Waziri wa afya mulika Kitengo cha figo Muhimbili

Dazzle 2

Senior Member
Oct 9, 2015
125
225
Mh Waziri wa afya pole na majukumu mazito ya kulitumikia taifa. Kwa heshima zote tunaomba umulike kitengo cha figo pale muhimbili maana wagonjwa tunateseka. Baadhi ya Madaktari wako wanafanya kazi kwa mazoea mno kiasi cha kutokujali uhai wa binadamu wanaofanya dialysis kila siku.

Kwanza baadhi ya madaktari wako hawana muda wa kutuhudumia. Mfano tunaingia kwenye mashine saa 1asb au 1:30 lakini Dr hufika kuanzia saa 4asb. Ikumbukwe sisi wagonjwa tunaingia kwenye mashine kwa masaa 4 tu na hapo katikati lolote linaweza kutokea lkn muda mwingi wanabaki wauguzi peke yao ambao hufanya kazi kubwa sana kutuhudumia.

Pili baadhi ya Dr wako wakija hawana muda wa kupitia wagonjwa na kujua maendeleo yao au dawa gani wanahitaji kuandikiwa na Dr bali wakifika mara nyingi wako busy na mambo yao mengine na inafikia hadi wagonjwa wanatoka bado Dr aliyeko zamu hajawaona wala kuwaandikia dawa.

Mh kilichonifanya hadi tukuandikie waraka huu ni mateso tunayopata sisi wagonjwa. Mara nyingi tunapomaliza matibabu inatulazimu kukaa nje kwa zaidi ya lisaa au hata mawili kusubiri waliotusindikiza wamfuatilie Dr kuwaandikia dawa.

Kibaya zaidi leo hii mh imefikia mahali Dr aliyekuwa zamu anawapa karatasi waliotusindikiza waje kwenye mashine tuliko kutuuliza aina ya dawa tunazohitaji badala ya Dr kufanya yeye hiyo kazi. Hii inatusababishia matatizo sisi kama wagonjwa maana hatumuoni Dr wa kutupitia kujua hali zetu.

Hali imezidi kuwa mbaya hasa katika kipindi hiki cha miezi miwili. Baadhi yetu tumejaribu kuongea lkn hakuna wa kutusikiliza. Tunaomba tena Mh mulika kitendo hiki hali ni mbaya na ikikupendeza fanya ziara uje uongee na wagonjwa moja kwa moja uone madudu ya kitengo hiki. Pole kwa kukusumbua lkn hatuna namna nyingine zaidi ya kuleta hali halisi ilivyo.
 

okonkwo jr

JF-Expert Member
Jun 14, 2015
2,423
2,000
Dah pole sana,naamini serikali yako ya awamu ya tano ni sikivu,na wamekusikia,Mungu awe pamoja nawe na akujalie upone.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom