Waziri Ummy Mwalimu: Watanzania tujivunie matunda ya Muungano wetu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Ummy Mwalimu amesema watanzania wote wanao wajibu wa kujivunia matunda ya Muungano ikiwa ni pamoja na miradi ya Maendeleo inayotekekezwa pande zote mbili za Muungano.

Akiwa visiwani Zanzibar katika siku yake ya pili ya ziara ya kikazi, Waziri Ummy ametembelea miradi ya TASAF na MIVARF ikiwa ni pamoja na Kituo cha Afya Kianga, Bwalo la Wanafunzi na Soko la Mbogamboga la Kinyasini.

Amesema pamoja na changamoto zilizopo zipo fursa kwa Watanzania kujiletea maendeleo na ustawi wao, kwa kuwa kuwepo kwa fursa hizo kumeleta tashwishi na matarajio makubwa kwa wananchi katika kuendeleza mafanikio yaliyopatikana na kuchochea mafanikio katika maeneo mengine kwa maslahi ya Taifa

“Tumejionea wenyewe mpango huu mkubwa wa kunusuru kaya maskini kupitia Muungano wetu unatekelezwa na pande zote mbili na haya ndio matunda ya Muungano kuhakikisha miradi mikubwa inatekelezwa pande zote mbili” Ummy alisisitiza.

Aimetaja baadhi ya Miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali zeto mbili yenye kunufaisha wananchi wake iko katika Nyanja za Elimu; Afya; Masoko; Maji; Mazingira pamoja na Usafiri na Usafirishaji.

“Kama mnavyofahamu tunataka kuulinda, kudumisha na kuuimarisha muungano wetu kwani ndio umoja wa watanzania, ndio usalama wa watanzania na ndio amani ya watanzania wote” Alisisitiza Waziri

Kupitia mradi wa MIVARF takriban masoko 16 yamejengwa Tanzania nzima kati ya hayo masoko 4 yamejengwa Zanzibar, kituo cha afya Kianga chenye kunufaisha takriban Shehia 3 za Kianga, Dole na Mazizini huku kikihudumia takribani wakazi 19,840, ujenzi wa madarasa katika Skuli za Fujoni na Mahonda ambazo zimeweza kutatua changamoto za elimu.

Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa ni vyema tukatumia ipasavyo fursa zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar kwa kuleta maendeleo yatakayoinua hali ya uchumi wa Watanzania, na kutoa rai ya kuulinda, kuuimarisha na kuudumisha Muungano wetu kwani ni dira ya mafanikio yetu.

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza la Uwakilishi (Mwera) Mihayo Juma N’hunga ameshukuru Serikali kwa kupata kusogeza huduma zenye kugusa Maisha ya wananchi.
 
Back
Top Bottom