Waziri: Uwezekaji wa Barrick una manufaa kwa taifa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
08 October 2012 | Mwananchi

SERIKALI imeipongeza Kampuni ya African Barrick Gold (ABG) kwa kuleta manufaa makubwa kwa taifa kutokana na uwekezaji unaoendelea kufanywa na migodi yake nchini katika nyanja mbalimbali ukiwamo uchumi wa nchi na maendeleo ya jamii.

Kampuni ya ABG inamiliki migodi minne ya dhahabu nchini -- Bulyanhulu, North Mara, Buzwagi na Tulawaka -- na ndiyo kampuni kubwa kuliko zote kwenye sekta ya madini.

"Nimejifunza mambo mengi sana baada ya kutembelea mgodi wa North Mara," alisema Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, baada ya kufanya ziara ya mgodi huo wa ABG ulioko Wilaya ya Tarime, mkoani wa Mara.

Katika ziara hiyo, Masele pamoja na Naibu Waziri wa Nchi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Charles Kitwanga, walitembelea miradi mikubwa ya jamii ambayo inatekelezwa na mgodi huo kwenye sekta mbalimbali ikiwamo elimu, maji na afya.

Masele alisema kuwa mgodi wa North Mara kihistoria umekuwa na matatizo ya uhusiano na jamii inayoizunguka, lakini hatua kubwa zimepigwa sasa kuboresha uhusiano na vijiji vinavyozunguka mgodi huo.

"Mimi binafsi, bungeni nimesikia pale wabunge wa huku wakilalamika kwamba kuna shule za msingi ziko jirani sana na mgodi. Kazi za mgodi zinapoendelea, ile milipuko inakuwa ikiwaathiri wanafunzi," alisema.

"Lakini leo nimetembelea shule ambayo inatakiwa kujengwa ili kuhamisha ile ambayo inaathiriwa na shughuli za mgodi. Nimejionea kazi ambayo inaendelea pale. Wakandarasi wako saiti wanajenga hizo shule."

Masele alisema kuwa kipindi cha nyuma kulikuwa na tatizo la wanafunzi kukaa chini katika shule zilizopo katika maeneo hayo ya mgodi, lakini mgodi wa North Mara sasa unatekeleza mradi kabambe wa kuzipatia shule hizo madawati.

"Nimejionea kwamba mgodi umeweza kutekeleza ahadi ya kuweka madawati katika shule zote ambazo zinazunguka mgodi na wanafunzi wamekaa kwenye madawati," alisema.

Hivi karibuni, mgodi wa North Mara ulitoa msaada wa zaidi ya madawati 1,000 kwa Shule za Msingi za Wilaya ya Tarime ambazo zinazunguka mgodi huo.
 
...Kishapewa shares huyu kule Barrick sasa anaanza kubwabwaja kwa kuwapigia debe hawa wachukuaji. Yaani kununua madawati ndio kuleta manufaa kwa Watanzania!? Mbona hajatia neno kuhusu royalties wanayolipa ya 4% ukilinganisha na nchi kama Botswana ambayo wanagawana na wawekezaji nusu kwa nusu!?

Nilidhani baada ya kuondolewa kwa Ngeleja tutaona mabadiliko makubwa pale Nishati na Madini katika kuhakikisha rasilimali za Taifa zinakuwa na maslahi kwa Watanzania lakini madudu bado yanaendelea tu!!!!
 
Damn.. I knew it..! Ile jezi aliopewa Presidaa inahucika na tamko hili.. Duuuh..
 
ridhiwan ana tenda ya kusomba mchanga (na malori yake) wenye madini kwenda kuchujwa nje ya nchi,mzindakaya na mkapa wana tnda ya kulisha nyama buzwagi,ole naiko sijui ni mkurugenzi,dalali ana hisa nao..nyambaf
 
Labda una manufaa kwake na kwa mke wake! Huyu n/waziri masele hafai hata kuwa katibu kata.
 
Nayakumbuka maneno ya Mkono kila kiongozi wa serikali anayeingia kwenye mgodi akitoka anabadilikasijui wanapewa nini sishangai kwani sio tamko la kwanza kutolewa na viongozi walioenda kutembelea migodi ya Barick
 
Ata na hayo madawatit haya manamba ni full uwongo. Sidhani kwamba barrick wanania nzuri. Wanaangalia vya kwao tu. Juzi peru wameshindwa kesi.
 
ridhiwan ana tenda ya kusomba mchanga (na malori yake) wenye madini kwenda kuchujwa nje ya nchi,mzindakaya na mkapa wana tnda ya kulisha nyama buzwagi,ole naiko sijui ni mkurugenzi,dalali ana hisa nao..nyambaf

Evidence?
 
...Hawa jamaa kwa kweli ni wapumbavu sana. Hawa jamaa wanavuna $ in billions halafu wakinunua madawati 2,000 eti wanaonekana wameliletea Taifa letu manufaa makubwa sana!!!

Inashangaza sana kusema kweli...Wengi tulifurahia kuondolewa kwa Ngelejea pale Madini na nishati lakini kuna kila dalili tumeruka mikojo na kukanyaga kinyesi tena cha mtu mzima...Yule Muhongo naye ameshaanza kutoa kauli ambazo zinapingana kuhusu rasilimali za Taifa...labda kweli Watanzania tuna laana ya Mungu maana hawa wanajua fika sababu mbali mbali zilizofanya Ngeleja ang'olewe pale Madini na Nishati, halafu na wao baada ya muda mfupi toka waingie pale madini na Nishati kuanza kurudia mistari ile ile kama ya Ngeleja inatia kichefuchefu sana.

Labda una manufaa kwake na kwa mke wake! Huyu n/waziri masele hafai hata kuwa katibu kata.
 
Tatizo ni kuwa sisi wenye mali hatuuzi kwao wanatupa zawadi kidogo. Kwann tusimiliki tukawauzia wao
 
...Kishapewa shares huyu kule Barrick sasa anaanza kubwabwaja kwa kuwapigia debe hawa wachukuaji. Yaani kununua madawati ndio kuleta manufaa kwa Watanzania!? Mbona hajatia neno kuhusu royalties wanayolipa ya 4% ukilinganisha na nchi kama Botswana ambayo wanagawana na wawekezaji nusu kwa nusu!?

Nilidhani baada ya kuondolewa kwa Ngeleja tutaona mabadiliko makubwa pale Nishati na Madini katika kuhakikisha rasilimali za Taifa zinakuwa na maslahi kwa Watanzania lakini madudu bado yanaendelea tu!!!!

Kwa Tanzania hakutakuwepo mabadiliko yeyote mpaka tumbadilishe yule jamaa aliye juu ya tiketi. Hata wabadilishe mawaziri kiasi gani the problem is the headmaster.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ni kweli Mkuu Jasusi na si kumtoa yule tu bali pia kuhakikisha haingii mwingine kutoka magamba...Huyo fisadi EL anayepigiwa debe hapa kila kukicha na wafuasi wake naye ndio kama wale wale waliopita au huyu aliyekuwepo, hatakuwa na jipya lolote la kuhakikisha Tanzania inapata maendeleo makubwa kutokana na utajiri kubwa wa rasilimali za Taifa.

Kwa Tanzania hakutakuwepo mabadiliko yeyote mpaka tumbadilishe yule jamaa aliye juu ya tiketi. Hata wabadilishe mawaziri kiasi gani the problem is the headmaster.
 
Last edited by a moderator:
Masele apeleke ujuha wake huko huko katika familia yake mwenyewe. Anafikiri ataweza kumdanganya nani mwenye akili yake timamu kwamba barrick wamechangia maendeleo ya nchi hii.
Hao waporaji kama wamemkabidhi jiwe la dhahabu aishie zake huko akamueleze huo ujinga aliyemteua.
 
Huwezi ku appriciate mchango wao kwa kusoma uzushi wa magazeti ya bongo. Ukienda ukaona na kusona taarifa za kweli ndo utajua. Watanzania ni watu wa kulalamika tu. Mnawaona wawekezaji ni wezi bila kuangalia fedha wanazotunia kuiweka hizo investment.

Je unajua operating costs za mgodi?
Je unajua ni kiasi gani kinazalishwa kwa mwezi?
Je unajua wanalipa mrabaha wa tsh ngapi?
Kama hujui bora usichangie.
Usiku mwema
 
Mkuu BAK, jibu la huu ujinga utalipata kwenye article ya Jenerali Ulimwengu, upo uzi wake leo kuhusu vijana wa CCM wanaogombea na kuupata uongozi.
 
Barrick ni kampuni ya kutokea Canada na mheshimiwa rais alikua Canada so akili kumukichwa ndugu mtoa mada
 
Huwezi ku appriciate mchango wao kwa kusoma uzushi wa magazeti ya bongo. Ukienda ukaona na kusona taarifa za kweli ndo utajua. Watanzania ni watu wa kulalamika tu. Mnawaona wawekezaji ni wezi bila kuangalia fedha wanazotunia kuiweka hizo investment.

Je unajua operating costs za mgodi?
Je unajua ni kiasi gani kinazalishwa kwa mwezi?
Je unajua wanalipa mrabaha wa tsh ngapi?
Kama hujui bora usichangie.
Usiku mwema
Aisee wacha kupumbaza watu na maswali yako. Je inapokamatwa helicopter inatorosha madini ni vipi? halafu ushahidi unapotelezewa? Michanga inayobebwa kwenye makantena je? Au yote ni uwongo?
 
Back
Top Bottom