Waziri wa afya aagiza kuboreshwa kwa takwimu Rukwa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,597
2,000
Waziri wa afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu, ameiagiza timu ya uendeshaji wa huduma za afya ya mkoa wa Rukwa, kusimamia utendaji wa vituo vyote vya kutolea huduma ya afya ili kudhibiti takwimu zisizokuwa sahihi, ambazo zinasababisha bajeti ya dawa isiwe halisi na kuendelea kuwepo upungufu mkubwa wa dawa.

Waziri huyo Ummy Mwalimu akiongea kwenye kituo cha afya cha Matai wilayani Kalambo, ameshangazwa kuona menejimenti ya kituo hicho cha afya ambacho hivi sasa kinatumika kama hospitali ya wilaya hiyo, inakuwa haijui kwa uhalisi bajeti ya dawa, na huku wakiendelea kupata bajeti ya kiwango cha kata kwa idadi ya watu elfu tatu, wakati sasa matai ni makao makuu ya wilaya na idadi ya watu ni zaidi ya 10,000 jambo ambalo haliendani na upatikanaji wa dawa.

Nao baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo akiwemo katibu tawala Bw. Frank Sichalwe, wamemueleza waziri huyo wa afya kuhusu utendaji wa bohari kuu ya dawa MSD kanda ya Mbeya, kuwa mara nyingi wamekuwa wakileta dawa nyingi ambazo tayari zinakaribia kuisha muda wa matumizi, na kwamba wilaya inakabiliwa na tatizo kubwa la kutokuwa na gari la wagonjwa kabisa.

Chanzo: ITV
 
Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,288

Wilaya ya Kalambo ina miaka kadhaa sasa. Huduma nyingi za kijamii ni hovyo. Kuna wakati nilifika huo mji wa Matai,duu,nguruwe wanazurura mitaani kama mbuzi. Barabara za mitaa hazieleweki,Hakuna grader la kurekebisha hizo barabara. Ukiangalia kwa undani,Idara nyingi zinaongozwa na wasomi wa low grade au waliotimuliwa maeneo mengine kwa kuharibu. Kipindi napita hapo kwa shughuli binafsi,ilidaiwa akiingia msomi,anapigwa juju ili asijepokonya vyeo! Sishangai kuwa,hospitali ya Wilaya ina hadhi ya kama ya Kata.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom