Waziri wa Afya, hizi gharama za matibabu Tumbi Hospital zinatisha

Charliemic

JF-Expert Member
Feb 17, 2019
530
1,000
Waziri wa Afya niombe uimulike hii hospital iliyopo mkoa wa pwani! Gharama za huduma ni kubwa mnoo! Mfano ukaenda pale kutibiwa gharama ya kujiandikisha ili umwone daktari ni Tsh 5000/= halafu anayehudumia ni intern.

Gharama za kupima malaria (MRDT) ni tsh 6000. Hapo bado huduma nyingine, bado gharama za dawa. Kiujumla gharama za matibabu Tumbi ni kubwa mnoo! Ni ngumu kuzimudu! Halafu kwa wale wenye bima za afya wanatibiwa sehemu yao tofauti, wana daktari maalumu anayewahudumia

Hii ni hospital ya serikali nategemea ipo kwa ajili ya kutoa huduma na sio biashara! Hizi gharama ni kubwa kuliko hata hospital binafsi. Ukiuliza wanasema ni hospital ya rufaa. Kwa hiyo hata wale tunaoishi jirani tusiende kutibiwa pale.
 
COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,547
2,000
Naomba nikupe ushauri.
1. Jiunge na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF)
au
2. Jiunge na Mfuko wa bima ya afya ya jamii ulioboreshwa (iCHF)

Ukifanya hivyo utakuwa umeondokana na tabu zote hizo
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
10,472
2,000
Huu uzi wako hautapata wachangiaji wengi kwasbb hali ya maisha ya watanzania inatofautiana sana.

Kuna viongozi wa serikali na wale wenye kazi zao hawataungana na wewe. Kwasabb wao wana bima za afya

Kuna wenye hali za chini ambao hawaendi hata hosp wakiugua. Wao hutafuna majani na mizizi ya mimea tu. Hawa pia hawatakuelewa.

Kuna wale tabaka la kati, hawa wamegawanyika makundi 2. Wapo watakauoungana na wewe. Na wapo watakaokupinhi
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
47,263

Lazima utibiwe Tumbe mkuu?
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
47,263
2,000
Naomba nikupe ushauri.
1. Jiunge na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF)
au
2. Jiunge na Mfuko wa bima ya afya ya jamii ulioboreshwa (iCHF)

Ukifanya hivyo utakuwa umeondokana na tabu zote hizo
Ushauri mzuri sn
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
6,417
2,000
Nilishapeleka kipimo cha makohozi pale mhimbili kwa ajili ya ndugu yangu nikatozwa elfu themanini, sasa nikajiuliza hii hospitali ni ya serikali, wataalamu na vifaa ni serikali inalipa, inakuaje raia anatozwa elfu themanini kwa ajili ya kipimo? kuna mtu anaweza kuniambia hapa hiyo elfu themanini kwa ajili ya cytology ya sputum ni subsidized rate? na baadaye nikaambiwa hiyo sampuli haikufaa na pesa imeshalipwa........hii ndo njia sahihi ya serikali kushughulikia changamoto za kiafya kwa wananchi?
 
Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
1,097
2,000
Tusubili sera ya bima kwa wote ila mpaka kutimia tutaisoma namba sio kijani,nyekundu Wala zambarau na sio bavicha Wala UVccm
 
zithromax

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
2,108
2,000
Waziri wa Afya niombe uimulike hii hospital iliyopo mkoa wa pwani! Gharama za huduma ni kubwa mnoo! Mfano ukaenda pale kutibiwa gharama ya kujiandikisha ili umwone daktari ni Tsh 5000/= halafu anayehudumia ni intern.

Gharama za kupima malaria (MRDT) ni tsh 6000. Hapo bado huduma nyingine, bado gharama za dawa. Kiujumla gharama za matibabu Tumbi ni kubwa mnoo! Ni ngumu kuzimudu! Halafu kwa wale wenye bima za afya wanatibiwa sehemu yao tofauti, wana daktari maalumu anayewahudumia

Hii ni hospital ya serikali nategemea ipo kwa ajili ya kutoa huduma na sio biashara! Hizi gharama ni kubwa kuliko hata hospital binafsi. Ukiuliza wanasema ni hospital ya rufaa. Kwa hiyo hata wale tunaoishi jirani tusiende kutibiwa pale.
Hizo gharam ndo kubwa Kama hujiu matibabu ni gharama nenda private yaani mnataka mtobiwa kijamaa jamaa tu
 
COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,547
2,000
Huu uzi wako hautapata wachangiaji wengi kwasbb hali ya maisha ya watanzania inatofautiana sana.

Kuna viongozi wa serikali na wale wenye kazi zao hawataungana na wewe. Kwasabb wao wana bima za afya

Kuna wenye hali za chini ambao hawaendi hata hosp wakiugua. Wao hutafuna majani na mizizi ya mimea tu. Hawa pia hawatakuelewa.

Kuna wale tabaka la kati, hawa wamegawanyika makundi 2. Wapo watakauoungana na wewe. Na wapo watakaokupinhi
iCHF ni Tshs 50,000/= kwa mwaka na inachukua wanachama 6 kwenye Familia yako. Kuliko kuhangaika kumuomba waziri msaada, tafuta hiyo Elfu 50 nenda kakate bima ya CHF utibiwe wewe na wanafamilia yako mwaka mzima kwa elfu 50 tu.
 
Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
1,950
2,000
Yule mbunge anayepokea 12M halafu anataka pesa aongezewe ikiwa ni pamoja na posho sidhani kama atakuelewa kwa hoja yako hii..

Watanzania tumetofautiana sana tena mnooo kama alivyosema mchangiaji mmoja hapa kwa mfano watu wa kanda ya ziwa hawana desturi sana ya kwenda hospitali hivyo hayo hawayajui kabisa.
 
signale

Member
Sep 17, 2020
54
125
Kuna kitu watu hawajui, serikali ikishalipa mishahara ya watumishi kwenye hz hospital ndo basi, pesa zingine za uendeshaji hazipelekwi, kwahy ili huduma isife lazima wateja walipie hz gharama.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
85,537
2,000
Waziri wa Afya niombe uimulike hii hospital iliyopo mkoa wa pwani! Gharama za huduma ni kubwa mnoo! Mfano ukaenda pale kutibiwa gharama ya kujiandikisha ili umwone daktari ni Tsh 5000/= halafu anayehudumia ni intern.

Gharama za kupima malaria (MRDT) ni tsh 6000. Hapo bado huduma nyingine, bado gharama za dawa. Kiujumla gharama za matibabu Tumbi ni kubwa mnoo! Ni ngumu kuzimudu! Halafu kwa wale wenye bima za afya wanatibiwa sehemu yao tofauti, wana daktari maalumu anayewahudumia

Hii ni hospital ya serikali nategemea ipo kwa ajili ya kutoa huduma na sio biashara! Hizi gharama ni kubwa kuliko hata hospital binafsi. Ukiuliza wanasema ni hospital ya rufaa. Kwa hiyo hata wale tunaoishi jirani tusiende kutibiwa pale.
Tuendelee tu kujifukiza jamani
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom