mtakachake
New Member
- Apr 16, 2021
- 1
- 0
Pamoja na yote naomba nikupe pole ya ujenzi wa Taifa.
Pili nipende kukupa hongera kwa kuaminiwa tena kuongoza Wizara hii nyeti ya Afya ambapo sisi ndio tunashikilia roho za binadamu baada ya Mungu hususani majeruhi wa barabarani waliokithiri kila kukicha.
Lakini licha ya yote kuna maeneo mengi hujayafikia bado au kuyagusa nina uhakika kuwa umewahi fika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na umeongea na uongozi mara kadhaa na kudanganywa mengi juu ya hii taasisi.
Kiukweli huwajui wafanyakazi wake wana hali gani, wana madukuduku gani mioyoni mwao. Milango yako iko mbali kuweza kufunguliwa tungeweza kukueleza hali halisi sisi wafanyakazi basi tunaomba uje uongee na wafanyakazi ujue yanawasibu nini kiasi cha kushusha morali ya kazi Hapa MOI.
Viongozi uliowaweka hapa wakali kama pilipili kuficha madhaifu yao katika utendaji basi uje utusikilize.
Ukishindwa kuja basi tutayasema humu bila kuchoka mpaka mama yetu Mh. Samia atasikia na. tunaimani atakusaidia kusikiliza.
Ni sisi wanyonge tuliochoka kuvumilia.
Mtaka Chake.