Waziri Ummy Mwalimu, tupia macho kituo cha afya Igoma

Chimo

JF-Expert Member
Aug 31, 2008
714
360
Kwako dada yangu Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, haitoshi na haitatosha kukuelezea mabaya na maovu yanayotokea kwenye kituo cha afya Igoma, Mwanza.

Naweza kukesha na kuandika mabaya hayo siku mbili au tatu na nisimalize yote.

Kwa ufupi, bora kituo hicho kifungwe kinaitia aibu serikali na Wizara yako.

Kuanzia mlinzi wa getini mpaka wauguzi ni wanyanyasaji, watesaji na wauaji na hawapaswi kuendelea kuwepo uraiani, walitakiwa wawe Butimba gerezani.

Imagine mimi ni dereva nilikodishwa tu kupeleka mgonjwa kwa muda wa dakika 20 ila niliyoyaona nililia nikasamehe na nauli.

MUUGUZI MKUU WA WILAYA YA ILEMELA
MGANGA MKUU WA WILAYA YA ILEMELA
MGANGA MKUU WA MKOA WA MWANZA

Ni AIBU KABISA!

Mlinzi wa getini, mwanamke, anatukana wagonjwa anafukuza wajawazito vitandani anagoma kufungua getini, mgonjwa mahututi yupo kwenye bodaboda, ana amri zaidi ya mkuu wa kituo cha afya - Aibu! Aibu! Aibu!

Inasikitisha sana Waziri, hizo ni pesa zetu wananchi tunalipa kodi ya kila aina; serikali yako ituhudumie kwanini mnashindwa kuweka utaratibu mzuri kwa vituo vya umma ilihali tunalipia huduma hizo? Ya Igoma haya tofauti na Hospital ya Mkoa Sekou Toure.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hicho sijui ni kituo ama zahanati, ni wajinga. Mwaka 2017 nilimpeleka wife kupma. Sisemi uongo, nilikaa masaa mawili bila kuona mgonjwa/muhitaji yeyote akiingia ndani. Kulikuwa na nesi mmoja na mzee wanapiga stori. Wagonjwa wanatukanwa mno, hata huruma tu wale wanawake hawana.
 
Andika barua kwa mkuu wa mkoa wa mwanza anaitwa john mongela, hicho kituo tulishaachaga kwenda hapo wanaenda watoto kupima uzito tu na mtu ambae hawezifika hata sekoture.
 
Mwenye Namba ya Mkuu wa Mkoa Mongella Tafadhali anitumie Inbox

Sent using Jamii Forums mobile app
Juzi nimeenda na malikia wangu zahanati moja inaitwa Itensa ili aanze kliniki nakutana na wajawazito wengine wanarudi wanaambiwa muda umeisha nami nilipofika nikajibiwa hivyo hivyo.

Kesho yake nikaenda hospitali ya Igawilo jijini mbeya nikiwa na mke wangu nikamkuta muuguzi yupo lakini muda ule wa saa 5 alichosema ni kuwa mmechelewa ondokeni.

Sasa najipanga niende hospitali binafsi maarufu kama Sijabaja ili kupata huduma.Sasa ninaposikia haya nagundua kuwa kumbe ni mwendo wa sare mpishano ni mdogo sana.

Wauguzi ni watu wazuri lakini pia ndiyo watu wanaoongoza kwa ukatili na majibu mabovu duniani.
Mwaka 1999 kaka yamgu alivunjika mkono nikiwa naye hospitali ya mkoa Rukwa madaktari walifika na kuvamia mkono kuunyosha bila ganzi alipolalamika sana kwa maumivu mmoja kati yao akasema unahitaji tutumie ganzi kwani ulipoumia ulihitaji ganzi yaani sintosahau kabisa.

Kweli duniani mapito tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnataka kwendabali sana!Hata kwa mganga mkuu wa Manispaa tu inatosha na mtaona hatua zinachukuliwa.

Ila nashangaa pia kwani eneo hilo halina diwani?Maana madiwani wana nafasi kubwa ya kuongea na mkubwa yeyote iwapo hawaoni hatua zikichukuliwa.

Nawaomba wananchi wenzangu muwe mnajua kufuata taratibu za kudai haki zenu.
Nina uhakika hilo suala lenu ni dogo sana wala halihitaji mkuu wa mkoa.Mganga mkuu wa Manispaa tu ana nguvu kubwa sana ya kilimaliza kabisa.Na wakimshinda mganga mkuu wa Manispaa ina maana hata kazi hawaitaki.
Mwenye Namba ya Mkuu wa Mkoa Mongella Tafadhali anitumie Inbox

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwako dada yangu Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, haitoshi na haitatosha kukuelezea mabaya na maovu yanayotokea kwenye kituo cha afya Igoma, Mwanza.

Naweza kukesha na kuandika mabaya hayo siku mbili au tatu na nisimalize yote.

Kwa ufupi, bora kituo hicho kifungwe kinaitia aibu serikali na Wizara yako.

Kuanzia mlinzi wa getini mpaka wauguzi ni wanyanyasaji, watesaji na wauaji na hawapaswi kuendelea kuwepo uraiani, walitakiwa wawe Butimba gerezani.

Imagine mimi ni dereva nilikodishwa tu kupeleka mgonjwa kwa muda wa dakika 20 ila niliyoyaona nililia nikasamehe na nauli.

MUUGUZI MKUU WA WILAYA YA ILEMELA
MGANGA MKUU WA WILAYA YA ILEMELA
MGANGA MKUU WA MKOA WA MWANZA

Ni AIBU KABISA!

Mlinzi wa getini, mwanamke, anatukana wagonjwa anafukuza wajawazito vitandani anagoma kufungua getini, mgonjwa mahututi yupo kwenye bodaboda, ana amri zaidi ya mkuu wa kituo cha afya - Aibu! Aibu! Aibu!

Inasikitisha sana Waziri, hizo ni pesa zetu wananchi tunalipa kodi ya kila aina; serikali yako ituhudumie kwanini mnashindwa kuweka utaratibu mzuri kwa vituo vya umma ilihali tunalipia huduma hizo? Ya Igoma haya tofauti na Hospital ya Mkoa Sekou Toure.

Sent using Jamii Forums mobile app
Igoma ipo wilaya ya Nyamagana, City council wanahusika hapa na sio Ilemela Municipal Council

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom