Waziri Ummy Mwalimu usiishie kwa Mkurugenzi aliyeiba mabati huku Siha kuna Ndaki aliiba mbao

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Serikali kupitia waziri wa Tamisemi,Ummy Mwalimu hivi karibuni ilichukua uamuzi wa kumsimamisha kazi aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Gairo,Asajile Mwambambale kwa tuhuma za wizi wa mabati akiwa na wenzake wakati akiwa mkurugenzi wa halmashauri ya Kilosa.

Kabla ya kusimamishwa mkurugenzi huyu alikamatwa na jeshi la polisi na kisha kuhojiwa na sasa anachunguzwa na vyombo mbalimbali vya dola juu ya tuhuma hizo huku akiwa amepisha ofisini kwake.

Katika Siku za hivi karibuni shutuma na tuhuma mbalimbali kama matumizi mabaya ya madaraka,rushwa na ufisadi kwa kipindi cha hivi karibuni zimekuwa zikimwandama aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Ndaki Muhuli.

Ndaki ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa halmashauri ya Kakonko mkoani Kigoma anaandamwa na tuhuma mbalimbali kama ile ya kufanya biashara ya mbao kupitia msitu wa Sanya Forest ambazo alikuwa akiiuzia halmashauri hiyo ili zitumike katika miradi mbalimbali wilayani humo wakati akiwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo.

Taarifa kutoka wilayani humo zinaeleza kwamba Ndaki alitumia cheo chake cha ukurugenzi kuamuru apewe mbao hizo bila kuzilipia mapato na kisha kuiuzia halmashauri hiyo ili zitumike katika miradi mbalimbali kama ujenzi wa hospitali ya wilaya ili zitumike kinyume na sheria .

Lakini mbali na tuhuma hizo taarifa hizo zinadaia ya kwamba hivi karibuni kabla ya kuhamishwa inasemekana alikodisha malori kutoka kampuni ya Dangote kubeba mbao hizo na haikujulikana alikuwa akizipeleka wapi mpaka sasa haijulikani zilipo.

Mbali na tuhuma hizo Bwana Ndaki amekuwa akituhumiwa kwamba siku chache kabla ya kuhamishwa aliwaamuru wakusanya ushuru mbalimbali katika halmashauri hiyo kumpelekea fedha zote walizokusanya kwa kutumia mfumo wa POSS zikiawa taslimu(cash) huku akiwataka waseme kuwa mashine ziliharibika.

Mbali na tuhuma hizo Ndaki anatuhumiwa kufanya biashara ya nyama pori kutoka wilayani Siha na kisha kuzipeleka wilayani Kiteto ambako alikuwa na bucha mbalimbali za nyama ya pori.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Ndaki alikuwa akitumia gari ya serikali kupeleka bidhaa hizo wilayani Kiteto huku akimtumia dereva wa halmashauri hiyo ambaye alikuwa ameshastaafu na kisha kuongezewa mkataba kinyemela anayetambuoika kwa majina ya John Sanai Maimu .

Lakini mbali na tuhuma hizo Ndaki anatuhumiwa kuchukua fedha za halmashauri hiyo na kisha kununua machine ya kufyatulia matofali ambayo alikuwa akiyauza kwa watu binafsi na kwenye baadhi ya miradi ya halmashauri hiyo.

Tangu tuhuma hizi zisambae sio serikali wala wizara ya Tamisemi hatujasikia tamko lolote na hii inaleta ukakasi ndani ya serikali hivyo ushauri wangu kwa serikali ni muda sasa wa kujitokeza hadharani kusema chochote juu ya haya yanayoendelea wilayani Siha.

Mwisho.

View attachment 1935021
IMG_20210829_225842_110.JPG
 
Mpk pos hla zinapigwa khaah! Hpo ss kupatwa kw kiongoz. Maneno meengi kumbe matendo yke hayakuw yakishujaa km alivyojinadi?! Kazi iendelee kw kwl
 
Back
Top Bottom