Waziri Ummy Mwalimu tusaidie Bima ya Afya ihudumie mpaka Checkup ya Kawaida

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,160
1,492
Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya (MB), Watanzania wengi wanaumwa na hawajitambui, Watanzania wengi hawana utaratibu wa kufanya checkup kujua Afya zao.

Bahati mbaya sana gharama za checkup zimeondolewa katika bima ya Afya. Gharama za kumuona daktari na kufanya checkup ya kawaida bado sio rafiki sanaa.

Serikali ya Awamu ya sita, katika sekta ya Afya imejenga vituo vya kutolea huduma za Afya kribu kila kijiji , Serikali imesogeza huduma za Afya kwa Wananchi, Watalaamu wa huduma za Afya wapo, tunashukuru dawa zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

Mh. Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, kazi unayofanya ni kubwa, Mungu aendeleee kukusimamia uweze kuhudumia Watanzania.

Ombi langu kwako Mh. Waziri wa Afya , Ummy Mwalimu, angalia namna ya kuwasaidia Watanzania tuweze kufanya checkup (normal checkup) kwa kutumia bima ya Afya.

#Mungu ibariki Tanzania
#Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
 
Alikudanganya nani kuwa lengo ni kukuhudumia wewe?

Bima ya Afya isiwe lazima, Serikali msitake faida tu, wekezeni

Wanatakiwa wajiunge walio wazima ili kampuni lipate pesa. Maselule nani anawahitaji?
 
Back
Top Bottom