Waziri Ummy, Usipotoshwe maamuzi yako kuhusu ADDO na wafamasia mtawaumiza Watanzania

Hiii ligi ya Pharmacy Vs MD +Nursing huwa haiishi ....!! Wafamasia huwa hawataki kukubali kuwa MD yupo juu ya yote, mtu mwenye Bachelor ya Medicine doctor kwenye masters anaweza chepukia course karbia zote za Pharmacy, Ila mtu mwenye Bachelor of Pharmacy yupo limited Sana kuchepukia course za MD
Mwamba ngoma huvutia kwake.

Mwambie MD atengeneze dawa km ataweza.
 
Ooooh!
Huyu ni dokta na Profesa, kweli?

Nchi yetu hii imepoptea kweli kweli.
Hajui Famasia kazi yake ni nini, na wala hajui kwamba kuna sheria kabisa inayotambua kazi ya Famasia duniani kote?

Andiko lote toka mwanzo halionyeshi kuwa huyu ni mtaalam kama inavyoonyesha katika utambulisho wake, MD, Ph.D. n.k.
Ni kama andiko la mtu ambaye kamaliza kidato cha nne? Leo hii anatafuta kujitambulisha kwa waziri naye awe mshauri wa waziri?

Dr Koboko, kama wewe kweli ni daktari, udaktari wako ni wa shaka sana, na huo uProfesa unaojitangaza nao sijui umeupata wapi kama hata hujui kazi za mtaalam ambaye unapaswa kushirikiana naye wakati wa kumhudumia mgonjwa. Kama umesomea Muhimbili, kuna chuo cha maFamaciia hapo hapo na wote mpo chuoni hapo, utashindwa hata kudadisi na kujua famaciia anasoma nini?

Unasema "administration of drugs" hiyo ni kazi ya daktari? Na huko kumpa mgonjwa dawa, ina maana wagonjwa wote wapo hospitalini wamelazwa wakisubiri kupewa dawa wakiwa mahtuti?

Hujui sehemu nyingine nyingi ambako dawa nyingi zaidi hutolewa bila uwepo wa nesi wala daktari?

Hata historia ya hizi taaluma huijui ilikotokea?
Unaonekana kuwamburura kuliko unayemponda.
 
Bora wameifuta hiyo ADDO maana haingii akilini eti MD haruhusiw kuuza dawa mpaka awe na cheti cha ADDO wakat pharmacology yote ipo kichwan,tena mbaya Zaid unakuta Baadhi ya watu wanaopewa hiyo ADDO wengine ni form 4 failures.
Mkuu, siyo swala la "pharmacology yote yote kuwa kichwani"; pamoja na kwamba hilo siyo kweli, lakini kuna sababu muhimu zaidi inayozuia hilo. Conflict of Interest, pande zote mbili.

Mfamacia asianze kutoa dawa tu hata kama anajua tatizo la mgonjwa, na hivyo hivyo, daktari naye atakuwa na conflict of interest kama atakuwa ni yeye yule yule anayeshughulika na sehemu zote mbili, kuona mgonjwa na kutoa/kumiliki dawa.
 
Ooooh!
Huyu ni dokta na Profesa, kweli?

Nchi yetu hii imepoptea kweli kweli.
Hajui Famasia kazi yake ni nini, na wala hajui kwamba kuna sheria kabisa inayotambua kazi ya Famasia duniani kote?

Andiko lote toka mwanzo halionyeshi kuwa huyu ni mtaalam kama inavyoonyesha katika utambulisho wake, MD, Ph.D. n.k.
Ni kama andiko la mtu ambaye kamaliza kidato cha nne? Leo hii anatafuta kujitambulisha kwa waziri naye awe mshauri wa waziri?

Dr Koboko, kama wewe kweli ni daktari, udaktari wako ni wa shaka sana, na huo uProfesa unaojitangaza nao sijui umeupata wapi kama hata hujui kazi za mtaalam ambaye unapaswa kushirikiana naye wakati wa kumhudumia mgonjwa. Kama umesomea Muhimbili, kuna chuo cha maFamaciia hapo hapo na wote mpo chuoni hapo, utashindwa hata kudadisi na kujua famaciia anasoma nini?

Unasema "administration of drugs" hiyo ni kazi ya daktari? Na huko kumpa mgonjwa dawa, ina maana wagonjwa wote wapo hospitalini wamelazwa wakisubiri kupewa dawa wakiwa mahtuti?

Hujui sehemu nyingine nyingi ambako dawa nyingi zaidi hutolewa bila uwepo wa nesi wala daktari?

Hata historia ya hizi taaluma huijui ilikotokea?
Umejikita kumkosoa prof bila kupiga hoja zake

Mi sio mtu wa afya ila nilitaman kupata ukweli kuhusu machache ambayo prof ameaninisha
1. Mfamasia hasomei kuhusu magonjwa chanzo na dalili zake je ni kweli? Na kama kweli

Basi mfamasia hawezi kuwa mtu sahihi hapo

Maana ni ukweli nurse anasomea hayo na dr wake

Hoja hii binafs nahitaji majibu yake
Asante mtaalamu
 
Wazo potofu kabisa ambalo linaonyesha huna ufahamu na haya mambo.

Matibabu ya mgonjwa yeyote ni 'teamwork' hakuna aliye na uwezo juu ya mwingine katika timu hiyo. Kila mtu ana majukumu yake yanayofahamika vizuri kabisa.
Hiyo kasumba ya Daktari kuwa juu ya wengine ilishapitwa na wakati zamani sana.
Kwenye chumba cha upasuaji unahusika na nini?
 
Hiii ligi ya Pharmacy Vs MD +Nursing huwa haiishi ....!! Wafamasia huwa hawataki kukubali kuwa MD yupo juu ya yote, mtu mwenye Bachelor ya Medicine doctor kwenye masters anaweza chepukia course karbia zote za Pharmacy, Ila mtu mwenye Bachelor of Pharmacy yupo limited Sana kuchepukia course za MD
Upo sahihi
 
Umejikita kumkosoa prof bila kupiga hoja zake

Mi sio mtu wa afya ila nilitaman kupata ukweli kuhusu machache ambayo prof ameaninisha
1. Mfamasia hasomei kuhusu magonjwa chanzo na dalili zake je ni kweli? Na kama kweli

Basi mfamasia hawezi kuwa mtu sahihi hapo

Maana ni ukweli nurse anasomea hayo na dr wake

Hoja hii binafs nahitaji majibu yake
Asante mtaalamu
Mfamasia kazi yake siyo kutambua magonjwa, kazi yake ni dawa, sehemu zote zinazohusu dawa. Sijui kama kuna sehemu yoyote Tanzania Famacia anapolilia kuwa mtaalam wa magonjwa. Hiyo ni kazi ya wengine. Mfamasia anasomea dawa jinsi inavyofanya kazi mwilini mwa binaadam, magonjwa inayotibu, utengenezaji wa dawa hiyo, utunzaji wa dawa kufuatana na mazingira ya dawa yenyewe,kama ni kuwa kwenye ubaridi ili isiharibike au vinginevyo, n.k., n.k..

Lakini hata hivyo, kumbuka, katika kumtibu mgonjwa, kazi hiyo siyo ya mtu mmoja, ingawaje imekuwa ikifahamika hivyo tokea zamani kimakosa.

Mgonjwa anahudumiwa na timu, jopo la watu mbalimbali. siyo kazi ya daktari pekee. Hii ndiyo maana inatakiwa pawepo na ushirikiano katika utendaji wa kazi wa watu hawa.

Unaposema "Maana ni ukweli nurse anasomea hayo na dr wake" una maana gani? Nurse anasomea kazi yake, na anafanya kazi yake, hafanyi kazi ya daktari. Daktari hana nurse wake. Hawa ni watu wawili tofauti, kila mmoja anayo kazi yake na wanategemeana.
 
Kwenye chumba cha upasuaji unahusika na nini?
Kwani huko yupo daktari peke yake?
Na unajua kuna dawa ngapi zinazotumika huko kiasi cha kulazimu kila mtu awepo huko? Mazingira yenyewe ya sehemu hiyo yanalazimisha pasiwepo na utitiri wa watu hata kama ingetakiwa kuwe na kila mtaalam husika na kila jambo.

Kwa maana ya swali lako, una maana ni madaktari wote wanakuwepo kwenye vyumba vya upasuaji?
 
Wadaktri njaa wanataka kuhodhi kila kitu wao..hadi kazi yao ya msingi ya kutibu wagonjwa wameiacha..sasa wanakimbilia vyeo na pesa.

Kila kwenye pesa wanataka waingie wapige..

Nawaonya madaktari fanyeni kazi zenu za msingi..sio kuingilia kila seheme..

Ndio mana sekta ya afya nchini haisongi..ikedumazwa na madaktari wachumia tumbo.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazo potofu kabisa ambalo linaonyesha huna ufahamu na haya mambo.

Matibabu ya mgonjwa yeyote ni 'teamwork' hakuna aliye na uwezo juu ya mwingine katika timu hiyo. Kila mtu ana majukumu yake yanayofahamika vizuri kabisa.
Hiyo kasumba ya Daktari kuwa juu ya wengine ilishapitwa na wakati zamani sana.
Labda we ndo umepitwa na wakat
 
Wadaktri njaa wanataka kuhodhi kila kitu wao..hadi kazi yao ya msingi ya kutibu wagonjwa wameiacha..sasa wanakimbilia vyeo na pesa.

Kila kwenye pesa wanataka waingie wapige..

Nawaonya madaktari fanyeni kazi zenu za msingi..sio kuingilia kila seheme..

Ndio mana sekta ya afya nchini haisongi..ikedumazwa na madaktari wachumia tumbo.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa alichoandika ni kweli, anayetoa dawa kwa mgonjwa ni Nurse au Dr na sivinginevyo may be tupate uzoefu kwa nchi zilizoendelea kama Kenya
 
WAZIRI UMMY MWALIMU, USIPOTOSHWE NA WAFAMASIA KUHUSU ADDO, MTAANGAMIZA AFYA ZA WATANZANIA.

Na Prof Patrick Koboko(MD,MMED,PhD)

Salaam Mhe Waziri!

Kwanza kabisa nikupe pole na hongera nyingi sana kwa majukumu iliyonayo ya ujenzi wa taifa hususani dhamana kubwa uliyopewa ya kushikilia afya za watanzania. Maana wewe ukitetereka na afya za watanzania zinatetereka.

Mhe Waziri Ummy Mwalimu umekua ni miongoni mwa wanasiasa wanamama wanaofanya kazi kubwa sana na nzuri sana katika kulijenga taifa hili na hii ndiyo maana ulirejeshwa katika katika wizara iliyopo hivi sasa.
Lakini nikushauri Mama yangu kuna watu wanekuzunguka usipokua makini watakuharibia kazi, wanatumia mwanya kwa sababu wewe siyo Mtaaluma katika fani ya Afya. Katika hili swala la ADDO umepotoshwa na msipoangalia mnaenda kuliangamiza taifa, titatolea sababu hapa chini.

ADDO NI MRADI WA NANI?
Mhe waziri, tunashukuru kwamba mmesitisha mpango wa kutoa mafunzo kwa watoa dawa za binadamu ambao hawana taaluma ya famasia almaarufu kama ADDO. Huu ulikua ni mradi ambao ulibuniwa na baadhi ya wachumia tumbo wachache ambao walitaka kujitengenezea namna flani ya kula pesa za watanzania wenye taaluma za afya hasa wauguzi na matabibu kwa madai kwamba hawana taaluma za famasia(Sijui kuna uhusiano gani hapa). Huu ulikua ni upigaji wa pesa za watanzania tena walitoza pesa nyingi sana kuanzia shilingi 250,000 na kuendelea. Kuondoa ADDO ni kuwandolea ulaji wachumia tumbo hawa ambao hawakua na maslahi kwa taifa. Maana vyeti vilitolewa kwa rushwa nyingi sana na hata walipewa wasiokua na taaluma za afya ndiyo maana tuliona yanayotokea kwenye baadhi ya maduka, mtu ana cheti cha ADDO lakini taaluma ya Afya hana. Niwe muwazi mradi huu uliratibiwa na baraza la famasia Tanzania, hata leo ukaguzi ukifanyika yatagundulika Madudu mengi sana na ningeomba mamlaka za serikali kama vile PCCB na CAG walichunguze baraza la famasia Tanzania mtajionea mengi.

KATI YA MFAMASIA, NESI NA DAKTARI NANI ATOE DAWA KWA MGONJWA? WAZIRI UMEPOTOSHWA!

1.MFAMASIA KAZI YAKE NI IPI?
Kwa bahati mbaya sana Mhe waziri sijui lengo lako la kusitisha mafunzo ya ADDO ni kudhibiti mianya ya Rushwa au mnalenga kazi hii ifanywe na wafamasia pekee? Kama lengo ni wafamasia watoe dawa kwa wagonjwa basi umepotoshwa vibaya sana mnataka kuangamiza Afya za wananchi.
✓Kazi ya Mfamasia ni kutunza na kuhifadhi dawa,kusambaza maeneo yenye uhitaji pamoja na kutengeneza dawa viwandani na siyo kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa . Kwahiyo kazi yake siyo drugs Administration, hii ni kazi ya watu wengine. Mfamasia hajasomea Magonjwa wala wadudu wanaosababisha maradhi, hajasomea dalili za magonjwa.Hivi anapoenda mgonjwa kwenye duka la dawa na hana cheti cha daktari, Mfamasia anajua Diagnosis ya ugonjwa wake? Amesomea dalili? Ni maduka mangapi yanayotoa dawa kwa vyeti vya madaktari nchini? Hivi mnajua kua mnataka kuliangamiza taifa kwa maslahi ya wachache?

2.DAKTARI NA NESI KWENYE UTOAJI WA DAWA.

Sihitaji kutoa utetezi katika taaluma hizi kwa sababu mimi ni mwanataaluma pia lakini huu ndio ukweli na Mhe waziri nitoe somo hapa ili ukatae wale waliokupotosha.

✓ Daktari yeye amesomea magonjwa na dalili zake hivyo, mgonjwa anapoumwa tayari anajua anaumwa kitu gani na anajua ampe dawa gani maana dalili za ugonjwa husika anazijua, sasa unaposema Mfamasia akae dukani auze dawa, akija mgonjwa bila cheti atanisaidia nini? Atatambuaje ugonjwa husika na kwa taaluma gani?

✓Nesi hana tofauti sana na daktari maana naye anasomea magonjwa na dalili zake pamoja kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa na yeye amejikita zaidi katika kumwangalia mgonjwa anapopata matibu. Kiutaratibu Nesi ndiye anayeenda na cheti cha daktari katika dirisha la dawa na atapewa dawa na Mfamasia kisha ataenda kumpa mgonjwa dawa maana anajua anatoa dawa ipi kwa mgonjwa na kwa ugonjwa upi. Ndiye anayepokea maagizo ya daktari kisha aende kwa mhifadhi dawa ambaye ni Mfamasia ampatie ili akampe mgonjwa.

Halafu kuna kikundi cha watu wachache wanaanzisha miradi wakaupa jina la ADDO ili manesi na madaktari wasomee kisha wakauze dawa.Mbona mahospitalini manesi na madaktari wanatoa dawa hawasomi ADDO? Utapeli mtupu!

USHAURI: NINI KIFANYIKE KATIKA UTOAJI WA DAWA NCHINI KWENE MADUKA YA DAWA?

1.KWENYE PHARMACY ZA JUMLA NA REJA REJA.
(i)Kwakua maduka haya ni makubwa na yana dawa nyingi, pawepo na Wafamasia ambao kazi zao ni kuhifadhi na kusambaza dawa kwenda kwa wauzaji au watoa dawa na siyo wao kuuza dawa kwa wagonjwa moja kwa moja maana wao hawana taaluma ya magonjwa.

(ii) Kuwepo na nesi au tabibu kwa ajili ya kutoa dawa kwa wagonjwa walioandikiwa kwenye vyeti au wawasikilize na kisha kubaini wanaumwa nini na kisha watoe dawa. Hizi ndizo kazi zao hasa kwenye maduka ya rejareja. Mfamasia hana utaalam wa kubaini ugonjwa, anaweza kuleta matatizo kwa mgonjwa.

(iii) Dawa zisitolewe bila cheti cha daktari katika duka lolote na ukaguzi wa kila mara ufanyike. Maana anaweza kutoa dawa mtu ambaye hana taaluma ya magonjwa ikiwa mgonjwa hana cheti na kuleta madhara makubwa.

2.MADUKA YA DAWA MUHIMU
Kwakua maduka haya mengi yapo sehemu ambazo ziko mbali na huduma za afya, wataalam wenye taaluma za kubaini mgonjwa anaumwa nini kupitia dalili waachwe wauze au watoe dawa. Hawa ndio waliosomea Magonjwa,dalili pamoja na kutibu. Hapa anaweza kukaa daktari au nesi akauza dawa. Kumwambia Mfamasia akae dukani auze dawa wakati hajasomea dalili wala kubaini magonjwa ni kutaka kuleta madhara makubwa kwa wagonjwa.
Kwakua maduka haya hayana dawa nyingi, uhifadhi unaweza kufanywa na daktari au nesi mwenye stoo maana pia wamefundishwa kipengele hicho.

HITIMISHO.
Nishsuri tuwe na chombo cha ukaguzi wa maduka ya dawa ambacho kitahusisha wanataaluma wa Famasia,Udaktari na Uuguzi ili ifanye kazi ya kusimamia maduka ya madawa na isifanywe na Barazaa Famasia wala TMDA. Hatutaanza sisi, mataifa ya wenzetu wanafanya hivi na wamefanikiwa sana wala hawana migogoro kama hii ya kwetu. Baraza la Famasia libakie kazi yake kudhibiti taaluma na siyo kukagua maduka ya dawa.TMDA wanamajukumu makubwa wabakie kukagua dawa zinazoingia nchini na vifaa tiba na kukakua ubora wa madawa viwandani huko zinakotengezwa, kwenye maduka ya dawa kiundwe chombo maalumu kijitegemee

Prof Patrick Koboko(MD,MMED, PhD in Human anatomy)
Nimjuavyo Waziri Ummy...usikute kishakasirika kupewa ushauri huu uliokwenda shule.
 
Hakuna university Teaching hospital nchini ndiyo tatizo kubwa kwetu hapa.Wabunge hawana ulewa nini maana ya hospital ya mloganzila kujengwa?

Tujenge university Teaching hospital nchini , Tutapata wanataaluma wa uhakika siyo kama ilivyo sasa. Maprofesa wote hawafundishi tena mawodini baada ya kuishusha hazi hospital ya mloganzila.

Chonde waziri iweke hospital mloganzila under Muhas tusikilize masomo kutoka Teaching univesities duniani.
 
👍
 
Back
Top Bottom