka mniambie michango ya hifadhi ya jamii imeishia wapi
 
Back
Top Bottom