Waziri wa afya Dkt. Gwajima hana legitimacy ya kubaki kwenye hiyo Wizara

howardlite

JF-Expert Member
Jul 16, 2016
234
368
Nafasi ya uwaziri, tena wa Afya ni eneo sensitive sana, tena kwa kipindi kama hiki ni more sensitive.

Kwa kipindi hiki cha mgawanyiko mkubwa wa mitazamo kuhusu chanjo kwenye taifa letu,sio hekima kama waziri,msomi na mtaalamu kuzungumzia mambo binafsi ya mtu mwingine.

Hivi work ethics za udaktari zinaruhusu kweli hiki?Kwanini usiwaachie wengine wajibizane lakini usiwe wewe?

Ona kelele zinazopigwa na wananchi kukuhusu,umepoteza sifa ambayo waziri wa afya anapaswa kuwa nazo,mbaya zaidi huchafuki peke ako,na mamlaka ya uteuzi unaipaka matope.

Mamlaka ya uteuzi kwa nafasi hii,kihekima,angalieni upya sio dhambi.

Hekima na busara ni vitu muhimu sana katika uongozi(Reference mfalme Sulemani).
 
Kwa kuwa nafasi ya waziri wa ulinzi bado ipo wazi, basi itampasa Mh. Rais wetu atumie fursa hii kufanya mabadiliko makubwa ktk baraza lake la mawaziri. Nafikiri ameshajionea mwenyewe wizara zilizoyumba na hata kumuingiza matatizoni kutokana na ushauri mbaya aliopewa.
 
Bora ummy mara elfu kumi huyu mama ni kifuniko fulu
Labda kwa kuwa Watanzania ni wasahaulifu tu ila Ummy alipwaya sana pia katika suala zima la Uviko.

Serikalini kuna kulindana sana. Huyu wanagwaya kumtoa, fursa ikitokea wanamchomoa hapo wakati hamuangalii. Kesho mtaanza kumkumbuka tena mkiwa mmesahau maujinga yake.
 
Hata ndumba zinahusika sana
 
Nafasi ya uwaziri,tena wa Afya ni eneo sensitive sana,tena kwa kipindi kama hiki ni more sensitive.
Kwa kipindi hiki cha mgawanyiko mkubwa wa mitazamo kuhusu chanjo kwenye taifa letu,sio hekima kama waziri,msomi na mtaalamu kuzungumzia mambo binafsi ya mtu mwingine.Hivi work ethics za udaktari zinaruhusu kweli hiki?...
Huna hoja. Ina maana kama rais akiingia kwenye mgogoro kama huu dhidi ya watu wa familia yake naye utamwambia aachie ngazi? Nyinyi mnaotumwa na huyo tapeli mnajipotezea heshima na muda.
 
Bora ummy mara elfu kumi huyu mama ni kifuniko fulu
Hakuna Waziri mbovu na aliyefanya Madudu mengi katika Wizara hiyo kama Ummy Mwalimu na ndiyo maana hata 85% ya Watu wa Kada ya Afya alivyohamishwa hapo so tu walifurahi bali walisheherekea pia.
 
Hakuna Waziri mbovu na aliyefanya Madudu mengi katika Wizara hiyo kama Ummy Mwalimu na ndiyo maana hata 85% ya Watu wa Kada ya Afya alivyohamishwa hapo so tu walifurahi bali walisheherekea pia.
Ummy pale hakua na taaluma ya udaktari ,lakini huyu docta ndo hewa hana ushawishi wala ethic yoyote
 
Back
Top Bottom