Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima anafanya kazi nzuri. Mnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake

field marshall1

JF-Expert Member
Sep 17, 2017
1,171
2,730
Binafsi sina chama cha siasa na sijawahi kuwa mshabiki wa chama chochote cha siasa katika maisha yangu yote.

Naomba niseme yafuatayo, kwanza sina chuki na kiongozi wowote wa aidha CCM au CHADEMA au chama chochote cha siasa.

Nimefuatilia ziara na ufanyaji kazi wa waziri wa Afya Dr. Dorothy Gwajima, ndiyo anakosea kwenye uongeaji wake hasa akichamba zaidi au akiongea sana kumsifu Magufuli sana kupita kiasi lakini huyu Waziri anaongea mambo yalio uozo kwenye serikali na anajaribu kufuatilia kila kitu na kuweka wazi.

Huyu mama anajitahidi mno na nina imani uchapaji wake wa kazi utaleta matunda mazuri kwenye wizara hii iliyoharibiwa vibaya na waziri aliyepita.

Ninapenda kumpongeza na kumwambia asikate tamaa, kuna uozo mwingi kwenye wizara ya Afya kwa kiasi kikubwa na kuna uzembe mkubwa, wizi mwingi wa madawa, fedha na miradi hewa inayoibiwa pesa kila siku.

Waziri Gwajima endeleza uzi huo huo, uzembe na wizi uondoe hapo wizarani.
 
Sasa sijui watu wanamuelewa au vip!?

Maana kila clip naona anajitahidi kuchamba tu tu.

Au siku hizi ukichamba wenzako na kuwadharau ndio imekua ufanyaji kazi mzuri!?

Sijaona akiibua madudu au kurudisha dawa zilizoibiwa na kuuzwa maduka ya watu binafsi.

Huyu mi namuona hayupo vizuri kichwani.
 
Sikujua kuwa Madaktari nao wanapenda masengenyo na Majungu. Maaana sasahivi hawafanyikazi zaidi ya kuwaza namna ya kumpaka matope Mwanamama Gwajima. Sisi watu weusi tuko na shida mahala hakika, kama lengo ni kuturudisha kwenye mstari shida iko wapi?
 
Dorothi Gwajima ni version ya kike ya Josefu ( Unknown 2021)
 
Tunajua anahaha kama si kujitahidi kufanya vizuri ili kumzidi Mwanamke mwenzake aliyekuwepo na kumuonyesha kuwa alikuwa hawezi lolote lile.
 
Anajitahidi kuwa katili kama aliyemteua, hana lolote ni kujionyesha kuwa ni mkali, ujinga tu! Kwani akiwa na sauti ya chini kazi haitafanyika? Limbukeni tu!
 
Kwani kabla ya kuteuliwa kuwa waziri alikuwa na cheo gani?

Huko alikotoka alifanya jitihada fani kuzuia haya madudu, kwa sababu naona sawa tu Magufuli kabla ya kuwa Rais alikuwa mbunge wa CCM na sikuona chochote alichofanya ila sasa hiv anawasema wenzake kila siku wakati na yeye pia amezalishwa kwenye hiyo mifumo.
 
Sikujua kuwa Madaktari nao wanapenda masengenyo na Majungu. Maaana sasahivi hawafanyikazi zaidi ya kuwaza namna ya kumpaka matope Mwanamama Gwajima. Sisi watu weusi tuko na shida mahala hakika, kama lengo ni kuturudisha kwenye mstari shida iko wapi?
Hao ni wale waliotumia elimu waliyopewa kujineemesha badala ya kuujenga msingi bora wa sekta ya afya ili wakizeeka wautuimie
 
Mbowe chama kimetoka kuwa na wabunge 100 mpaka Mbunge mmoja lakini bavichaaa wako kimyaaaa wako bize kumpinga Waziri Dr Dorothy Gwajima ili ufisadi wa dawa uendelee.
Hivi una tatizo ganimkuu?
Hapa anazungumziwa waziri wa afya na utendaji wake,mbowe anaingia vipi hapa na chadema?
Aisee,wahindi hua Wana msemo wao,(ane duniya Peru nagaro) kwa maana kweli dunia imekwisha,ndo hivi Sasa.
 
Tatizo ni pale anapoona kwamba ndani ya afya anajua a to z, kisa kwamba amewai DMO,RMO, MKURUGENZI WA TIBA, inasaidia nini, sawa anauzoefu na wizara, lakini hawezi jua yote,ndani ya wizara, ALAFU Iyo mph, yake asisumbue nayo ndani secta ya afya ni elim ndogo, so hakuna foka foka kwani ukikaa na mtumishi mkaelezana, wenda ukapata majibu mazuri kutoka kwake ,anafikili ukali ndo utawala,
 
Back
Top Bottom