Waziri Ummy: Ni Marufuku watendaji na wenyeviti wa vijiji nchini kuchangisha michango bila kibali, awasimamisha mtendaji na m/kiti wa Kijiji sengerema

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,904
Sengerema .

Waziri wa Tamisemi Ummy Mwalimu ameagiza kukamatwa na kuwasimamisha kazi watendaji wawili akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamlilio wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza, kwa madai ya kuwachangisha wananchi kwa nguvu fedha za maendeleo.

Viongozi hao ni Mariamu Mgunda ambaye ni mtendaji wa kijiji hicho pamoja na mwenyekiti Mateso Shibayi.

Agizo hilo amelitoa leo Jumamosi Agosti 14, 2021 baada ya wananchi kulalamikia mambo wanayofanyiwa.

Baada ya malalamiko hayo, Ummy ameagiza watendaji wote wa vijiji na kata nchi nzima wasichangishe fedha kwa wananchi bila kibali kutoka kwa mkuu wa wilaya husikia.

Mkazi wa Kijiji cha Nyamililo, Sijali Matias amesema, Machi 18 mwaka huu, mtendaji na mwenyekiti huyo walifika nyumbani kwake na kuchukua mbuzi jike.

Amesema baada ya siku tano alikwenda ofisi ya mtendaji na Sh30,000 kwa ajili ya kuchukuwa mbuzi wake lakini kitendo kilichofanyika alikosa amani.

Akijibu malalamiko hayo, mtendaji Mariamu Mugunda alisema michango hiyo walikubalina na wananchi kupitia vikao vyote vya kijiji hicho na hajaenda kinyume na utaratibu.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabriey amesema atafanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo na atakayebainika atafikishwa Mahakamani.
 
Mwenye mbuzi atakuwa CHADEMA
 
Mnnnh. Hapa serikali iwe wazi tu.
1. Zile 20% nguvu za wananchi huwa zinatoka wapi? Haka kakipengele wakatoe.
2. Ili kuondoa haya Sasa serikali ihudumie miradi yote kwa 100% Kama ilivyo Barabara n.k.
3. Local Government kuna mambo mengi Sana yanaendeshwa Locally. Naona kuna Kiongozi hapo aliruka wakati anajua fika kilichofanyika na ndio huwa wahimizaji wakubwa.
Anyway ngoja tuendelee kujenga nchi.
 
Si walikubaliana wenyewe wanananchi kwenye vikao vyao.
Kumbuka mtendaji ni msimamizi tu wa maamuzi au maazimio waliyoyaweka wenyewe wananchi.
Hapa na Mimi napata hofu,huku niliko tumeazimia kila mwananchi achange elfu 10 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa,na soon tunaanza mchakato wa kuwasaka wale wote waliokaidi kulipa ,hapa napata hofu ya kuharibu kibarua changu ,wanasiasa wanakosea Sana kuingilia Mambo ambayo yako kiutendaji,

Kwani Michango hujadiliwa kwenye kikao Cha serikali ya Kijiji,baada ya hapo hupelekwa kwa wananchi kupitia mkutano mkuu ,wananchi wakiupitisha au kuukubali mchango Basi kanuni na taratibu za ukusanyaji mchango huwekwa .

Kabla ya msako ,Jambo Hilo hupaswa kujadiliwa kwenye kamati ya maendeleo ya Kata,ambapo mwenyekiti wa kamati Ni diwani na mtendaji kata Ni katibu,sasa kusimamisha Veo na mwenyekiti wa Kijiji Ni kuwaonea tu.

Wanasiasa acheni kuingilia Mambo ya kiutendaji,mnakwamisha maendeleo.
 
Back
Top Bottom