Waziri wa Afya ajiuzulu baada kutokea vifo vya watoto

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,521
9,325
Waziri wa afya wa TunisiaAbdurrauf esh-Sherif amejiuzulu wadhifa wake baada ya kutokea vifo vya watoto 11 katika hospitali moja ya serikali mjini Tunus.

Waziri mkuu wa Tunisia Yusuf Esh Shahid alitoa taarifa baada ya kuitembelea hospitali ya Er Rabita ambapo ndipo vifo hivyo 11 vya watoto vilipotokea, alisema kwamba amepokea na kukubali kujiuzulu kwa waziri wa afya Sherif.

Katika taarifa ya kwanza iliyotolewa na wizara ya afya inasema vifo vya watoto hao vilisababishwa na ugonjwa wa maambukizi kwenye damu.

Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa nchi hio ilitoa taarifa kwamba inafuatilia kwa ukaribu kesi hiyo na kwamba ikifahamika kuna uzembe wowote ulifanyika, wahusika watachukuliwa hatua kali

TRT
 
Mhhh hapa kwetu wajiuzulu ili iweje kwani wapo kwa ajili ya hao wananchi au kwa ajili ya bosi wao???Wakimkosea bosi watajiuzulu na sio kuwakosea wananchi. Venezuela hapa shida sana
 
Kwa ajari ya mabasi tumenunua kamera na kwenye mahospitarini wapo wauguzi na sehemu zoote Zina watu wake Mimi wa na mawaziri was sehemu hizo wanahusika vipi

Cc mawaziri tunachoangalia ni posho na kusubiri Cha juu kinachobaki baada ya shughuli yenye pesa kutanyika bana
 
Back
Top Bottom