Jumaaly
Member
- Sep 5, 2015
- 74
- 21
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto mh. Ummy Mwalimu leo ameendelea na ziara yake mkoani Geita ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea hospitali teule ya rufaa ya Mkoa wa Geita na kutazama wagonjwa pamoja na hali ya utoaji huduma katika hospitali hiyo.
Aidha Mh. Ummy pia ametembelea hospitali na kituo cha afya cha
Nyankumbu na kuwajulia hali wagonjwa na kuzungumzana baadhi ya watumishi wa afya ili kutambua kero mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo.
Katika ziara yake hiyo mkoani Geita mh. Ummy Mwalimu aliwataka watumishi wa kada za afya nchini kufanya kazi kwa kufata maadili na viapo vya taaluma zao ili kuhakikisha huduma ya Afya nchini inakuwa bora na ya kuridhisha.