Waziri Ummy: Serikali haitoi taarifa za COVID-19 kutokana na zoezi la uhakiki wa maabara ya Taifa

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,666
22,674

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema sababu ya kutotangaza mwenendo wa ugonjwa wa Corona ni kutokana na maboresho yanayofanyika kwenye Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, ambapo kuna marekebisho yanafanyika na ndani ya siku chache marekebisho yatakamilika na watatoa taarifa

Waziri Ummy ameeleza hayo leo wakati akizindua mfumo wa mawasiliano wa huduma kwa wateja katika Wizara hiyo ambapo amesema itasaidia wananchi kupata taarifa sahihi kwa haraka zaidi.

Aidha Waziri Ummy amesisitiza kuwa vifo vinavyotokana na Corona vipo na kesi za maambukizi zipo, hivyo wananchi wanatakiwa waendelee kuchukua tahadhari ili kuepuka kuambukizwa huku akiwataka kufuata taarifa sahihi na kuacha kujawa na hofu.
 
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema serikali haijatoa taarifa za mwenendo wa ugonjwa wa Covid-19 nchini kwa wiki moja sasa kutokana na uwepo wa zoezi la uhakiki wa maabara ya taifa na uhakiki huo utakapokamilika, taarifa zitaendelea kutolewa.

AzamTV
Kwa hiyo wanaficha vifo vya korona na kusema ni vya homa na matatizo ya kupumua, au siyo?
 
Katikati ya vita, unamsimamisha kazi kamanda mkuu wa jeshi - unamwambia akae chini na mwingine achukue injini. .. wakati wote huo wa kufanya hii restructuring je adui yako atakuachia nafasi ujipange kwanza ili ukiwa tayari muanze vita tena?

Tanzania VS Covid -19

Dk ni ya 30 ya mchezo, Tanzania kashafanya Sub mbili, CoVID bado kakomaa... wacha tuone.

(Stay Home)
 
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema serikali haijatoa taarifa za mwenendo wa ugonjwa wa Covid-19 nchini kwa wiki moja sasa kutokana na uwepo wa zoezi la uhakiki wa maabara ya taifa na uhakiki huo utakapokamilika, taarifa zitaendelea kutolewa.

AzamTV
Na mavifo yote haya yanayotokea ghafla bado anazungusha viuno tu! Ila tuna kila aina ya viashiria kuwa hatuna serikali makini.
 
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema serikali haijatoa taarifa za mwenendo wa ugonjwa wa Covid-19 nchini kwa wiki moja sasa kutokana na uwepo wa zoezi la uhakiki wa maabara ya taifa na uhakiki huo utakapokamilika, taarifa zitaendelea kutolewa.

AzamTV
Mmmmmm! Siasa za kikomunisti kwani waliacha kutangaza hata kabla ya hotuba tata.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom