Waziri wa Afya aeleza viwanda vya dawa zitakavyookoa mamilioni ya fedha kwenda nje

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
500
1550914391952.png


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kukagua Maendeleo ya ujenzi wa viwanda vya Dawa vya Vista Pharma Ltd na Kairuki Pharmaceutical Ltd vinavyoendelea kujengwa kwa kasi katika Mkoa wa Pwani.

Katika ziara hiyo Waziri Ummy alilenga kujionea na kutatua Changamoto zinazowakumba Wawekezaji nchini hususani katika Viwanda vya Dawa ili kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kinachoendelea kupotea kutokana na kuagiza Dawa nje ya nchi.

"Katika kila Shilingi 100 ambayo Serikali inatumia kununua Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba, Shilingi 94 tunaipeleka nje ya nchi kununua Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba, na ndiomaana nimefanya ziara hii pamoja na viongozi wa Mkoa na kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na Kituo cha uwekezaji ili kuokoa fedha hiyo inayopotea nje ya nchi" alisema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewaagiza Tanesco ndani ya Mkoa kuhakikisha wanaleta huduma ya umeme ndani ya wiki moja ili hatua za mwanzo za ufungaji wa mashine katika Viwanda hivyo uanze Mara moja. Pia, Waziri Ummy amewaagiza Mamlaka ya Maji Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanaleta huduma ya maji ndani ya Machi 15 katika eneo hilo la Viwanda ili kuharakisha shughuli za ujenzi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom